KUMEKUCHA! JNHPP Kuanza kujazwa maji Disemba 15, 2022

KUMEKUCHA! JNHPP Kuanza kujazwa maji Disemba 15, 2022

Leo 15 12 2022 nimewahi siti kwenye mawe ndani ya mto mkavu Ruaha niyaone vizuri maji yanayokwenda kulijaza bwawa la umeme la Julius Nyerere.
Wewe unafikiri Mto Rufiji unategemea chanzo kimoja?. Kuna mito mingi mikubwa inaingia Rufiji hasa kutoka Morogoro. Kilombero, Luwegu, Mbarangandu, Kihansi na mingine ambayo inatoka kwenye hari ya hewa inayotofautiana(Mingine milimani au mingine misituni). Kwahiyo kama Ruaha kuna ukame basi Kilombero au luwegu inarisha.
Screenshot_20221215-071139.jpg
 
Labda aliyeleta uzi yupo busy anatafuta nini cha kusifia kwa sasa anasahau kuleta mrejesho wa aliyosema mwanzo...

Au bado hapajakucha....
 
Kubwa jingine kuhusu bwawa hili ni kwamba hata kuwe na ukame utakaodumu kwa miaka mitatu bwawa hili halito acha kuzalisha umeme kwani lina uwezo mkubwa sana wa kutunza maji.


Hapa inabidi wataalamu wakae na watufafanulie sie tusiojua, ukame wa miaka 3 sio mchezo, huu wa miezi kadhaa tu unatusumbua sembuse wa miaka 3 ?!!
 
Crane la Tani 26 halijafika, mnatuambia mnajaza maji😠😠
 
Ngoja na mm niweke kambi hapa... nisubiri kuona bwawa linavyojazwa maji...
 
Hakuna bwawa duniani linajaa kwa muda mrefu hivi hata kama mmefungulia maji ya bombardier ya nyumbani week limejaa
 
Leo ni siku mhimu sana kwa ukombozi wa kiuchumi wa taifa letu. Ilipaswa kuwa public holiday tukisherekea kujazwa maji JNHPP. Tunatarajia rais au waziri mkuu kuwepo kwenye tukio hilo akikata utepe na kuyafungulia hayo maji!
 
Sa100 yupo anatembeza bakuri..lingekua linaanza kujazwa leo..tungeona misafara ya wahuni huko kwenye bwawa wakishuhudia maji yakiruhusiwa kuingia bwawani..huku tukio likiwa live.

Nawakumbusheni tu viongozi wa ccm ni kikundi cha walaghai hasa hawa wa awamu hii ya wahuni.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kama ulikuwa na shaka kuhusu ujenzi wa Bwawa la JNHPP kwamba litaanza lini kufanya kazi ya kuzalisha umeme, basi wakati wa kumaliza kabisa shaka zako umefikia tamati.

Serikali imesema kwamba kuanzia Disemba 15, 2022 itaanza kujaza maji kwenye bwawa hilon ambapo maji hayo yatajazwa hadi Aprili mwaka 2023 ili kufikia kiwango ambacho kinatosha kuzalisha umeme.

Hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia 77.15% ambapo hadi kufikia tarehe 15, 2022 ambayo ni siku ya kuanza kujaza maji bwawani, ujenzi unatazamiwa kufikia 80% huku uzalishaji wa umeme ukitarajiwa kuanza rasmi Aprili 2024.

Ujenzi wa Bwawa la JNHPP ni wa teknolojia ya kisasa na uimara wake bwawa hilo litadumu kwa miaka 100 ijayo.
Mradi huu umeleta ajira nyingi sana kwa Watanzania. Mradi umeajiri watu 12,298 huku 11,190 sawa na 90.99% ni Watanzania na 1,108 sawa na asilimia 11.01% wakiwa ni raia wa kigeni.

Kubwa jingine kuhusu bwawa hili ni kwamba hata kuwe na ukame utakaodumu kwa miaka mitatu bwawa hili halito acha kuzalisha umeme kwani lina uwezo mkubwa sana wa kutunza maji.

Nimependa sana namna vile Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alivyoweza kusimamia vizuri kabisa miradi iliyoachwa na mtangulizi wake. Mama anafanya kazi kubwa sana na kwa hili anapaswa kupewa pongezi za dhati kabisa. Hongera sana Rais Samia Suluhu.

kama waziri wa umeme atakuwa huyu huyu mtoto wa mropokaji si ajabu ikawa vinginevyo
 
Back
Top Bottom