Kwanza na declare interest Kambogi ni mshikaji wangu-rafiki ni mmoja ya mabinti wastaarabu sana na wako poa tuu!
Lazima tukubali kabisa DSTV hadi inafika hapo watu hawa ambao wanaonekana wanakula rushwa au wamechukua rushwa wamekuwa na mchango mkubwa sana kufanya Watanzania kununua visimbusi vya DSTV na watu kufatilia DSTV na pia kuweka maudhui yanayaendana na watanzania maana zamani DSTV ilikuwa inaonekana ya matajiri ila kwa sasa imekuwa ya kila mtu hasa kwa ubunifu wa vipindi na hasa Tamthilia…
Kwa vyovyote vile washindani wa DSTV hawawezi kutulia kuona mshindani wao anazidi kuchanja mbunga namna ile …ni lazima watatafuta njia za kuwachafua watu ili watimize malengo yao…
Tamthilia kali mnazo ziona leo pale DSTV haziwi vile kwa sababu ya Lamatah tuu bali kuna watu nyuma hasa watu wa DSTV ambao huwa wanajaribu kuhakikisha standards za maudhui na kila kitu kiwe kizuri lakini bahati iliyo mbaya wale ambao wanaona kama kina Lamatah wanapendelewa wameona wawachafue watu ili wao washinde….
Watanzania hatupendi kuambiwa ukweli kabisa ,mtu anaambiwa kabisa hichi kitu bado hakijakidhi vigezo na hakimiti vigezo tunavyo vitaka hapa DSTV basi ana kasirika anaona ameombwa rushwa…Mtu anaambiwa rekebisha hili na hili hataki eti anakwenda kusema South Africa…
Jamani Maproducer wa Tz lazima mjue hakuna Msouth(Mzungu) ataweza kuwapa kipaumbele zaidi ya Mtanzania mwenzenu…Watazamaji wanataka kilicho bora lazima wakina Kanboge wahakikishe watanzania wanapata kila kizuri….
Kuna Tamthilia zimekatishwa hapo DSTV kwakuwa maproducer hawataki kufata standards wakishindwa wanakimbilia South Africa..na bahati nzuri huyu binti hajaanza kuandamwa leo maana kama kusimamishwa angeshasimamishwa toka mwaka jana maana watu wakiambiwa tu kipindi chako hakijakidhi tunayo yahitaji basi wao ni kwenda kusema south kwa kuwa wanajua kitika majungu watafanikiwa…
Hii vita ni zaidi ya hicho ulicho kiandika hii ni Vita ya wabongo wenyewe baadaya ya kuona juakali imefanikiwa basi kila mbongo hasa maproducer wanataka ile nafasi na hapa Lamatah ajiandae na Juakali yake….
Watanzania hasa maproducer wanapenda hela lakini hawako tayari kupika vitu vizuri wakiambiwa hiki kibaya basi wanaanza kumchukia yule anayetengeneza kitu kizuri badala ya kujirekebisha!
Mimi nilishamwambia Babra kama atafukuzwa DSTV haiwezi kuwa mwisho wa maisha na mambo yatasonga na atapata kazi nyingine maana uwezo anao ..Tanzania ni kiwanda cha majungu hasa ukifanikiwa….!