Kumekucha: Baraza la Mawaziri kivuli - Mbatia out

Sasa bunge lenyewe ni la mwisho kabla ya serikali mpya, hao mawaziri vivuli wapya watakao ziba nafasi hizi watafanya nini?
Na wa zamani waliotemwa wangekuwa na athari gani?
Inabidi ujishangae mwenyewe kwa kutoona mantiki ya mabadiliko hayo.

Nadhani kwa aina fulani unataka uonekane kama kituko kwa kutoona maana ya mabadiliko yaliyofanywa.

Hata kama ni siku moja ingekuwa imebaki, kusimamia 'principle' ni mhimu kuliko kitu chochote maishani.

Watu wa aina yako msiokuwa na mnalosimamia ndio mnaowapa watawala kiburi.
 
Point

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja, Chadema pekee yao hawawezi na haitakuja kutokea wakaweza!. Sisi Tanzania tuna tatizo kubwa la kitu kinachoitwa "Managing The Political Diversity" from both parties, CCM na Wapinzani, hadi ndani ya mihimili Bunge, Serikali na Mahakama.

Kwa muda uliobakia, hata kama Chadema inajua NCCR imenunuliwa na CCM, hivyo itajitenga nao, na Wabunge wote wa CUF wanasubiria tuu Bunge livunjwe watur rasmi ACT Wazalendo, Chadema walipaswa wawavumilie tuu, sometimes its good kumvumilia adui yako ili usiwaudhi wale waliokuja kwako kwasababu ya huyo adui yako. Kura milioni 6 za Lowassa ile 2015 sio za wana Chadema pekee.

Kosa kubwa la Chadema kuelekea 2020 ni kujidhania kwenye kambi ya upinzani, Chadema bado ni determinant, it's not!. Kuendelea 2020, Chadema is a dying horse, hivyo kitendo kama hiki cha kuihodhi kambi rasmi ya upinzani Bungeni, it's like a final kick of a dying horse.

Ili upinzani uweze kuvuna mavuno yoyote ya maana 2020 kwanza lazima Chadema wakubali kugawana himaya yake kwa kukubali ku share na vyama vingine vya upinzani.

Kabla ya Bunge kuvunjwa, Chadema ambacho kwa sasa ndio chama kikuu cha upinzani, kifanye SWOT na PEST analysis kwa Wabunge wake wote, matokeo ya analysis hiyo yakionyesha Mbunge huyu anachaguliwa kama mtu na sio chama, then Chadema ikubali matokeo, wabunge wote wa Chadema watakaojiunga CCM, Chadema ijihesabu hayo majimbo yamepotea unless wana CCM wenyewe ndio waipigie Chadema kura za chuki kutokubali wapinzani waja leo na kusimamishwa kugombea CCM.

Pili wabunge wote wa Chadema watakao hamia vyama vingine, Chadema ikubali to share them na wapinzani wengine kwa kutosimamisha wagombea wengine ili kila jimbo na kila kata mgombea wa CCM apambane na mpinzani mmoja tuu. Ikitokea jimbo lilikuwa Chadema kama Moshi Vijijini na Rombo, wabunge wake wwkahamia NCCR Mageuzi, Chadema ikubali matokeo. Ikisimamisha wagombea wapya, hii itakuwa ni vita vya panzi, furaha ya kunguru, wapinzani wata split kura zao, CCM atayatwaa majimbo ya upinzani kama ameokota dodo chini ya muembe.

Upinzani pamoja na tofauti zao za ndani, lazima wavumiliane by managing diversity kwa kushirikiana hivyo hivyo pamoja na tofauti zao, wasimame united and stand as one against a common enemy, vinginevyo kwa huku bara, tunarudi kuwa nchi ya chama kimoja CCM only and only CCM!.
P
 
Kweli upinzani Tanzania ni upuuzi mtupu. Kweli hivi ndio vyama vinavyotaka kuongoza nchi. CCM haina mpinzani watangoja sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wangekuwa wepesi kiwango hicho Chama cha Wafuga Chatu kisinge waogopa na kutumia mbinu za ushetani kiwango wanachotumia kupambana nao.
 
Huu ujumbe ungemwambia jiwe mapema nazani lisu angekuwa bado yupo bungeni mpaka leo, Ben Saanane na akina Azory Gwanda na wengineo wangekuwa bado wanapumua hapa duniani.

Kutuma ujumbe ambayo hauna mazara kwa mtu kwamba unajua kinachoendelea si vibaya sana, maana unampa nafasi ya pili kujilekebisha kama anaeweza kufanya hivyo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…