Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

Bongo ndio style ya viongozi wengi kuanzia sector binafsi na serikalini, mpaka tumesha tengeneza misemo mkono mtupu haulambwi na ndio maana hii nchi kiendelea ni ngumu.Sababu viongozi wengi vichwani mwao kuna mind za kupiga na ufisadi.

Watu hawangalii, content,talent,uwezo wa mtu bali wana angalia utaoa nini,ndio maana bongo hata ukitizama project zetu za ujenzi nyingi hazina ubora na watu wenye uwezo wakutoa vitu vyenye ubora kwa hela ile ile tuliyo itenga tunao.
 
Mimi naona hili jambo ni zuri sana katika sanaa ya maigizo bongo, italeta mapinduzi kwa kazi bora kupitishwa bila rushwa iliyozaa maigizo na waigizaji wabovu.
 
Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake!
 
Choyo kimempoza mkurugenzi, angeridhika na makubaliano ya awali, haya yasingempata.
 
Hii nayo umeipata Itoshe kusema wewe ni Mbeya Promax
 
Kuna familia kuanzia saa 12 jioni hadi saa 4 usiku ni tamthilia bandika bandua. Yaani hata taarifa ya habari ya saa 2 usiku unaangalia kupitia youtube kwani remote hugusi na TV yenyewe moja tu.
Hatari sana mkuu, inabidi ukubaliane nayo tu, Mimi najipa moyo taarifa nishazipata mitandaoni.

..........Furaha ya familia kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…