Yawezekana kweli?! au na wewe umekuja na konkulusheni!
Hebu fikiria, nikwanini usimwambie mwenza wako unachotaka na kitakachokuridhisha kuliko kwenda kumchungulia ******? mimi ninafikiri hapa swala muhimu ni kukosekana kwa mawasiliano,watu wawili walioamua kushare miili yao inabidi wazungumze! Ni katika mazungumzo unaweza kumjua mwenzako na kufanya kile anachotaka, lakini hawa wote kila mtu hajiamini mbele ya mwenzake na ndio maana mwanamke anajifunukafunika na mwanaume anaishia kuchungulia. au labda mwanaume kila wakati anayakosoa maumbile ya mwanamke na mwanamke anakosa uhuru wa kukaa 'wazi' kwa mwenzake. kwa ujumla wana tatizo. jamani tuanze kuzungumza,tuambiane ukweli,na kama unaona mwenzako ana aibu jaribu kumtoa aibu akuone rafiki,zaidi ya yote usikosoe maumbile ambayo hakuna mtu mwenye uwezo wa kuyarekebisha.