johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mchungaji Msigwa ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa anayemaliza muda wake amepinga Mjumbe wa sekretari Mrema kusimamia Uchaguzi jimboni kwao
Source Jambo TV
Yajayo yanafurahisha😀
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya Nyasa, ambaye pia anagombea kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho, Mchungaji Peter Msigwa, amewasilisha malalamiko dhidi ya Mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho, John Mrema, kwa kile alichokitaja kuwa mgongano wa masilahi katika uchaguzi wa kanda wa chama.
Katika barua aliyomwandikia Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, Msigwa ameonesha wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa John Mrema. Ameeleza kuwa Mrema ameonesha wazi kuegemea upande wa mgombea mwenza wa uenyekiti wa kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, na kuonesha dalili zote za rushwa, kinyume na "Kanuni ya 1 (vi) ya Mwongozo wa Chama dhidi ya Rushwa Kwenye Uchaguzi ndani ya Chama Toleo la 2012."
“Tarehe 24 Mei, 2024 kabla na baada ya uchaguzi wa chama wa Mkoa wa Iringa, kuanzia majira ya asubuhi lakini pia saa kumi na mbili jioni alikutana na mgombea mwenzangu wa Kanda ya Nyasa katika nafasi ya uenyekiti Mhe. Joseph Mbilinyi, Twiga Night Club ambapo mgombea mwenzangu aliweza kununua kreti 4 za bia wakaendelea kunywa na msimamizi huyu wa uchaguzi mpaka majira ya saa sita usiku,” imeeleza barua ya Msigwa.
Msigwa ameendelea kueleza kwamba kwa nyakati tofauti, Mrema amekuwa akiwapigia simu wajumbe (wapiga kura) katika ngazi ya kanda, akiwashawishi wasimchague Msigwa bali wamchague Sugu, kwa madai kuwa hayo ni maagizo ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.
Aidha, Msigwa amemtuhumu Mrema kumsaidia mgombea uenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) kanda ya Nyasa, Vitusi Nkuna, kwa kueleza kuwa tarehe 26 Mei, 2024 Mrema, ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi, alipanda gari ya Nkuna kutoka Iringa mpaka Makambako, na kwamba siku mbili nyuma alikunywa naye pombe mpaka usiku wa manane.
Kutokana na mambo hayo, Msigwa ameomba Mrema aondolewe kwenye shughuli zinazohusiana na usimamizi wa uchaguzi na waletwe wasimamizi wengine ambao hawana masilahi binafsi katika uchaguzi huo ili haki iweze kutendeka kwa wagombea wote bila ubaguzi wala upendeleo.
Wengi wetu tumekua tukielezea rushwa iliokithiri ndani ya Chadema. Kwa bahati mbaya kuna ambao walikua hawataki kuuona ukweli au walikua wanaona ukweli na kuufumbia macho. Kwa bahati mbaya au nzuri, mchuano kati ya Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi umefanya matendo ya rushwa ndani ya taasisi yao uanikwe na wanachama wenyewe hivyo inakua ngumu kupuuza.
Disemba mwaka 2022, ni John Mrema huyu huyu ambae anatumika kuchafua uchaguzi wa Kanda ya Nyasa alitoa shutuma za rushwa kwenye uchaguzi ndani ya CCM. Wakati huo John Mrema alinukuliwa akisema yafuatayo, "Washughulike kwanza na rushwa kwenye uchaguzi ndani ya chama chao ambayo imekithiri imeota mizizi , kuna Video Clip zimesambaa nchi nzima na hatuoni hata mmoja akinyanyua mdomo akichukua hatua kuwa fulani achukuliwe hatua, hatuoni TAKUKURU ikichukua hatua, matokeo yake tunaona wapo kimya tu.”
Aliendelea kusema yafuatayo, "Kuna matukio mabaya yamefanywa na wana CCM lakini hawajawahi hata kukemea , Katibu Mkuu wa UVCCM alipokuwa Katibu wa Chama kule Iringa alitoa kauli zenye ukakasi sana badala yake alipandishwa cheo akapelekwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Arusha, nako akatoa kauli mbaya kabisa hasa kwenye uchaguzi mkuu wa 2020, wakaona huyu anastahili akapandishwa cheo na siyo kukemewa ndiyo akawa Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana Taifa" amesema.” Ajabu ni huko huko Iringa ambapo Mrema anatuhumiwa kufanya uchafu.
Ni siku chache tu zimepita ambapo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAWACHA), John Pambalu alipo bwaga manyanga kwenye kinyanganyiro cha kumtafuta mwenyekiti wa Kanda ya Victoria. Pambalu Alidai kuwa hapo awali walizoea kushuhudia wanachama wao wakinunuliwa na kuhamishiwa vyama vingine, lengo likiwa ni kudhoofisha nguvu za CHADEMA. Hata hivyo, alieleza kuwa sasa mbinu zimebadilika, kwani baadhi ya wanachama wananunuliwa na kubakishwa ndani ya chama ili kukivuruga zaidi kutoka ndani.
Aliekua anashutumiwa kutoa rushwa ni mgombea mwenzie na mwenyekiti aliekua anatetea nafasi yake Ezekia Wenje. Wenje alitangazwa mshindi wakati Pambalu akitoweka ukumbini wakati uchaguzi unaendelea.
Swali ni je, tunaendeleaje kuwaamini Chadema pale wanapokemea rushwa wakati rushwa imekithiri ndani ya chama chao? Kwanini wanakua wanafiki wakati viongozi wakuu wa chama chao ikiwemo Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Tundu Lissu, wanatoka hadharani na kuiambia umma kuwa rushwa ipo ndani ya Chadema? Mpaka lini baadhi ya wananchi wetu wataendelea kuhadaliwa na hawa wanaharakati wa kimkakati?
Mpaka sasa tunavyo zungumza huko mitandaoni utaratibu wa kumchangia Tundu Lissu kununua gari la kifahari unaendelea. Ndani ya siku nane mchango umefikia milioni 25 na kasoro. Ni dalili nzuri ya kwamba Watanzania wengi wanaanza kufunguka macho na kugoma kutoa hela zao kwa ajili ya kumchangia mtu kununua gari la milioni 400. Gari aina ambayo wao wenyewe Chadema kila siku wanaipigia serikali kwa matumizi mabaya ya fedha za wananchi kwa kununua magari ya kifahari.
Sisi wapenda nchi tutaendelea kuwahabarisha wananchi taarifa mbalimbali na kumulikia matokeo yote ya Chadema yanayoenda kinyuma na wanayo yahubiri majukwaani. Na huu ni chaguzi za kanda tu tunasubiria kitimtim cha uchaguzi wa kitaifa pale ambapo Lissu na Mbowe wanatendeleza vita zao kwa ngazi ya kitaifa.
Nimalizie na nukuu ya Rais Samia Suluhu Hassan ambae tarehe 17 ya mwezi Januari aliwaonya wana-CCM kwa kuwaambia, “ELFU KUMI KUMI ZENU UBUNGE HAMPATI” RAIS SAMIA AWAONYA WANATOA RUSHWA”. Niwaulize, tokea shutuma za rushwa ndani ya Chadema zianze kutolewa na viongozi wa chama hicho ni lini mmemsikia mwenyekiti wao Freeman Mbowe akitoka hadharani na kukemea tabia hiyo? Jibu bila shaka mnalo.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa