GE2025 Kumekucha! CCM yaitisha mkutano mkuu wa dharura kwa njia ya mtandao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kama ni kweli basi inawezekana kukawa na mabadiliko wa wagombea wa ngazi za juu. Hususani, Majaliwa kuwa mgombea mwenza na Nchimbi akisubiri uwaziri mkuu. Kwani kile kikao cha January 2025 hakikutarajia Majaliwa hatagombea ubunge, walitarajia ataendelea na uwaziri mkuu. Ndiyo matatizo ya kuteua mapema mno. Busara huwa ni kusubiri hadi dakika za mwisho ukipima upepo unakoelekea.
 
Wacha tusubiri ingawa walishatangaza kuanza kufanya vikao kwa njia ya mtando tangu January walipokutana kwa mara ya mwisho.
Ccm kwa mara ya mwisho walikutana January??
Wewe msahaulifu au ni mvivu wa kukumbuka. Ccm kamati kuu walikutana March,
Baada ya hapo wakakutana tena mkutano mkuu May 30, ambapo walizindua Ilani, wakabeba wasanii wote kwenda nao. Ndio hiuo siku walisema Wana wanachama million 13
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuitisha Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa utakaofanyika kwa njia ya mtandao siku ya Jumamosi, Julai 26, 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vyetu vya kuaminika ndani ya CCM, tangazo hilo lililotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Idara ya Oganaizesheni, Issa Haji Ussi Gavu, kwa Makatibu wa Wilaya na wa Mikoa wa CCM linaeleza kuwa mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika maandalizi ya mkutano huo, Makatibu wa Wilaya na wa Mikoa wa CCM wameelekezwa kuwaelekeza wajumbe wote wa Mkutano Mkuu waliopo katika maeneo yao kuhakikisha wanakusanyika katika ofisi za CCM za Wilaya au Mikoa, kutegemeana na nafasi, ili kushiriki kwa pamoja.

Taarifa hiyo pia imeweka msisitizo juu ya maandalizi ya mazingira ya kufanikisha mkutano huo, ikiwemo kuweka vifaa vya kuoneshea kama televisheni au skrini, viti vya kutosha, na kuhakikisha mazingira ni tulivu pamoja na kuwa na miundombinu imara ya mtandao.

Jambo TV imezungumza na makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa mbalimbali ambao wamethibitisha kupokea tangazo hilo huku wakieleza kuanza maandalizi ya mkutano huo.

Hata hivyo ajenda zenyewe za mkutano hazijawekwa wazi huku kukiwa na tetesi juu ya uwepo wa maamuzi kadhaa mazito yatakayopitishwa na mkutano huo wakati ambao chama hicho kiko katika mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali za chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

View attachment 3417211
Kwi Kwi Kwi
 
Maza kaanza kuwaogopa Wajumbe mpaka kaamua kutumia mtandao....!!?

Ila kwa nini hizi taarifa za hivi karibuni zinatolewa ba Wazanzibar badala ya Makalla au Nchimbi...!?
 
Back
Top Bottom