Kumekuwa na sintofahamu kwa wananchi wanaohamishwa kutoka vijiji vya Utegi, Wilaya ya Rorya. Hizi ni baadhi ya maswali yanayojitokeza:
- Hawa wananchi hawajaelezwa ni kwa nini wanahamishwa.
- Wananchi hawa hawajaelezwa ni wapi wanapopelekwa.
- Malipo yao hayakuzingatia tathmini kama ilivyo utaratibu wa Serikali.
- Ni kwa nini malipo ya ardhi yao hayakuzingatiwa katika tathmini ya malipo yao?
- Ni kwa nini Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikilalamikiwa sana katika suala la uhamisho wa wananchi, mfano Kata ya Nyatwali - Bunda, Ngorongoro - Arusha, Hifadhi ya Arusha National Park, Mbarali n.k.?