Kumekucha, hatimaye lango la mwisho limefunguliwa rasmi

Nimekuelewa sana maono yako ndo maono yangu. China ndo inaenda kuwa nchi yenye nguvu
 
Nimekuelewa sana maono yako ndo maono yangu. China ndo inaenda kuwa nchi yenye nguvu
Ongezea hapo!

Na wachina watakuja wengi Africa HASA Bongo tutawazalisha na kupata wabongo wa kichina wenye akili sana na ndio kizazi bora hicho kitaleta maziwa na asali hapa NCHINI!

Nimeshaanza kujifunza kichina ili nijue kutongoza kichina China!

Mkuu changamkia FURSA Hiyo!!
 
Siamini kama wanyonge watanzania watakua matajiri na hao wanaoitwa mapapa wawe ombaomba!!!

Serikali za ulaya eti zije kuomba msaada wa kibajeti kwa hizi nchi ombaomba zilizojaza walarushwa,wafujaji mali za umma,wezi,wanyanganyi nk ndani ya miaka mitano ijayo?

Tutafakari kwa kina zaidi
 
Unabii ni unabii tu, ni kosa kuupinga wala kuukataa.hata kama ni utabiri.
Ni kweli,chakufanya ni mtu kwenda kwa Mungu wake yeyote anayemwabudu na kumuuliza tupo msimu gani?(kuthibitisha),kama anauwezo wa kusikia sauti ya Mungu wake awe na uhakika jibu litakuwa ni ndiyo.Hakijibiwa hapana arudi hapa.
 
Kwahiyo Mama la Mama, Mama SaSHa anatupeleka katika nchi ya ahadi?

Au umemuona nani mwingine?
Sukuma gang wametoboa?
Anapaswa kujua kuwa amepata bahati ya kipekee kwa lango la msimu mpya kufunguliwa akiwa ameshika hatamu (mwenzake aliishia langoni kwa sababu maalumu). Akitumia akili vizuri na kupata watu makini wenye akili za kujua majira na nyakati hizi zinahitaji nini Tanzania tunaenda kung"aa duniani.( watu hao wapo wengi sana sema si rahisi kuwajua kutokana na kufichwa na mfumo kwani kila nchi ipo makini kupambana na hali yake).
 
Siyo huyo!

Inasemekana huyu atamalizia nyakati hizi chungu za zamani halafu YUPO mwenye maono kesha andaliwa NDANI ya chama atasimama Hapo mbeleni!YUPO top ten ya NEC pale!
Asante kwa nyongeza yako,kama watu wa ndani ndani wameshatambua nyakati hizi na kuanza kuandaa watu wakuendana nazo ni jambo zuri sana hili.
 
Inawezekana sana tu,inategemea na namna nchi zilivyojipanga na si lazima waje kuomba msaada wa kifedha huku,hata sisi kama nchi kujitegemea tu na kuishi maisha ya hali nzuri na watoto wetu itatutosha sana. Cha msingi nafasi hii ya dhahabu tusiichezee.
 
Nyongeza;Hili ndilo lango la msimu wa mwisho wa watu wema na waovu kuchanganyika,linalofuata soon litawatenga watu wema na waovu na hapo fujo yake itakuwa ya kutisha sana!.(naomba tuliache kwanza hilo tulipambanie hili).
 
Sawa kiongozi
Ila hujatoa hatma ya sukuma gang
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…