Ndugu zangu juzi nimeleta taarifa hapa yuko "publisher," anatafuta mswada mradi wa African History, "Facts, Denial and Acceptance," hakuna mtu wa kuchukua kazi hii? Naona ukumbi umekuwa kimya.
wote
Sent using
Jamii Forums mobile app
Wana Majlis.
Katika maisha yangu nimejuana na Wazungu wawili,
Peter Colmore na
Jim Bailey na wote hawa walini-inspire sana baada ya kujua maisha yao.
Peter Colmore alikuwa na ofisi yake karibu na nyumba yetu Mtaa wa Kirk
Street (Sasa Mtaa Lindi) karibu na International Hotel kama unaelekea
Nkrumah Street.
Ofisi hii alikuwa pamoja na
Ally Sykes na hapa ndipo kwa mara ya kwanza
niliona, ''aircondition na reel to reel tapedeck.''
Colmore aliweza kwa kushirikiana na Waafrika katika ukoloni kuwanufaisha
wasanii wengi wa Kiafrika na yeye kutajirika.
Nitaweka ''link,'' uweze kusoma maisha ya
Colmore kama nilivyomwandikia
taazia yake alipofariki.
Jim Bailey huyu ni kutoka Afrika Kusini.
Yeye ndiye alikuwa na gazeti maarufu Afrika katika miaka ya 1950 na 1960
na yeye pia kwa kuwatumia waandishi Waafrika aliweza kuwanufaisha kwa
hali ya juu waandishi Waafrika ndani ya Afrika Kusini na katika nchi zilizokuwa
chini ya ukoloni.
Hawa Wazungu nilijuananao kwa karibu sana kupitia mgongo wa Ally Sykes
na nilifanyanao kazi ambazo zilipanua ubongo wangu na kunitia katika dunia
nyingine.
Peter Colmore na
Jim Bailey ndiyo walionifundisha umuhimu wa kuweka
kumbukumbu na umuhimu wa picha.
Baba yangu
Said Salum alikuwa mpenzi wa ''gadgets,'' na yeye ndiye alinipa
camera yangu ya kwanza nikiwa na umri wa miaka 13 mwaka wa 1965.
Maisha yangu yote ninaweza nikayaeleza kwa picha zangu.
Nilipokwenda kufanya mahojiano na
Peter Colmore mwaka 1995 nyumbani
kwake Muthaiga, Nairobi 1995 alinifungulia maktaba yake ya picha na ''cuttings,''
za magazeti kuanzia 1940s wakati yeye na
Ally Sykes wakiwa na band ya muziki
wako vijana wakifanya maonyesho yao Nairobi Theatre, 1945 baada ya Vita
Vya Pili Vya Dunia.
Niliyoyaona katika maktaba ile sina maneno ya kuelezea.
Nilifahamishwa kuwa katika usia wake alisema kuwa maktaba yake ipelekwe mahali
fulani baada ya kifo chake.
Hapa katika maktaba hii nilikuwa nimejifunza jambo katika umuhimu wa kuhifadhi
nyaraka na pamoja na picha.
Bahati mbaya sana maktaba ya Colmore ni, ''private,'' siyo ''public.''
Tuje kwa J
im Bailey.
Bailey ameacha maktaba ya haja naamini ingawa sina hakika ni moja ya maktaba
muhimu katika picha na historia ya uhuru wa Afrika - Bailey African History Archive.
Hapa ndipo nilipotaka kufika.
Azma yangu mimi ni kuacha maktaba kama aliyoacha
Jim Bailey ikiwa na maelezo
na picha za historia ya Tanzania.
Ndugu zanguni,
Moyo hausahau kile ambacho jicho la camera limeona na picha inazungumza maneno
1000.
Hii picha hapo chini ni ya bibi yangu mkuu tukimwita
Bibi Popo.
Huyu alikuja Tanganyika kutoka Belgian Congo katika miaka ya mwisho 1800 na mimi
nilimwona hiyo picha nilimpiga 1965 nadhani alikuwa na zaidi ya miaka 80:
Mohamed Said: KUTOKA JF: ALLY SYKES, PETER COLMORE NA JIM BAILEY