Kumekucha: Mawakili wa Mbowe waweka pingamizi kesi ya Ugaidi

Kumekucha: Mawakili wa Mbowe waweka pingamizi kesi ya Ugaidi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mawakili wa Freeman Mbowe ambaye ni Mwamba wa siasa za Tanzania, anayeshitakiwa na serikali ya Tanzania kwa makosa ya Ugaidi wa thamani ya hela za madafu shilingi laki 6, Wameiwekea pingamizi kesi hiyo kwa madai kwamba Mahakama ya Uhujumu uchumi na Rushwa, ambako kesi hiyo imepelekwa haina uwezo wa kusikiliza kesi ya Ugaidi.

Mahakama imepokea pingamizi hilo na inatarajia kulitolea uamuzi kesho saa 3 asubuhi.

Mungu ibariki Chadema



=========

Mahakama kutoa uamuzi pingamizi la Mbowe na wenzake​

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kesho Jumatano Septemba 1, 2021 itaamua pingamizi la Mbowe na wenzake kama mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza kesi yao ama la.

Mbowe na wenzake wameipinga mahakama hiyo kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao kwa mashtaka ya ugaidi na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya kawaida na si hiyo ambayo ni Divisheni Maalum.

Serikali imepinga hoja hizo ikidai kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 ya Mwaka 2016 makosa yaliyoko kwenye Sheria ya Ugaidi yaliwekwa kwenye Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba kwa hali hiyo mahakama hiyo ya ufisadi ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka yao.

Jaji Elinazer Luvanda baada ya kusikiliza hoja za pande zote ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano asubuhi atakapotoa uamuzi.

Chanzo: Mwananchi
 
Ni Jambo jema Sana!
In deed, Mungu Bariki CHADEMA, pia mbariki mbowe mtoe katika mikono ya watesi wake!

Lakini 600k sio hela ya madafu kwa uchumi huu wa Kati wa Magu na Dictator wa kike ndg Erythrocyte , tunapambana mwezi mzima hatuipati!
investment ya Ugaidi haiwezi kuwa duni kiasi hicho , fuatilia mafungu ya Alshabab
 
Mungu ibariki Chadema
1326.gif
 
Back
Top Bottom