KUMEKUCHA! JNHPP Kuanza kujazwa maji Disemba 15, 2022

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
270
Reaction score
362
Kama ulikuwa na shaka kuhusu ujenzi wa Bwawa la JNHPP kwamba litaanza lini kufanya kazi ya kuzalisha umeme, basi wakati wa kumaliza kabisa shaka zako umefikia tamati.

Serikali imesema kwamba kuanzia Disemba 15, 2022 itaanza kujaza maji kwenye bwawa hilon ambapo maji hayo yatajazwa hadi Aprili mwaka 2023 ili kufikia kiwango ambacho kinatosha kuzalisha umeme.

Hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia 77.15% ambapo hadi kufikia tarehe 15, 2022 ambayo ni siku ya kuanza kujaza maji bwawani, ujenzi unatazamiwa kufikia 80% huku uzalishaji wa umeme ukitarajiwa kuanza rasmi Aprili 2024.

Ujenzi wa Bwawa la JNHPP ni wa teknolojia ya kisasa na uimara wake bwawa hilo litadumu kwa miaka 100 ijayo.
Mradi huu umeleta ajira nyingi sana kwa Watanzania. Mradi umeajiri watu 12,298 huku 11,190 sawa na 90.99% ni Watanzania na 1,108 sawa na asilimia 11.01% wakiwa ni raia wa kigeni.

Kubwa jingine kuhusu bwawa hili ni kwamba hata kuwe na ukame utakaodumu kwa miaka mitatu bwawa hili halito acha kuzalisha umeme kwani lina uwezo mkubwa sana wa kutunza maji.

Nimependa sana namna vile Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alivyoweza kusimamia vizuri kabisa miradi iliyoachwa na mtangulizi wake. Mama anafanya kazi kubwa sana na kwa hili anapaswa kupewa pongezi za dhati kabisa. Hongera sana Rais Samia Suluhu.

maxresdefault.jpg
 
Ila huu Miradi umekuwa na variation nyingi sana za kifisadi unaweza kugharimu hata 8trillion tofauti na bajeti ya 5trilion ila chawa watakuja kisifia kuwa mama anakimilisha Miradi yote ya mwendazake.
 
Nimetoka mjini Twitter si muda mrefu nimeiona umepost hii kitu,
Mbona unatumia nguvu sana
Acha matunda ya serikali yataonekana yenyewe
 
Kama ulikuwa na shaka kuhusu ujenzi wa Bwawa la JNHPP kwamba litaanza lini kufanya kazi ya kuzalisha umeme, basi wakati wa kumaliza kabisa shaka zako umefikia tamati.

Serikali imesema kwamba kuanzia Disemba 15, 2022 itaanza kujaza maji kwenye bwawa hilon ambapo maji hayo yatajazwa hadi Aprili mwaka 2023 ili kufikia kiwango ambacho kinatosha kuzalisha umeme.

Hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia 77.15% ambapo hadi kufikia tarehe 15, 2022 ambayo ni siku ya kuanza kujaza maji bwawani, ujenzi unatazamiwa kufikia 80% huku uzalishaji wa umeme ukitarajiwa kuanza rasmi Aprili 2024.

Ujenzi wa Bwawa la JNHPP ni wa teknolojia ya kisasa na uimara wake bwawa hilo litadumu kwa miaka 100 ijayo.
Mradi huu umeleta ajira nyingi sana kwa Watanzania. Mradi umeajiri watu 12,298 huku 11,190 sawa na 90.99% ni Watanzania na 1,108 sawa na asilimia 11.01% wakiwa ni raia wa kigeni.

Kubwa jingine kuhusu bwawa hili ni kwamba hata kuwe na ukame utakaodumu kwa miaka mitatu bwawa hili halito acha kuzalisha umeme kwani lina uwezo mkubwa sana wa kutunza maji.

Nimependa sana namna vile Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alivyoweza kusimamia vizuri kabisa miradi iliyoachwa na mtangulizi wake. Mama anafanya kazi kubwa sana na kwa hili anapaswa kupewa pongezi za dhati kabisa. Hongera sana Rais Samia Suluhu.

Ili tuijaze haraka ni vizuri kila raia apeleke maji kwenye ndoo mbili za lita 20.
 
Maji hayo hayo ilipaswa yajazwe mwaka Jana!

Lkn alipoingia mzee wa ten percent, kila kitu kimeharibika
 
Back
Top Bottom