Kumekucha: Wakili msomi Peter Kibatala na Tundu Lissu kumtetea Ney wa Mitego mahakamani

Kumekucha: Wakili msomi Peter Kibatala na Tundu Lissu kumtetea Ney wa Mitego mahakamani

Ney katumia fasihi tu hajataja jina lolote la kiongozi na hakuna neno la kashfa lolote alilolitaja kwenye wimbo wake, anayetakiwa kukamatwa na kushtakiwa ni yule anayejihisi ameimbiwa yeye. Huwezi kumfunga mtu kwa kutoa mawazo yako kichwani na kutafsiri. Labda kama mahakama itathibitisha pasipo na shaka kuwa kiongozi fulani hapendi kushauriwa, au kiongozi fulani ni kweli amepoteza marinda hivyo kuimbwa ni kumdhalilisha, au Bashite wa kolomije ni jina halali kisheria la kiongozi fulani,
Ukweli haujifichi, Ney ni mwanafasihi
 
WENGI WENU "KIPENDACHO ROHO" HAMUWEZI SIKIA MATUSI.
 
Kikujishuku nako si Tania nzuri hata kidogo,Ney wadongoe hao.
 
Sanaa ni kioo cha jamii, ni kile kinachofanyika ktk maisha yetu ya kila siku.....ukiona reaction km hizi ni jambo zuri sn na ushindi ktk tasnia ya sanaa, ni kielelezo kwmb ujumbe umefika, umepokelewa na umeeleweka vizuri na hadhira.
 
Nilijua matokeo yake baada ya ile ishu ya kashifa juu ya makanisa, nkajua jamaa anapotea si muda, maswala ya MUNGU hakuna binadam ana mamlaka ya kuyasema HATA kama uendeshwaji wake si mzuri, ndo MUNGU anatumia watu kumdhoofisha
 
Ney katumia fasihi tu hajataja jina lolote la kiongozi na hakuna neno la kashfa lolote alilolitaja kwenye wimbo wake, anayetakiwa kukamatwa na kushtakiwa ni yule anayejihisi ameimbiwa yeye. Huwezi kumfunga mtu kwa kutoa mawazo yako kichwani na kutafsiri. Labda kama mahakama itathibitisha pasipo na shaka kuwa kiongozi fulani hapendi kushauriwa, au kiongozi fulani ni kweli amepoteza marinda hivyo kuimbwa ni kumdhalilisha, au Bashite wa kolomije ni jina halali kisheria la kiongozi fulani,
Always mtu mwenye makosa huwa anajihisi
 
Kosa kuikashfu serikali period... Hakuna kuwekewa dhamana
 
Katika ukurasa wake wa FB peter kibatala amesema watapigana mpk tone la mwisho leo hii 27/3/2017 kuhakikisha ney wa mitego anapelekwa mahakamani na anapewa dhamana.

Ameandika hawawezi kumwacha mpigania haki peke yake, pia kibatala ametoa pongeze za dhati kwa ney wa mitego kwa kuwa jasiri. Mungu ibariki Tanzania yetu

View attachment 487319
Hongera Ney we are together bro
 
Back
Top Bottom