Umenikumbusha ile 2013 baada ya kumaliza kidato cha nne nlienda mwanza mjini kusaka chochote, nikawa nauza CD. siku moja nlipita pale mkuyuni kwa mteja wangu kwenye nyumba za NHC. Akaona nina CD ya "MV Bukoba", yule bibi alibadirika mood nikaona machoz yanamlengalenga. Nlisiktika sana nkawa namdadis anisimulie ilikuaje
Alidai yeye alikua anafanya biashara pale bandarin, kwaio walikua wanaisubiri meli ili wafanye biashara, kwaio ilivoanza kuzama alishuhudia kila kitu.
Alidai ilisimama kwanza kwa masaa kadhaa, ni kama vile ilipata hitirafu. Pembeni yake kulikua na Mv Serengeti ambayo pia ilisimama kwa pembeni kuona kama inawezakutoa msaada.
Kwa maelezo yake anadai kulikua na mvutano juu ya nini kifanyike sababu jitihafa za kurekebisha hitirafu ili safar iendelee zilishndkana, wale wazungu wakatoa opinioni walete zile ferry zao ziikokote meli lakin kwa maelezo ya yule mama ni kwamba watu wa serikali waliopt kufanya jitihada zao wenyewe na kureject ofa ya mzungu.
Hapo ndipo walikuja na option ambayo ilifanya pale bandarini kukatanda vilio na simanzi. Waliingia na boat na mitungi ya gesi, wakatoboa upande mmjoa wakaanza kuhamishia watu kwenye boat.
Watu wote wakahamia upande uliotobolewa ili waokolewe haraka, ndipo uzito ukaelemea upande mmoja, meli ikageuka ikaanza kuchota maji polepole. Inachota, inarudi, inachota inarudi. Ilivochota maji mengi ikageuka jumla ikaanza kuzama kichwa chini miguu juu.
Msimlizi wangu alidai ilichukua takribani dakika 45 meli kuzama yote. Baada ya hapo CCM kirumba na Nyamagana stadium zilifurika miili, kumbukumbu ya kuhuzunisha sana.
Nlivorudi jioni nliiangalia ile movie nkafanikiwa kuona baadhi ya matukio (kama yalivyorekodiwa na kampuni la BARMEDAS) hasa lile la kuitoboa meli na ilivoanza kuswing had kuzama.
Kwa harakaharaka nligundua kulikua na uzembe mkubwa sana kwenye management ya meli.
Nliingia mtandaoni kutafuta majibu ya maswali yangu ambayo sikupata majibu kutoka kwa msimuliaji wala kwenye movie.
Kuna article moja ilidai hapakua na boya wala lifejacket hata moja kwenye meli.
Maiti zilizookolewa ni zaid ya mara tatu ya carrying capacity yake ( & mauzo ya tiketi yaliyorekodiwa), 900/3000+!
Inadaiwa ilikua imemaliza miezi 6 haijafanyiwa service, ambavyo inatakiwa ifanyiwe service kila kabla ya kufanya safari.
Yote katika yote ni kumbukumbu ya kuhuzunisha ambayo iligusa wengi sana kwa uzembe wa watu wachache.
Lakini pia wenye mamlaka husika walipata somo la kujifunza.