Kumbukumbu ya siku ya uhuru Lindi 9 December 1961

Kumbukumbu ya siku ya uhuru Lindi 9 December 1961

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Nimekuta hayo hapo chini mahali na mimi nimeamua kuunga mkono kukumbisha siku ya kupokea uhuru Lindi:

KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU WA TANGANYIKA TUJIKUMBUSHE HISTORIA YA BARABARA YA UHURU ILIYOPO KATIKA MANISPAA LINDI.

Msomaji wa makala za durusu durusu za historia mapema nimepita barabara ya uhuru ambayo inapatikana katika manispaa ya Lindi.

Nikasema ni vyema kama nitashea nanyi historia inayohusu uhuru wa Tanganyika kwa hapa Lindi kuelekea maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika katika makao makuu ya jimbo la kusini Lindi.

Kama tunavyofahamu kwamba sikukuu hii ya umma inaadhimishwa kila inapofika siku ya tarehe 9 Desemba kila mwaka. Siku hii huadhimisha na hukumbukwa kama sehemu ya mwisho ya utawala wa Uingereza kwa Tanganyika mwaka wa 1961. Mwaka huu ni mwaka wa 63 wa uhuru wa Tanganyika.

Endelea kudurusu historia ya barabara ya uhuru wa Tanganyika hapa Lindi.

✍️
Katika barabara hii ya uhuru kabla ya mwaka 1961 ilikuwa ikifahamika kwa jina la Queen Elizabeth Avenue ambapo walowezi wa kikoloni walikuwa hapa Lindi tayari walikuwa waendesha shughuli za utawala huo walikuwa wakipita katika barabara hii kuenenda shughuli zao za doria nyakati za usiku hata mchana wakati wa utawala.

Ambapo barabara ilikuwa imeshasimikwa jina la malkia wa uingereza kama mtawala mkuu wa Tanganyika kwa wakati huo ulinzi uliokuwa umeimarishwa ilikuwa ni kwa ajili ya kuimarisha mkuu wa mkoa wa makao makuu ya jimbo la kusini Lindi anakuwa salama wakati wote.

Baada ya kutangazwa kwa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 jina la barabara hii sufufu lilibadirishwa mapema katika siku ya mkesha na kuitwa jina la Uhuru Avenue jina ambalo limekuwa likitumika tokea kipindi hiko cha mwaka 1961 hadi hivi leo tunapoelekea kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika.

DUA ILIYOSOMWA NA YUSUF CHEMBERA UWANJA WA GOFU LINDI KUPOKEA UHURU
Siku ya ukumbusho mkubwa sana mjini Lindi ilikuwa siku ya uhuru, tarehe 9 Desemba, 1961.

Sheikh Mohamed Yusuf Badi, bingwa wa mashairi, aliombwa na TANU kuandika hotuba ya uhuru itakayotolewa na Yusuf Chembera mbele ya DC akiwa kama mwakilishi wa utawala wa Kiingereza uliokuwa uking'oka.

Hotuba hiyo ya Sheikh Badi iliandikwa kwa herufi za Kiarabu na Yusuf Chembera.

Akiwa mtoto mdogo Yusuf Chembera alipelekwa kwa Sheikh Yusuf Badi na baba yake kwenda kusoma elimu ya dini na aliendelea kuwapo hapo chuoni kwa Sheikh Badi hadi alipohitimu.

Yusuf Chembera na Salum Mpunga vijana waasisi wa TANU chini ya mzee wao Suleiman Masudi Mnonji ndiyo waliomuingiza Sheikh Yusuf Badi TANU na akashiriki mstari wa mbele kumuunga mkono Julius Nyerere kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sheikh Badi hakuona kama ipo hotuba yoyote iliyoandikwa na mwanadamu iliyostahiki hafla kama ile ya siku ya kujikomboa kutoka minyororo ya ukoloni.

Sheikh Badi alimsomea mwanafunzi wake Chembera, dua ya "Kunut," ambayo husomwa na Waislam katika kila sala ya Alfajr.

Usiku wa manane wa tarehe 9 Desemba, 1961 ulikuwa usiku adhim sana kwa wote wawili, mwalimu na mwanafunzi wake, pale watu walipokusanyika katika Uwanja wa Gofu kumsikiliza Yusuf Chembera mwanafunzi wa Sheikh Mohamed Yusuf Badi akisoma "Kunut" kupokea uhuru wa Tanganyika.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes).

1732984935366.jpeg

Mtaa wa Sheikh Mohamed Yusuf Badi
1732985024785.jpeg

Yusuf Chembera akiwa katika mavazi ya Mayor wa Mji wa Lindi​
 
Back
Top Bottom