Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi sijui chochote dear😂Wewe unajua mengi? Upate kitengo huko na wewe maana nimekufuatilia hapa sana kimyakimya uko nondo.
👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾Mimi ni mtoa habari tu Mkuu, sihusiki kwa namna yoyote na wala sifahamiani na mhusika yeyote.
Sikuwa na maana mbaya kukujibu vile, ushahidi ni muhimu kabla ya kuchukua hatua yoyote.
ACHA UONGO WEWE WEMA HAJAWAI KUIGIZA KWENYE HUBAHuba ilikuwa na kick kubwa sababu ya Wema kuwepo msimu wa kwanza kama sikosei.
aziz mohamedHii huba ni isidingo maana toka jaana kuisikia😁😁🙌🏾🙌🏾. Nani ni director
unaongea nini wewe wema alishawai kunja hadi million kumi kwa filamu mmojaMil. 3 Bongo hii?
Hata Wema Sepetu hapati hiyo kwenye hayo maigizo yao.
Ngoja nikaulize nikipata data vizuri nitakurudia.
yule jamaa hapendi umaarafu na hapendi interview sijui yupo wapiHivi mtitu wa Game first Quality yupo wapi maana ni moja ya director bora wa films lakini hapendi spotlight kabisaa.
Hapati maua anayostahili
waproducers ndo wana hali ngumu sio waigizajiHee[emoji15]
Hadi Azam kumbe Kuna hayo mambo?
Maskini waigizaji wetu wana hali ngumu[emoji3064]
Mwalimu unafikiri unaweza kuzalisha hata 0.00001 ya huyo Mkurugenzi???Kama mshahara wa mkurugenzi dstv hautoshi sisi waalimu wa daraja la iii B vijijini tusemeje
ACHA UONGO WEWE WEMA HAJAWAI KUIGIZA KWENYE HUBA
Mkuu, mbona nilionesha kutokuwa na uhakika kwenye post zangu?unaongea nini wewe wema alishawai kunja hadi million kumi kwa filamu mmoja
Tabia haina jinsiaWanawake wengine wana tabia za kiume!💔
Sasa huoni kafanana kabisa na baba.Wanawake wengine wana tabia za kiume!💔
Hata director naye haelewi inaelekea wapi.Bora hata hao wameongeza wanawake,mi huba ndo sielewi mwelekeo wake kila siku watu wanaanzisha mapenzi hovyohovyo sijui maudhui yake ni yapi yaani hata direction haieleweki kila siku watu wanapendana
Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
Kuna tamthiliya ilikuwa inaitwa Yalaiti ilienda baadae ikarudishwa nyuma alaf ikafutwa kumbe kuna kamchezo kanafanyika. Kuna kipindi pia tamthiliya ya Pazia ilisitishwa alaf ikarejea tena na kwenda kumalizika,.This is exclusive!
Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.
Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.
Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!
Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.
Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!
Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…
Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwa kuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo awali kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.
Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.
Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.
Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,
Nifah.
View attachment 2825510View attachment 2825511
Wacha weeeee. Kama ambavyo wewe unapenda kuangalia connection nduvyo wengine wanapenda kuangalia Tamthilia maana kupanga ni kuchagua.Kumbe kuna watu wanaangaliaga hivyo
Vipindi
Ova
Kwamba mwanamama alikua anataka apelekewe moto na wasanii/directors wanaotaka kazi zao zirushwe DSTV?Si tu kutaka fungu la kumi, bali walikuwa wanatembea na wasanii wanaotaka kazi zao zionyeshwe Dstv.
Lakini producer ndio anabaki na kitita kirefu.waproducers ndo wana hali ngumu sio waigizaji
wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ...