Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!

Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!

Mbona mambo yako wazi kabisa??
Mwenye Mzigo ni Kinje Ngombale Mwiru. Huyu anajulikana na narudia kusema tena ndiye aliyetumika kumuharibu mtoto wa Sitta ALIYEMZAA kwa mkewe mkubwa aitwaye Valeria(rip).

Huyu tena anashirikiana na Shomar Kimbau sijui kwanini watu wanawaonea aibu hawa watu.
Makonda ana habari hizi ? Maana alituambia sijui kabla hujatajwa ushafuatiliwa miaka 10 nyuma

Wacha tufukue makaburi hamna namna

Halafu kuna wehu walitaka eti kuifungia Jf

Long live Jf
 
Sasa wametajwa
Hawajatajwa. Makonda alikuwa awataje kwenye ile orodha yake ya episode 3 lakini baada ya bunge kumpiga stop imebidi atii amri ya bunge kwani ndiyo check and balances ya mihimili hii mitatu. Ndiyo hivyo tena, tusahau kutangaziwa majina hayo ya mapapa 97 wa biashara hii. Bunge kama wawakilishi wa wananchi wamepiga stop kuyatangaza majina ya washukiwa wa network ya madawa. Tumekosa pale patamu. Sijui kwa nini Makonda hakuanza na pale patamu. Angeanza na mapapa na kumalizia na wasanii/ wabebaji wa madawa hao + mateja, ingekuwa poa zaidi ila nchi ingetikisika na ku vibrate. Kwa busara za wabunge wetu hawakutaka nchi yetu i vibrate maana tunaweza pata madhara zaidi ya yale yaliyopatikana huko Kagera yaliyosababishwa na vibration ya eneo hilo.
 
Sasa unatoa ushirikisno upi taja majina kwa kuwasaidia afisa upelelezi kumbe watu mnawajua wahusika afu mnaweka mafumbo kwani sisi ni watabiri acheni mambo ya kuficha ficha taja watajane hadi waishe wote
 
Hawajatajwa. Makonda alikuwa awataje kwenye ile orodha yake ya episode 3 lakini baada ya bunge kumpiga stop imebidi atii amri ya bunge kwani ndiyo check and balances ya mihimili hii mitatu. Ndiyo hivyo tena, tusahau kutangaziwa majina hayo ya mapapa 97 wa biashara hii. Bunge kama wawakilishi wa wananchi wamepiga stop kuyatangaza majina ya washukiwa wa network ya madawa. Tumekosa pale patamu. Sijui kwa nini Makonda hakuanza na pale patamu. Angeanza na mapapa na kumalizia na wasanii/ wabebaji wa madawa hao + mateja, ingekuwa poa zaidi ila nchi ingetikisika na ku vibrate. Kwa busara za wabunge wetu hawakutaka nchi yetu i vibrate maana tunaweza pata madhara zaidi ya yale yaliyopatikana huko Kagera yaliyosababishwa na vibration ya eneo hilo.
Na jana Makonda akasema inaweza fika mpaka awamu ya Saba (7), maana kuna mengi ambayo hatuyafahamu/hatuyajui
 
Na Mwandishi Wetu
IMEVUJA! Staa muuza nyago kwenye video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu za Kibongo, Agnes Gerald &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Masogange' na shosti wake, Mellisa Edward kabla yakupandishwa kizimbani kwa msala wa dawa za kulevya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];unga' Afrika Kusini waliingizwa kwenye chumba cha mateso kwa saa 24 ili kutaja waliowatuma.

Habari kutoka kwa chanzo chetu kilichopo jijini Johannesburg nchini humo zilidai kuwa baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, walipelekwa polisi ambapo walichukuliwa maelezo.

Ilielezwa kuwa mwanzoni waligoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.

MATESO SAA 24
Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema aliyewatuma.

USHUHUDA
"Unajua Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.

"Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.

"Kwanza utaanzia kwenye chumba kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.

"Wakishakuingiza mle ndipo utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung'ata mwili mzima, zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.

"Kama bado ukijifanya mbishi au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja ndogo kwenye waya wa umeme.

"Si unajua tena waya wenye umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.

"Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.

"Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.

WALIOWATUMA
"Baada ya mateso hayo, waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8," kilisema chanzo hicho ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa wa Rissik, Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi kukumbwa na mkasa kama huo.

MTOTO WA KIGOGO ATAJWA
Habari za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).

Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha mwili wa msanii Albert Mangweha &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Ngwea' aliyefia Johannesburg Juni, mwaka huu.

Ilivuja kuwa mwingine aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];mtoto wa mjini' Mangunga likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe.

Gazeti hili lilipozungumza na Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kupewa majina hayo lakini akaliomba gazeti hili kutoyachapisha kwa sasa kuepuka kuvuruga ushahidi.

ULINZI KAMA SHEHE PONDA
Baada ya polisi wa upelelezi na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na maelezo ya mabinti hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti 19, mwaka huu chini ya ulinzi mkali kama ule &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];anaowekewaga' Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anapofikishwa kwenye mahakama mbalimbali nchini kwa kesi zake za madai ya uchochezi.

WAPANDISHWA TENA KORTINI
Habari kutoka Sauzi zilieleza kuwa akina Masogange walipandishwa tena kizimbani hivi karibuni ambapo tayari kesi yao imeanza kuunguruma ikielezwa kuwa endapo watakutwa na hatia watakula mvua ya kifungo si chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi hiyo.

Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga.
 
Back
Top Bottom