RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 55,727
- 123,094
Pale nakumbuka one down two to goPale Drive In walikuwa wanaongoza kuweka movie za Kihindi khaaaa...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pale nakumbuka one down two to goPale Drive In walikuwa wanaongoza kuweka movie za Kihindi khaaaa...
Mtu binafsi. Akahamia Kenya waliopo sasa hivi wakaomba awauzie akataja bei za ajabu kilichotokea hataki tena kuisikia Tz kama bado yupo hai.hili lilikuwa eneo la mtu binafsi au serikali?
Watu binafsi Wahindi, baadae ndo wakaja kununu ubalozi wa marekanihili lilikuwa eneo la mtu binafsi au serikali?
Na movie hz zilikuwa na wapenzi sanaPale Drive In walikuwa wanaongoza kuweka movie za Kihindi khaaaa...
Umesahau tulivybanana empire na empresss kwa 'Endless Love' na bibie Brooke Shields na 'Three the Hard Way' ya Akina Jim Kelly, Jim Brown na Fred Williamson, maniga watupu! Ilikuwa raha sana!Ilipotoka movie la cyborg nakumbuka watu tulienda kubanana kuicheki
Sema pale drive in kwa nje cinema bubu shuguli
Ilikuwa syo ndogo,kila mtu anajuaa,wakalimani wapo wa kutoshaaa
Ova
Duh!Fred WilliamsonUmesahau tulivybanana empire na emprass kwa 'Endless Love' na bibie Brooke Shields na 'Three the Hard Way' ya Akina Jin Kelly, Jim Brown na Fred Williamson, maniga watupu! Ilikuwa raha sana!
Bila kusahau pale Empire,ile movie matata sana WAR BUS.....na Break Dance....Disco Dancer(mithun huyu..kihindi)looo kipindi nchi ina heshima na adabuUmesahau tulivybanana empire na empresss kwa 'Endless Love' na bibie Brooke Shields na 'Three the Hard Way' ya Akina Jim Kelly, Jim Brown na Fred Williamson, maniga watupu! Ilikuwa raha sana!
Yes mkuu nakumbuka mwaka fulani...usiku wa kuamkia uchaguzi mkuu wa nchi,Vigunge wa Lumumba wakaamua ile movie ya Vita vya Kagera ionyeshwe pale Drive Inn...weee ilikua propaganda kubwa mno yenye mafanikio makubwa,kila mara sura ya Brig.Mayunga aka mti mkavu ikitokea kwenye screen watu wanashangilia kupita kiasi,Brig. Mayunga ile vita ndio alikua main attraction. Uchaguzi mkuu asubuhi yake ni ushindi mkubwa mno kwa ....,yeah maisha yenye heshima na adabu kubwa kipindi hicho.Na movie hz zilikuwa na wapenzi sana
Enzi hizo umri mdg lkn unakesha mpaka usiku
Mnene
Ova
Hapo tulikuwa Harbours Club KURASINI....Meneja Mzee Naido hahahaUmenikumbusha Enter the Dragon!
Majestic cinema, Tanga hii?
Umeisahau ODEON hii ilikuwa Kisutu, sana picha za kihindi.Nimeona uzi hapa JF ukisifia Jumba la Senema la Empire la siku hizo, nikaona nikumbushie (na kuwajuza uzao wa dot.com) majumba ya senema yaliyokuwepo Dar enzi hizo.
Miaka ya 70 kulikuwepo na majumba sita ya senema jijini Dar. Bila kufuatilia mpangilio wa umaarufu au kigezo kingine cho chote, nayataja majumba hayo kama ifuatavyo:-
1. Empire: Hili lilikuwa mtaa wa Azikiwe mkabala na Posta Mpya.
2. Empress: Hili lilikuwa Mtaa wa Samora maeneo ya Askari Monument, likiangaliana na tawi la benki la Bank House.
3. Avalon: Hili lilikuwa Mtaa wa Zanaki, jirani na Halmashauri ya Jiji. Jumba hili lilidumu muda mrefu kushinda yote, hadi mwaka 2000.
4. New Chox: Hili lilikuwa Mtaa wa Nkrumah likitazamana na viwanja vya Mnazi Mmoja, jirani na Chinese Restaurant ambayo ilikuwa ikijulikana sana kwa 'fried rice'.
5. Cameo: Hili lilikuwa Kisutu, Mtaa wa Jamhuri, karibu na Tawi la Posta La Kisutu. Hili lilijikita katika kuonyesha senema za Kihindi. Pamoja na hayo, Waswahili walikuwa wakifurika kuangalia senema hizo.
6. Drive-In: Hili lilikuwa palipo Ubalozi wa Marekani hivi sasa. Halikuwa jumba bali uwanja wa wazi, unaingia na gari lako na unaangalia senema ukiwa kwenye gari.
Majumba hayo yalikuwa yakionyesha senema tofauti mara mbili kwa siku. Senema ya "The Ten Commandments" mwaka 1975 (or was it 1976?) ndiyo ilikuwa ya kwanza na ya mwisho kwa majumba yote sita (pamoja na Cameo) kuonyesha senema hiyo hiyo mara zote mbili kwa wiki nzima na bado watu walikuwa 'wakipigana' kuingia. Huo ni ushahidi tosha wa jinsi senema hiyo ilivyopendwa.