Kumekucha, List of shame inanukia!

Kumekucha, List of shame inanukia!

Ngoja tuone

Kimya kingi kina mshindo mkuu. Ngoja wenye uzalendo na nchi hii waibuke kutoka machimboni waliko.

Hayupo mwenye kuwavumilia hawa wanaotudanganya, kutuibia na hata kutubambukizia kesi kwa jina la kuwa wao ni serikali.

Izingatiwe kwenye mada wameyatamka wao wenyewe Wala siyo sisi.

Hatuwezi kuwaonea haya watu hawa.
 
Vyama vya siasa havitegemewi kuwa na malaika. Uchafu wa mtu ni wake labda kama una baraka za chama chake.

"Vyama vya siasa vinategemewa tu kuwa na agenda za maanq zenye kuwavutia watu."

Agenda zetu za wazi za kutaka usawa, haki na maisha bora kwa watu haziwezi kumvumilia mwizi bila kujali alipo.

Kwamba kuna rundo la mapesa lilishia China? Tunataka ushahidi upi kuwaaibisha wenye kuhusika? Labda kama tunadhani kuna majini yalifanya hilo?

Kwani waliozikusanya pesa hizo wanasema walizipeleka wapi au kwa nini walizipeleka huko? Kwa nini kuoneana aibu au kulindana hapa? Kila mmoja na akaubebe msalaba wake mwenyewe.

Kwamba hatujui mlolongo wa utunzaji wa pesa za serikali? Kwamba hata kikinuka kama hivi nani wanapaswa kuwajibika hatuwajui? Labda kama ni shamba la bibi.

Ushahidi upi tunaoutaka?

Kwani mzee Lowassa na akina Msabaha waliachia ngazi kwa ushahidi upi? Wengine si walisema walikuwa mbangusilo tu?

Au list Ile pendwa of shame ilituathiri sisi nini? Haikusaidia kuwawajibisha watu ile?

Wana tuingieni chimbo. Wote waliohusika kwenye hili wakapate kuanikwa peupe.

Hata kama Mbowe, Lissu, Samia, Mpango, Luoga, Dotto, Zitto, Rungwe, wewe, mimi nk walihusika na waanikwe tu!
"Agenda za kuwavutia watu".

Muhimu ni kuchunga hizo agenda zinazowavutia watu zisije kugeuka mtego kwako, ukisema fulani yuko hivi, simamia hapo hapo, ili usijekubanwa na mazingira mbele ya safari ukajikuta unabadilika, hivyo kuwaacha wale watu uliowavutia kwa agenda zako wasijue la kufanya.
 
"Agenda za kuwavutia watu".

Muhimu ni kuchunga hizo agenda zinazowavutia watu zisije kugeuka mtego kwako, ukisema fulani yuko hivi, simamia hapo hapo, ili usijekubanwa na mazingira mbele ya safari ukajikuta unabadilika, hivyo kuwaacha wale watu uliowavutia kwa agenda zako wasijue la kufanya.

Agenda za kupigania haki, usawa na ustawi wa watu ni agenda zenye kuwavutia watu. Kwenye agenda hizo koleo na liitwe kwa jina lake. Mwizi na aitwe mwizi.
 
Ingawa siasa ndivyo zilivyo, ila muda unaongea...
 
JINSI CHAMA CHA MAPINDUZI KINAVYOJUA KUJISAFISHA CHENYEWE NA HATIMAYE, KUKOSEKANA KWA HOJA MPYA AMBAYO MTANZANIA ATATAKA KUISIKIA, ALL GENIUS KNOW THIS....
 
JINSI CHAMA CHA MAPINDUZI KINAVYOJUA KUJISAFISHA CHENYEWE NA HATIMAYE, KUKOSEKANA KWA HOJA MPYA AMBAYO MTANZANIA ATATAKA KUISIKIA, ALL GENIUS KNOW THIS....

Genius humo kwa wahuni? Bashiru, Polepole na wa namna hiyo? Wahuni si watu wazuri. Kataa wahuni.
 
Back
Top Bottom