Yericko,
Mbona najibu maswali mengi humu na kuweka rejea zote?
Tatizo ni kuwa hamkubaliani na majibu na inaelekea hata hizo rejea hamsomi.
Hli swali la tatizo la udini wala si la kuuliza nyie kwani wanaoshutumiwa kwa hilo
wamefahamishwa na kitabu kikaandikwa, ''Mwembechai Killings...'' kitabu hiki cha
Prof. Njozi kimepigwa marufuku na serikali wakati wa utawala wa
Rais Mkapa.
Tusiende mbele zaidi.
Someni aliyosema
Prof. Njozi kisha Mag3 arejee tujadili:
http://www.islamtanzania.org/mwembechai/mchai-chap1.pdf
Chapter zote zinapatika search google: ''Mwembechai Killings...''
NB: Mag3 kakosea kuliuliza swali kwani kalitia mahali sipo.
Afanye rejea katika kitabu cha
Abdul Sykes asome:
''The First Muslim Congress 1962''
''The Second Muslim Congress 1963''
Baada ya hapo ndipo swali litaaingia mahali pake vizuri.
Ndugu zangu,
Swali linatakiwa linaloulizwa linatakiwa liwe ndani ya maudhui inayojadiliwa.
Swali linapokuwa kwanza limeulizwa ndani ya ''assumptions,'' swali kama hilo
linakuwa gumu kulijibu.
Swali linatakiwa liwe ndani ya ''facts,'' likiwa nje ya ''facts,'' yaani ukweli hili
pia linakuwa shida kulijibu.
Mathalan muulizaji anasema
Abdul Sykes alijitoa TANU.
Wapi yeye kasikia kuwa
Abdul alijitoa TANU?
Muulizaji anauliza iweje
Abdul alisalitiwa na wapenzi wake?''
Ndipo ninapposema soma kwanza kitabu au naweka sehemu ya kitabu ili
muulizaji asome na afahamu ukweli.
Lakini kubwa ni kuwa waulizaji wanauliza maswali wakiwa katika hali ya kuwa
wameghadhibika na maswali yanajaa lugha za shari.
Hali kama hii inavunja moyo kumjibu muulizaji kama huyo.
WATOTO WA WAPIGANIA UHURU BI. MAUNDA PLANTAN, JUMA MWAPACHU, HAPPY MTAMILA NA KLEIST SYKES WANAPOWAKUMBUKA WAZEE WAO
Mohamed Said June 19, 2016 0
Huyo hapo chini ni Nguruvi3:
↑
Hewalaa, ni kweli ni Juma Mwapachu aliyekuletea habari hiyo. Nimefanya editing ya hoja zangu kwa kuondoa jina Bakari na kuweka Juma, Mwapachu ikibaki pale pale,hoja ni hizi hapa chini
Wanajamvi
Mnakasha umefikia mahali patamu sana.
1. Tunasubiri Mohamed Said atuletee nakala ya draft(rasimu) au katiba ya kuandika au kukopi iliyokuwepo, andikwa au tumiwa na Abdul Sykes kabla ya katiba iliyoandikwa/kopiwa na Nyerere.
2. Tunasubiri Mohamed Said atueleze kabla ya kutangazwa kwa TANU mwaka 1954, jina la TANU lilitumika katika mkutano au mkusanyiko gani ambao Adul Sykes au mwingine nje ya Nyerere
3. Halafu kuna sauti hii ya Mohamed Said katika dakika 51-53 akimueleza mtangazaji wa radio kuwa kabla ya mwaka 1952 hakuna aliyemsikia au kumjua Nyerere. Sikiliza hapa
Kisha usome maneno haya ya Juma Mwapachu aliyempa Mohamed Said atueletee kama zawadi. Lengo lilikuwa kuonyesha sisi 'vichekesho' hatujui na wala hatuna mawasiliano na watu wakubwa kama akina Mwapachu.
Hata hivyo, katika maandishi hayo tunapata habari nyingine ikihusiana na introduction iliyofanywa na Hamza Mwapachu kwa Nyerere katika kile alichosema TAA Leadership
Kumbuka TAA leadership wakati huo ilikuwa chini ya Abdul Sykes, hivyo Hamza Mwapachu alimjulisha Nyerere kwa Abdul Sykes kama sehemu ya TAA leadership.
Soma hapa maneno ya Juma Mwapachu
''I still recall the visit vividly. I was a standard three pupil then and together with my brother Bakari had to sleep in the sitting room leaving our bedroom to the two guests.
Abdul Sykes was then President of TAA and the TAA leadership plus Dar-based political activists who were predominantly Moslems wanted Abdul Sykes to retain the Presidency.
Abdul was eager to secure Hamza's position on the matter given the fact that it was Hamza who introduced Nyerere to the TAA leadership in Dar back in 1949 before Nyerere left for Edinburgh University''
Kwa faida ya wasomaji, tunaweka maneno ya Juma Mwapachu katika tafsiri isiyo rasmi
Tunaomba radhi ikiwa kuna mapungufu yatakayojitokeza. Juma Mwapachu anasema hivi
''Bado nakumbuka kwa uyakinifu. Nilikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu na pamoja na kaka yangu Bakari tulilala sebuleni kuacha chumba kwa wageni wawili.
Abdulwahidi alikuwa Rais wa TAA na uongozi wa TAA pamoja na wanaharakati wa siasa wengi wao wakiwa waislam walitaka Abdul Sykes abaki kuwa Rais
Abdulwahid alikuwa tayari kumuafiki Hamza katika suala hilo katika ukweli kuwa ni Hamza ndiye aliyemtambulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA Dar es salaam mwaka 1949 kabla Nyerere hajaondoka kwenda chuo kikuu Edimburgh''
Ndipo tunakuja kutafuta ufafanuzi kwa Mohamed Said katika hoja ya 4 na 5
4. Mohamed Said , je bado unaamini kuwa kabla ya 1952 hakuna yoyote aliyewahi kumsikia Nyerere katika TAA HQ chini ya Abdulwahid Sykes?
5. Je, maneno ya Juma Mwapachu ni uzushi au ni ukweli?
6. Ikidhihirika J.Mwapachu maneno yake ni sahihi,utaliomba radhi jamvi kwa upotoshaji?
Je, utawaomba radhi wasikilizaji uliowapotosha katika redio na lini utafanya hivyo?
7. Kama maneno yako ni nkweli, je utakuwa tayari kukanusha maneno ya Juma Mwapachu hapa jamvini na kutuomba radhi kwa kutuletea habari zisizo na ukweli?
Na mwisho, Mohamed ajibu hoja hizi, hatuwezi kuburuzwa tu tukubali hata upotoshaji eti kwavile tunataka kujua mengine.
Haina maana kujua mengine ikiwa yapo tusiyoyajua kama haya tunayomuuliza
Mohamed Said, tafadhali sana usihamishe mjadala na kukwepa hoja.
Tunataka kusahihisha historia ya kivukoni kwa ukamilifu wake.
Hatutaki kuwaacha vijana wamechanganyikiwa kwa hoja kinzani.
Tutaendelea baada ya majibu, vinginevyo ukiri makosa kama tunavyokubali ya kivukoni.
Ahsante
Jibu langu:
Nguruvi3,
Ama ingekuwa si kwa kuwa naburudika kufanya mjadala na wewe
mie muda mrefu ningelikwisha nyanyua mikono juu lakini nastarehe
kuongea na wewe.
Allah amekupa kipaji cha aina yake.
Majibu nimekupa kuhusu katiba ya TAA Political Subcommittee kuwa
nyaraka na microfilm zote hazionekani Maktaba ya CCM Ddodoma
na TNA.
Sikuishia hapo nimekueleza kuwa kabla yangu katiba hiyo ilitajwa na
Listowel mwaka wa 1965 na
Pratt 1976.
Bado unataka nikuletee hiyo document.
Kama wewe hodari sana mbona huwaulizi CCM nyaraka hizo zilipo?
Lakini ninastarehe katika mnakasha huu kwa kuwa natoa darsa na
wengi wanasoma historia ambapo hawakupatapo kuisikia hata kwa
mbali.
Ndiyo maana narudi hapa tena na tena na tena.
Nakushukuru sana kwa hili.
Sasa nisikilize kwa makini na tuliza ubongo wako nikufunze mbinu
za ''critical analysis'' na kujifunza kusoma katikati ya mistari.
Sitakujibu hayo yote uliyoandika nitakujibu hayo tu ambayo umeweka
rangi nyekundu.
Hamza Mwapachu alimjulisha
Nyerere kwa uongozi wa TAA 1949.
Akili yako mara moja imekwenda kuwa walikuja hadi New Street na
kuzungumza na
Mwalimu Thomas Saudtz Plantan aliyekuwa rais na
Clement Mohamed Mtamila aliyekuwa katiibu wa TAA wakati ule.
Lakini ukweli ni kuwa
Mwalimu Thomas Plantan na
Clement Mtamila
walikuwa hawajapata kukutana na
Nyerere hadi alipokuja kwa
Abdul
Sykes 1952.
Inawezekana ujulisho huo ulikuwa wa salam za mdomo au wa barua.
Nakuwekea picha nikifanya mahojiano na
Bi. Maunda Thoams Plantan
mtangazaji wa kwanza wa kike Tanganyika, Sauti ya Dar es Salaam 1952
na mwalimu wa shule.
Mjukuu wa
Affande Plantan na mtoto wa
Mwalimu Thomas Saudtz
Plantan.
Kushoto
Bi. Maunda Plantan na Mwandishi
Katika mazungumzo yetu hakupatapo kunambia kuwa baba yake
alipata hata kwa siku moja kuonana na
Nyerere.
Nimezungumza pia na
Happy Mtamila hata mara moja hajanieleza
kama baba yake alipata kuonana na
Nyerere kabla ya 1952.
Kulia
Bi. Happy Mtamila na Mwandishi
Ningependa kukufahamisha tu kuwa uamuzi wa
Nyerere kuacha kazi
ulifanyika nyumbani kwa
Clement Mtamila Mtaa wa Kipata na Sikukuu.
Nyumba hii ilikuja kununuliwa na ukoo wa
Baharoon ikavunjwa na
sasa ni ghorofa.
Kushoto: Kleist Abdulwahid Sykes, Ebby Abdulwahid Sykes, Saudtz
Thomas Plantan na Abdulwahid Ally Sykes
Yako mengi hapo chini:
Mohamed Said: WATOTO WA WAPIGANIA UHURU BI. MAUNDA PLANTAN, JUMA MWAPACHU, HAPPY MTAMILA NA KLEIST SYKES WANAPOWAKUMBUKA WAZEE WAO