hapa kuna ubabaishaji, au kuweka chumvi nyingi pasipokuwa na lazima.Hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia 77.15% ambapo hadi kufikia tarehe 15, 2022 ambayo ni siku ya kuanza kujaza maji bwawani, ujenzi unatazamiwa kufikia 80% huku uzalishaji wa umeme ukitarajiwa kuanza rasmi Aprili 2024.
Hiyo asili mia 77.15 imejengwa kwa muda gani? Hiyo iliyobakia kufikia asilimia 80 itamalizika kwenye siku kadhaa tu?
Hizi ni porojo zilezile zilizozoeleka.Ujenzi wa Bwawa la JNHPP ni wa teknolojia ya kisasa na uimara wake bwawa hilo litadumu kwa miaka 100 ijayo.
Mradi huu umeleta ajira nyingi sana kwa Watanzania. Mradi umeajiri watu 12,298 huku 11,190 sawa na 90.99% ni Watanzania na 1,108 sawa na asilimia 11.01% wakiwa ni raia wa kigeni.
Hawa waTanzania waliajiriwa huko wamejengewa uwezo, ili kama pakitokea uhitaji wa dharura watausimamia wao bila ya kuwaita tena hao wanaojenga?
Tukitaka kujenga bwawa jingine dogo zaidi ya hili, hawa waTanzania wenzetu wataimudu kazi hiyo?