Kumbukumbu ya Mpigania Uhuru na Muaisisi wa TANU Moshi Mjini Kituo Cha Mayatima Cha Halima Selengia (1919 - 2013)

Kumbukumbu ya Mpigania Uhuru na Muaisisi wa TANU Moshi Mjini Kituo Cha Mayatima Cha Halima Selengia (1919 - 2013)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Marehemu Bi. Halima Selengia aliyefariki dunia mwaka wa 2013 akiwa na umri wa miaka 94 alikuwa kati ya waasisi wa TANU mwaka wa 1954 na mmoja wa wanawake waliokuwa mstari wa Bi. mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Bi. Halima Selengia anaingia katika kundi la akina mam wapigania uhuru kama Dharula bint Abdulrhamani wa Tabora pamoja na mwenzake Nyange bint, Chande, Shariffa bint Abdulrahman wa Lindi, kwa kuwataja wachache lakini wote hao taifa na wanahistoria wamewasahau.

Moshi Mjini wamejipambanua kwa kuwa na kituo cha kulea mayatima kilichopewa jina la Halima Selengiya.
Naweka kipande kifupi cha harakati za TANU Moshi mjini kutoka kitabu cha Abdul Sykes:

''Miongoni mwa matawi yote ya TANU nchini Tanganyika, tawi pekee lililoungwa mkono na wanawake na wao kuwa ndiyo nguvu kuu ya chama, lilikuwa tawi la TANU la Moshi mjini.

Nguvu kuu ya TANU ilikuwa wanawake wafanyabiashara na kiongozi wa hawa wanawake wajasiri amali alikuwa mwanamke mmoja wa Kimasai, Mama Binti Maalim.

Ingawa mume wa Binti Maalim, Jumbe Mohamed, alikuwa mtumishi wa serikali, na kwa hiyo alijitenga na siasa, hili halikumzuia mke wake, Binti Maalim kuwa mwanachama na mwanaharakati wa TANU.

Binti Maalim alihakikisha kwamba kila mwanamke aliyekuwa akifanya biashara alikuwa mwanachama wa TANU na alikuwa akitoa sehemu katika kipato chake kusaidia harakati za kudai uhuru. Wanachama wa mwanzo kujiunga na TANU walikuwa akina mama hawa waliohamasishwa kujiunga na chama na Mama Binti Maalim.

Nafasi ya wanawake katika harakati mjini Moshi inaweza kuonekana katika katika safari yake ya pili ya Nyerere Kilimanjaro.

Katika safari hiyo Nyerere alifikia nyumbani kwa Bibi Halima Selengia aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya tawi la TANU Moshi.''

1664658924883.png
1664659051646.png
1664659096407.png



 
Back
Top Bottom