GE2025 Kumekucha! CCM yaitisha mkutano mkuu wa dharura kwa njia ya mtandao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Amesema mabadiliko madogo ya katiba ya chama chao. Japo wanaweza ingiza ajenda zai zilee za kuwaacha watu midomo wazi
 
Kikao Cha Mkutano Mkuu na agenda ni za Siri, kweli CCM imetekwa na wenyewe. Wajifunze kwa CHADEMA waliofanya mambo yao kwa uwazi Dunia yote ikishihudia.
 
yule mama wa ACT alisema sahihi khs KUCHANGANYIKIWA

Mabadiliko madogo ndio yanafanyika siku ya Mkutano Mkuu?. Yani wajumbe wataletewa agenda siku ya Mkutano au walishapewa agenda kwenye notisi ya Mkutano.
 
Jimama limechanganyikiwa hili silipendi sana hilo limama lenu aisee. Why mungu asilibebe tu liondoke chap chap hapa nchini kwetu
 
Wajumbe wa mkutano mkuu wenye access na internet ni wangapi?
 
CCM hatimaye wako kwenye kitanzi na sasa wanatambua umuhimu na maana ya reforms.

Bi Mwenda amesigina katiba ya nchi alipochoka muda mrefu sana na sasa kahamia ya chama anaendesha nchi na chama kama jiko lake.

Sasa inapigwa danadana mkutano kwa mtandao ambao mtandao wenyewe haupo.

No reforms no election.
 
Nchimbi amekaba watu koo
 
Watakaozungumza kwenye kikao mtandao ni waliopangwa na kitengo
 
FRIDA KAAYA ADAIWA KUVURUGA UCHAGUZI WA UWT WILAYA YA MOSHI MJINI

Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini Frida Kaaya amedaiwa kutaka kuharibu Uchaguzi wa UWT Wilaya ya Moshi Mjini baada ya kutuhumiwa kujaribu kuiba kura za Mgombea wake ambaye ni katibu wa CCM Kata ya Kiusa Yobineshi Mafie.

Katibu huyo amedaiwa kuchakachua kura wakati wa zoezi la kuhesabu kura ambapo kura zilizoharibika na za wengine alikuwa akimpatia mgombea wake jambo lililopelekea mabishano na wagombea wengine kabla ya Msimamizi wa Uchaguzi huo kuingilia kati.

Inadaiwa katibu huyo aliwaagiza makatibu wote wa CCM kata kwenda eneo la Mkutano na kumuombea kura mgombea wake huku baadhi yao wakihusishwa na vitendo vya rushwa hali iliyopelekea TAKUKURU kuwafukuza katika eneo hilo huku Mgombea udiwani kata ya Mjimpya Rashid Maarufu BABA MZAZI ambaye ni mtu wa karibu sana na Katibu huyo wa wilaya kufukuzwa eneo hilo baada ya kukuta akinunulia wajumbe chai na vinywaji.

Hata hivyo mgombea huyo alishindwa vibaya sana katika uchaguzi huo uliendeshwa kwa uwazi, haki na usawa na wagombea wote kukubari matokeo na kusaini fomu za matokeo kama kanuni zinavyoelekeza.

Katika hali ya kushangaza Katibu huyu wa CCM Wilaya alimshauri na kumsaidia mgombea wake kukata rufaa akidai kuwa hakuridhishwa na mchakato wa Uchaguzi hivyo anaomba uchaguzi urudiwe na huku akijinasibu kuwa atagharamia gharama zote za uchaguzi. Kitendo cha Katibu wa CCM wilaya kutumia nguvu kubwa kumsaidia mgombea wake, kumewavuruga wajumbe na kumshangaa kwa nini yeye ambaye kanuni za Uchaguzi zinamtambua kama mkurugenzi wa Uchaguzi anajiingiza kwenye makundi ya kuwabeba wagombea.

Tunaomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka kudhibiti vitendo hivi kwani vinaashiria kuwepo kwa mambo ya kihuni katika uchaguzi ujao wa wabunge na madiwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…