Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kabla hujaingia kwenye hiyo unayoita kunikumbusha, nakusihi jipe muda kutafuta taarifu na kuzisoma na kuzielewa...

Kaisome Jeisuti ni nini na ipo kwaajili ya nini? Kasome mashirika tanzu ya RC... Kija njoo ukae ufunzwe hapa mkuu... Juu ya haya ninayo ya kuwafunza wengi kuliko mimi kujifunza...

Labda uniambie unataka kujua nini kuhusu Jesuits, hivi unafikiri we ndio mbobezi unayejua zaidi, JF ni kichaka kuna kila aina ya watu humu, kwa kifupi ndugu yangu Yericko Nyerere , unaweza kuwa mzuri kwenye vitu vingi lakini kwa hili la Jesuits uko wrong,

Anyway tusitoke nje ya maada, japo nakuomba sana ujitahidi kuandika facts itakusaidia na itawasaidia wanaosoma humu
 
Sources zote zipo kwenye kitabu yaani nyaraka zote... Jipe muda mzee wangu ukisome kitabu hiki
Yericko,
Uandishi una sheria zake acha ubishi utakuwa mjinga daima.

Ilikuwa hizo, "source," ziwe kwenye kurasa kama, "notes,"...mathalan "angalia,"...au "opt cit," au "ibid," au "passim..."

Hivi ndivyo kazi za kisomi zinavyoandikwa vinginevyo utageuka kuwa kichekesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaaa asante sana... Review si kama pombe za ngomani maalim.

Nitafurahi ukiwa wewe kwakuwa ninakuwa tayari nina matokeo ya review yako hata kabla ya kukamilisha review yenyewe....

Umepata chain ya Uhuru wa Tanganyika, Julius Nyerere, Kanisa katoliki, Kanisa Anglikana, Malkia Elizaberth, wazee wa Dar na UNO?
Yericko,
Mimi sina umuhimu katika uandishi wako mimi katika hili nakuwa msomaji
kama wasomaji wengine.

Ikiwa patakuwa na makosa atakaebeba fedheha ni wewe mwandishi.

Ila nakuhurumia kwa hiyo jeuri uliyokuwanayo wakati ''ideology,'' ni
shida kuiandika.

Hakika inanijia simanzi.

Nina mengi ningeweza kukufunza na ukawa unajua lakini naona inazidisha
kibri na kejeli.
 
Labda uniambie unataka kujua nini kuhusu Jesuits, hivi unafikiri we ndio mbobezi unayejua zaidi, JF ni kichaka kuna kila aina ya watu humu, kwa kifupi ndugu yangu Yericko Nyerere , unaweza kuwa mzuri kwenye vitu vingi lakini kwa hili la Jesuits uko wrong,

Anyway tusitoke nje ya maada, japo nakuomba sana ujitahidi kuandika facts itakusaidia na itawasaidia wanaosoma humu
Kituko,
Huyu hajaandika kitabu kesha kuwa bingwa haelezwi kitu.

Kitabu chenyewe hakina mhariri na hata unapomwonyesha
makosa ya, ''spelling,'' ''facts'' hataki kusikia mtu kama huyu
mwache anajiangamiza kwa mikono yake mwenyewe.

Kitabu cha Amazon kinachapwa Kariakoo.

Kitabu cha Amazon hakina ''publisher ambae ndiye angeshughulikia
masoko nk. nk.

Kitabu cha Amazon hakifanyiwa, ''review,'' wala, ''catalogue,'' nk.

Hiki kitakuwa kitabu cha aina yake kabisa.
Tusibirini...
 
Mzee wangu wewe ni mswahili mzuri, umefunzwa kusherehekea mimba au kusherehekea mtoto?
 
Yericko,
Uandishi una sheria zake acha ubishi utakuwa mjinga daima.

Ilikuwa hizo, "source," ziwe kwenye kurasa kama, "notes,"...mathalan "angalia,"...au "opt cit," au "ibid," au "passim..."

Hivi ndivyo kazi za kisomi zinavyoandikwa vinginevyo utageuka kuwa kichekesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dunia inabadilika mzee wangu, vitabu haviandikwi kwa mtindo wenu wazee enzi zenu, hizi ni enzi zetu. Vitabu vinasimama na mambo mawili, vielele na marejeo tu. Hata mambo ya wasifu wa mwandishi hayo tumeondoka huko, bali tunabeba kitu kiitwacho maoni ya watu mashuhuri au maarifu....
 
Labda uniambie unataka kujua nini kuhusu Jesuits, hivi unafikiri we ndio mbobezi unayejua zaidi, JF ni kichaka kuna kila aina ya watu humu, kwa kifupi ndugu yangu Yericko Nyerere , unaweza kuwa mzuri kwenye vitu vingi lakini kwa hili la Jesuits uko wrong,

Anyway tusitoke nje ya maada, japo nakuomba sana ujitahidi kuandika facts itakusaidia na itawasaidia wanaosoma humu
Si nongwa maalim, liujazalo moyo ndilo ulijualo... Kitabu hiki kimeeleza kwa undani Jeisuti na shughuli zao na usharika wao katika uhuru wa nchi nyingi duniani
 
Dunia inabadilika mzee wangu, vitabu haviandikwi kwa mtindo wenu wazee enzi zenu, hizi ni enzi zetu. Vitabu vinasimama na mambo mawili, vielele na marejeo tu. Hata mambo ya wasifu wa mwandishi hayo tumeondoka huko, bali tunabeba kitu kiitwacho maoni ya watu mashuhuri au maarifu....
Yericko uandishi haujabadilika ila wewe huna ujuzi huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[B]Mohamed Said[/B], naomba jibu kwa swali moja tu lakini kabla naomba nitoe ufafanuzi kidogo kulingana na maandishi yako yanayosema TANU iliasisiwa mwaka 1954 na Mwalimu Nyerere akachaguliwa kuwa Rais wake wa kwanza baada ya kumshinda kipenzi cha wajumbe Abdul Sykes. Wakati Mwalimu anachaguliwa asilimia kubwa ya wajumbe, kulingana na maandishi yako, walikuwa Waislaam ikiwa ni pamoja na wazee wako...

Swali, toka mwaka 1954 hadi tunapata uhuru 1961 (miaka 7) udini ulipenyezwa vipi katika harakati za kudai uhuru, nani aliendesha hizo juhudi za kudhoofisha ushiriki wa Waislaam, ambao ndio walikuwa wengi, hadi kuzima nguvu kubwa walizokuwa nazo ndani ya TANU? Je ni Nyerere huyo huyo aliendesha kampeni akishirikiana na wakoloni kuhakikisha sauti za Waislaam hazisikiki tena wala kupata nafasi ya uongozi ndani ya TANU?

Je huko majimboni kulikuwa na harakati za kuhakikisha Waislaam hawachaguliwi kuongoza matawi ya TANU hata kama wanajitokeza? Mathalani sehemu kama Jimbo la Ziwa (Lake Province), Jimbo la Magharibi (Western Province), Jimbo la Nyanda za juu Kusini (Southern Highlands Province), Jimbo la Kaskazini (Northern Province), Jimbo la Kati (Central Province), Jimbo la Kusini (Southern Province) na Jimbo la Mashariki (Eastern Province)...nani aliendesha harakazi hizo?

Ni mwaka gani Abdul Sykes alijitoa TANU na sababu za kujitoa. Je baada ya kujitoa TANU hakujishughulisha tena na mambo ya siasa? Je ni lini mzee wako alijitoa TANU na baada ya kujitoa hakujishughulisha tena na siasa? Je yawezekana kwamba harakati za kudai uhuru ziliposhika hawakuweza kwenda na kasi hizo? Je yawezekana kwamba wasomi walipoanza kujiunga na TANU wazee wako walipatwa na mfadhaiko kwa elimu yao?

Sasa fikiria walivyojisikia harakati zilipopamba moto mwaka wa uhuru ulipokaribia na walivyosononeka wakijikuta nafasi zao zinachukuliwa na vijana wasomi nchi nzima. Unadhani walifurahia hali hiyo? La hasha yawezekana walijenga chuki mioyoni mwao na kuanza kutafuta wa kuwabebesha lawama kwa mgongo wa dini. Halafu fikiria ukazaliwa, ukakuta na ukakulia hali hiyo ukisikiliza malalamiko yao toka ukiwa mdogo...kila siku ni hayo hayo.

Ukaapa lazima siku moja ulipize kisasi kwa yanayowakwaza wazee wako, ukaanza harakati na kwa mgongo wa dini hukupata taabu kuwapata wafadhili na wafuasi. Ukaamua ipo njia moja tu ya kulipiza kisasi...kuandika ulichokibatiza historia ya kweli ya Tanganyika. Ukasubiri wazee watangulie mbele ya safari na hata wachache waliokuwepo hukuona umuhimu wa kuwatafuta na kupata ushuhuda wao wakiwa bado hai ingawaje walikuwa wengi tu.

Kuna wakati tulikuuliza kwa nini huwahoji wazee wa Kiislaam waliokuwa kwenye nafasi za juu wakati huo. Nakumbuka tulikuomba umhoji hata Marehemu Rashidi Mfaume Kawawa aliyekuwa mtu wa karibu sana na Mwalimu na wengine kadhaa lakini hukutaka. Ushahidi wote ulio nao ni wa kuhadithiwa na wazee wako na kila moja wetu anajua wazee wetu wanavyokoleza mambo hasa pale wanapoelezea yanayowakera. Pole sana [B]Mohamed Said[/B] na kwaheri.
 
Mag 3 yote niliyotaka kusema nimeyasema katika kitabu sasa yapata miaka 20 imepita soma kitabu changu utausoma ubongo wangu. Sina zaidi hivi sasa isipokuwa kuandika yaliyotokea katika miaka ya uhuru. Soma "Tanzania a Nation Without Heroes," hii ni paper yangu niliwasilisha Nairobi French Institute 2014.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"
Mag3, post: 22907209, member: 10873"][B]Mohamed Said[/B], Mwaka 1954 na Mwalimu Nyerere akachaguliwa kuwa Rais wake wa kwanza baada ya kumshinda kipenzi cha wajumbe Abdul Sykes. Wakati Mwalimu anachaguliwa asilimia kubwa ya wajumbe, kulingana na maandishi yako, walikuwa Waislaam ikiwa ni pamoja na wazee wako...
Ilikuwaje ''wazee wetu'' wakamsaliti kipenzi na mwasisi Abdul Sykes
1954 hadi tunapata uhuru 1961 (miaka 7) udini ulipenyezwa vipi katika harakati za kudai uhuru, nani aliendesha hizo juhudi za kudhoofisha ushiriki wa Waislaam, ambao ndio walikuwa wengi, hadi kuzima nguvu kubwa walizokuwa nazo ndani ya TANU?
Jamvi kimyaa linamsubiri ''mhadhiri''. Hapa ni maelezo tu ya kina si picha wala nini
Ni mwaka gani Abdul Sykes alijitoa TANU na sababu za kujitoa. Je baada ya kujitoa TANU hakujishughulisha tena na mambo ya siasa?
Mkuu!! usichafue historia ya 1929 hadi 1954 kisha kuruka hadi msiba 1968. Hii miaka kati ya 1954 hadi 1961 usiulize!
Je ni lini mzee wako alijitoa TANU na baada ya kujitoa hakujishughulisha tena na siasa?
Neno hili, hapa AMNUT sijui kama inakwepeka
Je yawezekana kwamba harakati za kudai uhuru ziliposhika hawakuweza kwenda na kasi hizo? Je yawezekana kwamba wasomi walipoanza kujiunga na TANU wazee wako walipatwa na mfadhaiko kwa elimu yao?
Kwa mujibu wa Mohamed, kura tatu wazee walikataa kwani nia ya Nyerere ilikuwa kuingiza wasomi! Labda kuna maelezo mengi. Jamvi kimyaaa linamsubiri Mudir
 
[B]Mohamed Said[/B], naomba jibu kwa swali moja tu lakini kabla naomba nitoe ufafanuzi kidogo kulingana na maandishi yako yanayosema TANU iliasisiwa mwaka 1954 na Mwalimu Nyerere akachaguliwa kuwa Rais wake wa kwanza baada ya kumshinda kipenzi cha wajumbe Abdul Sykes. Wakati Mwalimu anachaguliwa asilimia kubwa ya wajumbe, kulingana na maandishi yako, walikuwa Waislaam ikiwa ni pamoja na wazee wako...

Swali, toka mwaka 1954 hadi tunapata uhuru 1961 (miaka 7) udini ulipenyezwa vipi katika harakati za kudai uhuru, nani aliendesha hizo juhudi za kudhoofisha ushiriki wa Waislaam, ambao ndio walikuwa wengi, hadi kuzima nguvu kubwa walizokuwa nazo ndani ya TANU? Je ni Nyerere huyo huyo aliendesha kampeni akishirikiana na wakoloni kuhakikisha sauti za Waislaam hazisikiki tena wala kupata nafasi ya uongozi ndani ya TANU?

Je huko majimboni kulikuwa na harakati za kuhakikisha Waislaam hawachaguliwi kuongoza matawi ya TANU hata kama wanajitokeza? Mathalani sehemu kama Jimbo la Ziwa (Lake Province), Jimbo la Magharibi (Western Province), Jimbo la Nyanda za juu Kusini (Southern Highlands Province), Jimbo la Kaskazini (Northern Province), Jimbo la Kati (Central Province), Jimbo la Kusini (Southern Province) na Jimbo la Mashariki (Eastern Province)...nani aliendesha harakazi hizo?

Ni mwaka gani Abdul Sykes alijitoa TANU na sababu za kujitoa. Je baada ya kujitoa TANU hakujishughulisha tena na mambo ya siasa? Je ni lini mzee wako alijitoa TANU na baada ya kujitoa hakujishughulisha tena na siasa? Je yawezekana kwamba harakati za kudai uhuru ziliposhika hawakuweza kwenda na kasi hizo? Je yawezekana kwamba wasomi walipoanza kujiunga na TANU wazee wako walipatwa na mfadhaiko kwa elimu yao?

Sasa fikiria walivyojisikia harakati zilipopamba moto mwaka wa uhuru ulipokaribia na walivyosononeka wakijikuta nafasi zao zinachukuliwa na vijana wasomi nchi nzima. Unadhani walifurahia hali hiyo? La hasha yawezekana walijenga chuki mioyoni mwao na kuanza kutafuta wa kuwabebesha lawama kwa mgongo wa dini. Halafu fikiria ukazaliwa, ukakuta na ukakulia hali hiyo ukisikiliza malalamiko yao toka ukiwa mdogo...kila siku ni hayo hayo.

Ukaapa lazima siku moja ulipize kisasi kwa yanayowakwaza wazee wako, ukaanza harakati na kwa mgongo wa dini hukupata taabu kuwapata wafadhili na wafuasi. Ukaamua ipo njia moja tu ya kulipiza kisasi...kuandika ulichokibatiza historia ya kweli ya Tanganyika. Ukasubiri wazee watangulie mbele ya safari na hata wachache waliokuwepo hukuona umuhimu wa kuwatafuta na kupata ushuhuda wao wakiwa bado hai ingawaje walikuwa wengi tu.

Kuna wakati tulikuuliza kwa nini huwahoji wazee wa Kiislaam waliokuwa kwenye nafasi za juu wakati huo. Nakumbuka tulikuomba umhoji hata Marehemu Rashidi Mfaume Kawawa aliyekuwa mtu wa karibu sana na Mwalimu na wengine kadhaa lakini hukutaka. Ushahidi wote ulio nao ni wa kuhadithiwa na wazee wako na kila moja wetu anajua wazee wetu wanavyokoleza mambo hasa pale wanapoelezea yanayowakera. Pole sana [B]Mohamed Said[/B] na kwaheri.
Akikujibu hapa mimi nabadili uraia
 
Mag 3 yote niliyotaka kusema nimeyasema katika kitabu sasa yapata miaka 20 imepita soma kitabu changu utausoma ubongo wangu. Sina zaidi hivi sasa isipokuwa kuandika yaliyotokea katika miaka ya uhuru. Soma "Tanzania a Nation Without Heroes," hii ni paper yangu niliwasilisha Nairobi French Institute 2014.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee Mohamed Said, Kwa hakika humtendei haki mzee mwenzio Mag3, hebu jibu maswali yake hapo
 
Mzee Mohamed Said, Kwa hakika humtendei haki mzee mwenzio Mag3, hebu jibu maswali yake hapo
Yericko,
Mbona najibu maswali mengi humu na kuweka rejea zote?
Tatizo ni kuwa hamkubaliani na majibu na inaelekea hata hizo rejea hamsomi.

Hli swali la tatizo la udini wala si la kuuliza nyie kwani wanaoshutumiwa kwa hilo
wamefahamishwa na kitabu kikaandikwa, ''Mwembechai Killings...'' kitabu hiki cha
Prof. Njozi kimepigwa marufuku na serikali wakati wa utawala wa Rais Mkapa.

Tusiende mbele zaidi.
Someni aliyosema Prof. Njozi kisha Mag3 arejee tujadili:
http://www.islamtanzania.org/mwembechai/mchai-chap1.pdf

Chapter zote zinapatika search google: ''Mwembechai Killings...''

NB: Mag3 kakosea kuliuliza swali kwani kalitia mahali sipo.
Afanye rejea katika kitabu cha Abdul Sykes asome:

''The First Muslim Congress 1962''
''The Second Muslim Congress 1963''

Baada ya hapo ndipo swali litaaingia mahali pake vizuri.
 
Dunia inabadilika mzee wangu, vitabu haviandikwi kwa mtindo wenu wazee enzi zenu, hizi ni enzi zetu. Vitabu vinasimama na mambo mawili, vielele na marejeo tu. Hata mambo ya wasifu wa mwandishi hayo tumeondoka huko, bali tunabeba kitu kiitwacho maoni ya watu mashuhuri au maarifu....
Yericko,
Kazi yangu ya mwisho ni hii, ''Dictionary of African Biography,'' Oxford University Press, New York, 2011.
Hebu tazama ilivyo kuna, ''bibliography,'':

DSCN1142.JPG

Sijaona katika, ''volume,'' zote sita maoni ya mtu yeyote mashuhuri ndani mna
kazi za kisomi na rejea za watu wajuzi katika historia ya Afrika.

Nami niliingizwa katika mradi huu kwa kuwa nimeandika mengi katika historia
ya Tanganyika wala hapa Tanzania hakuchukuliwa mtu kwa umaarufu.
 
Mkuu Mag3 menine yote utaona kurasa nzima ya kitabu inawekwa hapa
Maswali yako unaambiwa ukasome vitabu

Mohamed maswali ya Mag3 yapo wazi kabisa tena akikunukuu katika vitabu vyako
Msomaji rejea bandiko [HASHTAG]#630[/HASHTAG]

1. ''TANU iliasisiwa mwaka 1954 na Mwalimu Nyerere akachaguliwa Rais wa kwanza baada ya kumshinda kipenzi cha wajumbe Abdul Sykes. Wakati Mwalimu anachaguliwa asilimia kubwa ya wajumbe, kulingana na maandishi yako, walikuwa Waislaam ikiwa ni pamoja na wazee wako...''

Nini kilitokea ikafikia mahali wajumbe wakamtosa Mwasisi Abdul

2.''Swali, 1954 hadi tunapata uhuru 1961 (miaka 7) udini ulipenyezwa vipi katika harakati za kudai uhuru, nani aliendesha hizo juhudi za kudhoofisha ushiriki wa Waislaam waliokuwa wengi, hadi kuzima nguvu kubwa walizokuwa nazo ndani ya TANU? Je ni Nyerere huyo huyo aliendesha kampeni akishirikiana na wakoloni kuhakikisha sauti za Waislaam hazisikiki tena wala kupata nafasi ya uongozi ndani ya TANU''?

3. ''Je huko majimboni kulikuwa na harakati za kuhakikisha Waislaam hawachaguliwi kuongoza matawi ya TANU hata kama wanajitokeza? Mathalani (Lake Province), (Western Province), (Southern Highlands Province), (Northern Province), (Central Province), J(Southern Province) na Jimbo la Mashariki(Eastern Province)...nani aliendesha harakazi hizo?''

4. a) Ni mwaka gani Abdul Sykes alijitoa TANU na sababu za kujitoa.
b) Je baada ya kujitoa TANU hakujishughulisha tena na mambo ya siasa?
c)Je ni lini mzee wako alijitoa TANU na baada ya kujitoa hakujishughulisha tena na siasa?
d)Je yawezekana kwamba harakati za kudai uhuru ziliposhika hawakuweza kwenda na kasi hizo?
e)Je yawezekana kwamba wasomi walipojiunga na TANU wazee wako walipatwa na mfadhaiko kwa elimu yao?

5. Swali binafsi
Nani alianzisha AMNUT na kwanini haikuungwa mkono na wazee wako baada ya kugundua Nyerere si miongoni

Haya ni maswali machache niliyoyanukuu kutoka bandiko la Mag3 na swali binafsi namba 5, hayahitaji reference ya kitabu cha Njozi, yametoka katika kitabu chako mwenyewe.

Ukumbi kimyaaa!! unakusubiri mhadhiri
 
Yericko,
Mbona najibu maswali mengi humu na kuweka rejea zote?
Tatizo ni kuwa hamkubaliani na majibu na inaelekea hata hizo rejea hamsomi.

Hli swali la tatizo la udini wala si la kuuliza nyie kwani wanaoshutumiwa kwa hilo
wamefahamishwa na kitabu kikaandikwa, ''Mwembechai Killings...'' kitabu hiki cha
Prof. Njozi kimepigwa marufuku na serikali wakati wa utawala wa Rais Mkapa.

Tusiende mbele zaidi.
Someni aliyosema Prof. Njozi kisha Mag3 arejee tujadili:
http://www.islamtanzania.org/mwembechai/mchai-chap1.pdf

Chapter zote zinapatika search google: ''Mwembechai Killings...''

NB: Mag3 kakosea kuliuliza swali kwani kalitia mahali sipo.
Afanye rejea katika kitabu cha Abdul Sykes asome:

''The First Muslim Congress 1962''
''The Second Muslim Congress 1963''

Baada ya hapo ndipo swali litaaingia mahali pake vizuri.

Ndugu zangu,
Swali linatakiwa linaloulizwa linatakiwa liwe ndani ya maudhui inayojadiliwa.

Swali linapokuwa kwanza limeulizwa ndani ya ''assumptions,'' swali kama hilo
linakuwa gumu kulijibu.

Swali linatakiwa liwe ndani ya ''facts,'' likiwa nje ya ''facts,'' yaani ukweli hili
pia linakuwa shida kulijibu.

Mathalan muulizaji anasema Abdul Sykes alijitoa TANU.
Wapi yeye kasikia kuwa Abdul alijitoa TANU?

Muulizaji anauliza iweje Abdul alisalitiwa na wapenzi wake?''

Ndipo ninapposema soma kwanza kitabu au naweka sehemu ya kitabu ili
muulizaji asome na afahamu ukweli.

Lakini kubwa ni kuwa waulizaji wanauliza maswali wakiwa katika hali ya kuwa
wameghadhibika na maswali yanajaa lugha za shari.

Hali kama hii inavunja moyo kumjibu muulizaji kama huyo.

WATOTO WA WAPIGANIA UHURU BI. MAUNDA PLANTAN, JUMA MWAPACHU, HAPPY MTAMILA NA KLEIST SYKES WANAPOWAKUMBUKA WAZEE WAO
Mohamed Said June 19, 2016 0
Huyo hapo chini ni Nguruvi3:

Hewalaa, ni kweli ni Juma Mwapachu aliyekuletea habari hiyo. Nimefanya editing ya hoja zangu kwa kuondoa jina Bakari na kuweka Juma, Mwapachu ikibaki pale pale,hoja ni hizi hapa chini

Wanajamvi

Mnakasha umefikia mahali patamu sana.

1. Tunasubiri Mohamed Said atuletee nakala ya draft(rasimu) au katiba ya kuandika au kukopi iliyokuwepo, andikwa au tumiwa na Abdul Sykes kabla ya katiba iliyoandikwa/kopiwa na Nyerere.

2. Tunasubiri Mohamed Said atueleze kabla ya kutangazwa kwa TANU mwaka 1954, jina la TANU lilitumika katika mkutano au mkusanyiko gani ambao Adul Sykes au mwingine nje ya Nyerere

3. Halafu kuna sauti hii ya Mohamed Said katika dakika 51-53 akimueleza mtangazaji wa radio kuwa kabla ya mwaka 1952 hakuna aliyemsikia au kumjua Nyerere. Sikiliza hapa

Kisha usome maneno haya ya Juma Mwapachu aliyempa Mohamed Said atueletee kama zawadi. Lengo lilikuwa kuonyesha sisi 'vichekesho' hatujui na wala hatuna mawasiliano na watu wakubwa kama akina Mwapachu.

Hata hivyo, katika maandishi hayo tunapata habari nyingine ikihusiana na introduction iliyofanywa na Hamza Mwapachu kwa Nyerere katika kile alichosema TAA Leadership

Kumbuka TAA leadership wakati huo ilikuwa chini ya Abdul Sykes, hivyo Hamza Mwapachu alimjulisha Nyerere kwa Abdul Sykes kama sehemu ya TAA leadership.

Soma hapa maneno ya Juma Mwapachu

''I still recall the visit vividly. I was a standard three pupil then and together with my brother Bakari had to sleep in the sitting room leaving our bedroom to the two guests.

Abdul Sykes was then President of TAA and the TAA leadership plus Dar-based political activists who were predominantly Moslems wanted Abdul Sykes to retain the Presidency.

Abdul was eager to secure Hamza's position on the matter given the fact that it was Hamza who introduced Nyerere to the TAA leadership in Dar back in 1949 before Nyerere left for Edinburgh University''
Kwa faida ya wasomaji, tunaweka maneno ya Juma Mwapachu katika tafsiri isiyo rasmi
Tunaomba radhi ikiwa kuna mapungufu yatakayojitokeza. Juma Mwapachu anasema hivi

''Bado nakumbuka kwa uyakinifu. Nilikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu na pamoja na kaka yangu Bakari tulilala sebuleni kuacha chumba kwa wageni wawili.

Abdulwahidi alikuwa Rais wa TAA na uongozi wa TAA pamoja na wanaharakati wa siasa wengi wao wakiwa waislam walitaka Abdul Sykes abaki kuwa Rais

Abdulwahid alikuwa tayari kumuafiki Hamza katika suala hilo katika ukweli kuwa ni Hamza ndiye aliyemtambulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA Dar es salaam mwaka 1949 kabla Nyerere hajaondoka kwenda chuo kikuu Edimburgh''

Ndipo tunakuja kutafuta ufafanuzi kwa Mohamed Said katika hoja ya 4 na 5

4. Mohamed Said , je bado unaamini kuwa kabla ya 1952 hakuna yoyote aliyewahi kumsikia Nyerere katika TAA HQ chini ya Abdulwahid Sykes?

5. Je, maneno ya Juma Mwapachu ni uzushi au ni ukweli?

6. Ikidhihirika J.Mwapachu maneno yake ni sahihi,utaliomba radhi jamvi kwa upotoshaji?

Je, utawaomba radhi wasikilizaji uliowapotosha katika redio na lini utafanya hivyo?

7. Kama maneno yako ni nkweli, je utakuwa tayari kukanusha maneno ya Juma Mwapachu hapa jamvini na kutuomba radhi kwa kutuletea habari zisizo na ukweli?

Na mwisho, Mohamed ajibu hoja hizi, hatuwezi kuburuzwa tu tukubali hata upotoshaji eti kwavile tunataka kujua mengine.

Haina maana kujua mengine ikiwa yapo tusiyoyajua kama haya tunayomuuliza

Mohamed Said, tafadhali sana usihamishe mjadala na kukwepa hoja.

Tunataka kusahihisha historia ya kivukoni kwa ukamilifu wake.

Hatutaki kuwaacha vijana wamechanganyikiwa kwa hoja kinzani.

Tutaendelea baada ya majibu, vinginevyo ukiri makosa kama tunavyokubali ya kivukoni.

Ahsante

Jibu langu:
Nguruvi3,
Ama ingekuwa si kwa kuwa naburudika kufanya mjadala na wewe
mie muda mrefu ningelikwisha nyanyua mikono juu lakini nastarehe
kuongea na wewe.

Allah amekupa kipaji cha aina yake.

Majibu nimekupa kuhusu katiba ya TAA Political Subcommittee kuwa
nyaraka na microfilm zote hazionekani Maktaba ya CCM Ddodoma
na TNA.

Sikuishia hapo nimekueleza kuwa kabla yangu katiba hiyo ilitajwa na
Listowel mwaka wa 1965 na Pratt 1976.

Bado unataka nikuletee hiyo document.
Kama wewe hodari sana mbona huwaulizi CCM nyaraka hizo zilipo?

Lakini ninastarehe katika mnakasha huu kwa kuwa natoa darsa na
wengi wanasoma historia ambapo hawakupatapo kuisikia hata kwa
mbali.

Ndiyo maana narudi hapa tena na tena na tena.
Nakushukuru sana kwa hili.

Sasa nisikilize kwa makini na tuliza ubongo wako nikufunze mbinu
za ''critical analysis'' na kujifunza kusoma katikati ya mistari.

Sitakujibu hayo yote uliyoandika nitakujibu hayo tu ambayo umeweka
rangi nyekundu.

Hamza Mwapachu alimjulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA 1949.

Akili yako mara moja imekwenda kuwa walikuja hadi New Street na
kuzungumza na Mwalimu Thomas Saudtz Plantan aliyekuwa rais na
Clement Mohamed Mtamila aliyekuwa katiibu wa TAA wakati ule.

Lakini ukweli ni kuwa Mwalimu Thomas Plantan na Clement Mtamila
walikuwa hawajapata kukutana na Nyerere hadi alipokuja kwa Abdul
Sykes
1952.

Inawezekana ujulisho huo ulikuwa wa salam za mdomo au wa barua.

Nakuwekea picha nikifanya mahojiano na Bi. Maunda Thoams Plantan
mtangazaji wa kwanza wa kike Tanganyika, Sauti ya Dar es Salaam 1952
na mwalimu wa shule.

Mjukuu wa Affande Plantan na mtoto wa Mwalimu Thomas Saudtz
Plantan
.

HF-E-j6n6D2pW-h8ANND7lxCGUZH73Fhpokdj2U2guz10UUuq33enwGopPRGbfU8HCP7ZcOmNxS-DYu2x5-G9w9vqeN1Qi-nUydPTJmLDHXRS5Py3_84OP_2iecQyjAYflQuA-tfQEQHjxuJ2g-u9pEPK4ambOrJMcYaSt3LVeEiUl_Vmzi9FR4Tc93Ia6bRAnRaPJaZduvvap83uIisUDG_MLkVDJflrFjbfG52G0QkumZ1Q8RLCfhByBEOZSMLvacusXptB2KzZUZsPAhrME9h_gdQ7j3rtG2ZsdVBVOrbgBhPzNax2ekRbIh04vu7ScoezknEk38PM7QP387nntcrgWcDyiEXt0YQPmsByTOz1rAvCc-6WY0lmImew7xIbgp98ByU2R77IA5nGTGz8u56qfwSP6b2qDXMgh6gTm5q6_htGMMiIpNWtqbNLOCELZGKVMJArxuwYYP0S9ZMKK-ZoOBxgFTNE8p2DBcjtpISFD4AdqyqQg2OxjxjVvoqSJPGzr0cyRCfG_8asDxe6xqXSCz2KmWUg2Ndylw8Pz1Fth1LBc2j5yNsnv-qClIy78x38wD3lCWFVEnKTs3aaibrjebomUxY=w480-h360-no

Kushoto Bi. Maunda Plantan na Mwandishi

Katika mazungumzo yetu hakupatapo kunambia kuwa baba yake
alipata hata kwa siku moja kuonana na Nyerere.

Nimezungumza pia na Happy Mtamila hata mara moja hajanieleza
kama baba yake alipata kuonana na Nyerere kabla ya 1952.

20140808_140140-001.jpg

Kulia Bi. Happy Mtamila na Mwandishi
Ningependa kukufahamisha tu kuwa uamuzi wa Nyerere kuacha kazi
ulifanyika nyumbani kwa Clement Mtamila Mtaa wa Kipata na Sikukuu.

Nyumba hii ilikuja kununuliwa na ukoo wa Baharoon ikavunjwa na
sasa ni ghorofa.
SKBStS8549EaS0LxcEjPslwMEGrAB07SVS4y1IX7IQnuFwFpUCQe_v4W3SeizHuDKf2QH3V0WlKT2EqL9kIQq6ednrg2U9uH6k3dlQmT8Mz7rNi1eqPmhE_EFy-NKlDVZ21yEeXyqFYXSn9KOClKilhcl_SRKRbOPBUWWLHdalTWPVz0WEbPArthXt8gVi3tWw2Bt21UquEHBsNTWOQY-NnX7QM5aT7wgpS00oAJGLZ8S02z_uMqJbKzQoFC1lnjt6NuvKlJ5uzUMEASF9-SovB663Ktqcylkzm9xxCARJHv6UgxrXqpU1O0ySM9kTZE3fTaI6aXWfF8jJBamFMv75OHkcKK_6YgSLp6jXkdIPVY0gjgjOF6UiCnxj1wJL3T6RMY2tJpgJFNaJJHxbKjfT6K_Y94ur8JrmjsBuDPrHefHLGHpt9Ys_Vp_gD8_JdI3Prg4jIltelpjXFSUapbD80qO1qU4zLrPk0cVcw3fl1tCD65m-3DiigAOFIUffL8YUwWMkCQhFlrHLX3VkiE9NGA6BrAfqp8ugUPHW1DzZYAtdD1pDyYduZPfJJvI4rsiw-4NqyadZXRvJVFziWXt48Oah53RcI=w986-h657-no

Kushoto: Kleist Abdulwahid Sykes, Ebby Abdulwahid Sykes, Saudtz
Thomas Plantan na Abdulwahid Ally Sykes

Yako mengi hapo chini:
Mohamed Said: WATOTO WA WAPIGANIA UHURU BI. MAUNDA PLANTAN, JUMA MWAPACHU, HAPPY MTAMILA NA KLEIST SYKES WANAPOWAKUMBUKA WAZEE WAO
 
Mkuu Mag3 menine yote utaona kurasa nzima ya kitabu inawekwa hapa
Maswali yako unaambiwa ukasome vitabu

Mohamed maswali ya Mag3 yapo wazi kabisa tena akikunukuu katika vitabu vyako
Msomaji rejea bandiko [HASHTAG]#630[/HASHTAG]

1. ''TANU iliasisiwa mwaka 1954 na Mwalimu Nyerere akachaguliwa Rais wa kwanza baada ya kumshinda kipenzi cha wajumbe Abdul Sykes. Wakati Mwalimu anachaguliwa asilimia kubwa ya wajumbe, kulingana na maandishi yako, walikuwa Waislaam ikiwa ni pamoja na wazee wako...''

Nini kilitokea ikafikia mahali wajumbe wakamtosa Mwasisi Abdul

2.''Swali, 1954 hadi tunapata uhuru 1961 (miaka 7) udini ulipenyezwa vipi katika harakati za kudai uhuru, nani aliendesha hizo juhudi za kudhoofisha ushiriki wa Waislaam waliokuwa wengi, hadi kuzima nguvu kubwa walizokuwa nazo ndani ya TANU? Je ni Nyerere huyo huyo aliendesha kampeni akishirikiana na wakoloni kuhakikisha sauti za Waislaam hazisikiki tena wala kupata nafasi ya uongozi ndani ya TANU''?

3. ''Je huko majimboni kulikuwa na harakati za kuhakikisha Waislaam hawachaguliwi kuongoza matawi ya TANU hata kama wanajitokeza? Mathalani (Lake Province), (Western Province), (Southern Highlands Province), (Northern Province), (Central Province), J(Southern Province) na Jimbo la Mashariki(Eastern Province)...nani aliendesha harakazi hizo?''

4. a) Ni mwaka gani Abdul Sykes alijitoa TANU na sababu za kujitoa.
b) Je baada ya kujitoa TANU hakujishughulisha tena na mambo ya siasa?
c)Je ni lini mzee wako alijitoa TANU na baada ya kujitoa hakujishughulisha tena na siasa?
d)Je yawezekana kwamba harakati za kudai uhuru ziliposhika hawakuweza kwenda na kasi hizo?
e)Je yawezekana kwamba wasomi walipojiunga na TANU wazee wako walipatwa na mfadhaiko kwa elimu yao?

5. Swali binafsi
Nani alianzisha AMNUT na kwanini haikuungwa mkono na wazee wako baada ya kugundua Nyerere si miongoni

Haya ni maswali machache niliyoyanukuu kutoka bandiko la Mag3 na swali binafsi namba 5, hayahitaji reference ya kitabu cha Njozi, yametoka katika kitabu chako mwenyewe.

Ukumbi kimyaaa!! unakusubiri mhadhiri
Wanajamvi kwa mujibu wa Mohamed, maswali yamejaa lugha ya kughadhabika na shari. Maswali ni hayo hapo juu, kama kuna mahali lipo tatizo naomba mtu anionyeshe kughadhabika au shari, nitaomba radhi.

Kama hakuna Mohamed maswali yapo wazi ndani ya mada na maudhui, jamvi linakusikiliza
 
Back
Top Bottom