Kumekucha: kamati ya waamuzi (ZFF) yasema Simba ilipendelewa

Hii makosa ya marefa huwa ni makubwa Sana sijui kwann huwa hayapewi uzito unaostahili. Hivi kweli kamati inaweza ikasema uzito WA Kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu? Hivi wanajua kama Hilo Kosa ndio limesababisha Singida kutolewa? Unasemaje Kosa halina uzito?
Na singida nao walifanya kosa kufungwa.
 
Kamati ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), imesema kuwa Mwamuzi Nasri Salum hakustahili kuipa Simba kona iliyoifanya ipate bao la kusawazisha, katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, wakati ikicheza na Singida Fountain Gate jana kwenye Uwanja wa Amaan.

Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Waziri Shekha amesema uamuzi wa kuipa Simba kona katika dakika za nyongeza, haukuwa sahihi na kwa mwamuzi huyo alifanya makosa, japo kamati hiyo haiwezi kumpa adhabu.

"Nilikwambia kwamba tutachunguza na tumekutana leo, tumebaini kwamba kulikuwa na makosa ya mwamuzi. Haikupaswa kuwa kona. Hakuna sehemu ambayo mpira ulichezwa na mchezaji wa Singida na kipa akaudakia nje, hivyo haikuwa sahihi kuwa kona,” amesema na kuongeza;

“Ni makosa ya kibinadamu na ndio kosa pekee tumeliona baada ya kupitia ripoti na marudio ila sehemu zingine zote alikuwaa sahihi. Uzito wa kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu refa huyo ukizingatia amekuwa akichezesha vyema mechi nyingi.”
511b8578af1f57c761f282fdf2558918.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona hii ilikuwa Kamati ya UTO.
Chenye hasira ya kufurushwa nje ya mashindano.
Lakini nasikia walichezesha timu ya vijana akina.
Mauya
Kibwana
Romalisa
Mzimze
Kibabage
Moroko
Skudu
Msheri
Shekan
Nk.
 
Kule tanga Ali Salim alitoka kwenye mstari na kule Zanzibar je alitoka kwenye mstari? Dadeki mtu akifanya vzuri awatak kukubali mseme na kule zenj
Watu wanalalamikia kona, wewe unakuja na taarabu zako?
wawapi wewe?
 
Hilo lilikuwa wazi toka ile siku baada ya dakika za nyongeza kuisha.

Vipi kuhusu team ya APR malalamiko yao?

Mbeleko kabisa ile bora Singida F na APR zishikilie msimamo wa kutoshiriki hiyo mapendeleo cup!
 
Kamati ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), imesema kuwa Mwamuzi Nasri Salum hakustahili kuipa Simba kona iliyoifanya ipate bao la kusawazisha, katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, wakati ikicheza na Singida Fountain Gate jana kwenye Uwanja wa Amaan.

Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Waziri Shekha amesema uamuzi wa kuipa Simba kona katika dakika za nyongeza, haukuwa sahihi na kwa mwamuzi huyo alifanya makosa, japo kamati hiyo haiwezi kumpa adhabu.

"Nilikwambia kwamba tutachunguza na tumekutana leo, tumebaini kwamba kulikuwa na makosa ya mwamuzi. Haikupaswa kuwa kona. Hakuna sehemu ambayo mpira ulichezwa na mchezaji wa Singida na kipa akaudakia nje, hivyo haikuwa sahihi kuwa kona,” amesema na kuongeza;

“Ni makosa ya kibinadamu na ndio kosa pekee tumeliona baada ya kupitia ripoti na marudio ila sehemu zingine zote alikuwaa sahihi. Uzito wa kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu refa huyo ukizingatia amekuwa akichezesha vyema mechi nyingi.”
Vipi kuhusu muda uliongezwa maana ilikuwa dakika 6 tukaenda mpaka dakika 8
 
Unachotakiwa kujua alipangalo mungu
Bin-adamu huwezi pangua
Over
 
Back
Top Bottom