Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

ACHA UONGO WEWE WEMA HAJAWAI KUIGIZA KWENYE HUBA
unaongea nini wewe wema alishawai kunja hadi million kumi kwa filamu mmoja
Mkuu, mbona nilionesha kutokuwa na uhakika kwenye post zangu?

Mimi sio mpenzi wa maigizo ya kibongo, sijui mengi.
Ungenirekebisha kwa kuweka ukweli na sio kunipinga bila kusema ukweli ni upi.
 
Bora hata hao wameongeza wanawake,mi huba ndo sielewi mwelekeo wake kila siku watu wanaanzisha mapenzi hovyohovyo sijui maudhui yake ni yapi yaani hata direction haieleweki kila siku watu wanapendana

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
Hata director naye haelewi inaelekea wapi.
Wabongo kwenye mtiririko na stroyline na matukio kutokea bado.
Ukitazama kina kwa mfano matokeo yako speed na ana mengi ya kukuonyesha. Njoo jua kali, miezi mitatu unasikia lazima profesa aseme ukweli. Yani katukoo kamoja kanakaa wee.
Mimi si mpenzo wa movie za kibongo ila wakenya nawaelewa elewa hata comedy zao zile ambazo si serious kama varshita zinanicheleshaga. Kuna crime and justice pia nliipenda.
 
This is exclusive!

Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.

Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.

Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!

Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.

Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!

Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…

Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwa kuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo awali kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.

Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.

Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.

Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,

Nifah.

View attachment 2825510View attachment 2825511
Kuna tamthiliya ilikuwa inaitwa Yalaiti ilienda baadae ikarudishwa nyuma alaf ikafutwa kumbe kuna kamchezo kanafanyika. Kuna kipindi pia tamthiliya ya Pazia ilisitishwa alaf ikarejea tena na kwenda kumalizika,.

Ila jaman Rushwa haiwezi kuisha kwa kweli, lakini Nikupongeze Samwel kwa Tamthiliya nzur sana, Chanda ni nzuri kuliko Pazia kwa kweli.
 
waproducers ndo wana hali ngumu sio waigizaji
Lakini producer ndio anabaki na kitita kirefu.

Japo sidhani kama Azam tv Wana hiyo michezo... Wote tunaona namna maproducers wanavyorotate , akitoka huyu, kesho huyu.
Na wamelimit namba ya episodes...
Huko DStv mtu mmoja anaruka hewani mwaka mzima.
 
Kwenye nchi hii, waadilifu tumebaki mimi, na Mama Samia na wengine kama 150 hivi...
wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ...
 
Back
Top Bottom