Kumchukia mtu kutokana na mafanikio yake ni kufilisika kwa uwezo wa kufikiri

Kumchukia mtu kutokana na mafanikio yake ni kufilisika kwa uwezo wa kufikiri

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Kufanikiwa kumekuwa moja wapo ya sababu ya kufanya maadui waongezeke kwani kadri neema zinavyoongezeka ndivyo hivyo hivyo maadui wanaongezeka. Swali kubwa ni kuwa Kuna mantiki yoyote kumchukia mtu aliyefanikiwa?

Iko wazi chuki ni miongoni mwa vitu vinavyosababisha msongo wa mawazo. Kumchukia mtu ni sawa na kujichukia wewe mwenyewe sababu madhara ya chuki ukirudia wewe mwenyewe kwa kuishi na maumivu ndani ya nafsi yako. Swali la msingi kwa nini uishi na maumivu kisa tu kumchukia mtu?

Mafanikio ni juhudi ya mtu na mpango wa mungu na maisha ni kuchagua kama umechagua kutojituma hiyo ni ishu yako binafsi usitake Kila mtu asijitume kama wewe waache watu wajitume katika kazi na matokeo ya kujituma siku zote ni mafanikio (hard work pays).

Mafanikio sio ya mtu mmoja bali ni ya jamii kumchukia mtu aliyefanikiwa ni kuchukia jamii nzima inayomzunguka. Vijana tufanye kazi mafanikio ya watu yatupe motisha kuwa inawezekana kufika sehemu fulani kwani chuki haiwezi kufanya mafanikio ya mhusika yaje kwetu bali kazi na sala zinaweza kutufikisha kwenye mafanikio kuliko wale tunaowachukia.

From Northern part of Tanzania.
 
Hii ni katika jamii ambazo hazijazoea mafanikio, utaonekana sio wa kawaida utaogopwa na maneno lukuki kuhusu ushirikina.

Ndugu watakuhofia ili usiwatoe kafara, na kila balaa likiwafika wanakushuku.
 
Back
Top Bottom