kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Hayati Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wetu kwenye awamu ya Kwanza ya uongozi wa taifa letu. Alikufa miaka 40 iliyopita lakini mwaka 2024 serikali inashiriki kikamilifu kwenye kumbukumbu yake kutimiza miaka 40 toka kuondoka duniani.
Maswali kichwani mwangu ni mengi, hasa yanayotokana na umaskini wetu unaotegemea mikopo kutoka nchi za nje ili kupeleka huduma kwa wananchi, kipato kidogo kwa watumishi wa umma, na ukosefu wa huduma kwa wananchi wa kipato cha chini.
Swali #1: Serikali imetumia kiasi gani cha pesa kufanukisha kumbukumbu hii?
Swali #2: Ni viongozi wangapi/wa ngazi zipi wanahitaji kufanyiwa kumbukumbu za kitaifa kama hizi?
Swali #3: Jambo hili ni la kikatiba, kisiasa au kijamii tu?
Swali#4: Pesa ya kufanikisha kumbukumbu kama hizi ni kwamujibu wa bajeti?
swali #5: Fursa zinazopelekwa na serikali (kodi zetu) kwenye jamii ya viongozi wanaokumbukwa kwa njia zitafikaje kwenye jamii ambazo hazina/hazikuwa na viongozi wa aina hii?
Tunafungua boksi ambalo tutashindwa kulifunga kama lilivyokuwa (presidency). Tutagawika, tutarudisha siasa na chaguzi za kikabila, kidini na kikanda polepole kwa makusudi au kwa bahati mbaya, kwakujua au kutokujua.
Kwanini pesa hizi zisipelekwe kutatua kero za watanzania?