OffOnline
JF-Expert Member
- Apr 23, 2022
- 644
- 478
SIMIYU: KAMPUNI ZILIZOSAMBAZA DAWA FEKI ZA PAMBA KITANZANI
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Ndugu David Kafulila amesema timu aliyounda kuchunguza ukubwa wa tatizo la dawa feki za pamba itamaliza kazi siku ya Jumatatu, Juni5, 2022.
Kafulila amesema hayo kufuatia malalamiko ya wakulima kuhusu bodi ya pamba kusambaza dawa feki ambazo zimeshindwa kuteketeza wadudu wa pamba na hivyo kuathiri mavuno..
"Dawa za pamba zilizosambazwa msimu huu ni feki. Hata uwachukue wadudu wenyewe uwaweke kwenye chupa la dawa ya pamba hawafi" walisema wakulima kwenye mkutano wa Katibu Mkuu CCM , Comrade Chongoro katika mkutano wake wilayani Meatu.
"Kwanza ninawapongeza wakulima kwa mwitikio mkubwa msimu huu kiasi ambacho mwelekeo unaonesha tutavuna zaidi ya kilo milioni 200 kutoka kilo milooni 82 msimu uliopita kwa mujibu wa makadirio ya bodi ya pamba. Kilo zaidi ya milioni 200 ni rekodi ya kwanza tangu mkoa uzaliwe.
Bei ya pamba msimu huu itavunja rekodi ya zaidi miongo 3. Lakn niwahakikishie kwamba timu niliyounda ya tathimini kuhusu ukubwa wa tatizo la dawa feki za pamba itanikabidhi ripoti ijumaa, Juni03, 2022 na niwakikishie Serikali itachukua hatua kali dhidi ya kampuni zilizouzia dawa feki bodi na kisha bodi kusambaza kwa wakulima kwani kosa hilo ni sawa na uhujumu uchumi" alisisitiza RC- Kafulila