Kumfanyisha Interview Medical Doctor aliyethibitishwa na Baraza la Madaktari (MCT) ni dharau kubwa sana

There ur aaa...
 
Interview kwa daktari ya nini? Nini unachokipima ukimfanyia interview MD wa entry level ?
 
Interview kwa daktari ya nini? Nini unachokipima ukimfanyia interview MD wa entry level ?
1- Experience
2-Uwezo wa kutoa maamuzi
3-Kujiamini
4-Kujua weakness zake
5-Kumjua kiundani
6-Communication Skills (unakuta mtu anaongea sauti haitoki, hana confidence au wengine wanaongea kwa dharau au mikogo mingi).

Mfano mdg tu, umeajiri mtu kumbe ni Shoga, amekuja kuripot siku ya kwanza Hospital nzima inasimama kushangaa nini kinaendelea..

(Sina maana Mashoga wasipewe kazi)

Utajuaje yote hayo kama linakuja jina na kulipitisha bila kumjua unaempitisha ni nani?
 
Wahasibu na wanasheria mnasoma miaka mitatu ndio maana ni muhimu kukaguliwa kaguliwa sana tofauti na madaktari. Madaktari wanapewa leseni ku deal na maisha ya watu, nyie mnapata vyeti kucheza na makaratasi.
UDSM sheria ni miaka minne, kwa hoja yako Ina maana wanaograduate sheria UD hawapaswi kufanyiwa interview

Pia sio kozi zote za afya ni miaka 5, lakini wote walikua hawafanyiwi interview.

Architecture ni miaka 5 Ila wanafanyiwa interview.

Nimekueleza hayo ujue kuwa miaka sio issue
 
Usilinganishe takataka hizo na fani ya udaktari wewe. Sio kitonga jaribu kusoma MD uone. Why ni daktari pekee akimaliza degree yake ya kwanza anapewa hadhi ya PhD or MD?
Hata usome PhD bado hulingani na iyo MD ya dokta bana. Wote tumepita shule tunajua mziki wake jamani,acha tuwaheshimu madaktari
 
Lazima upigwe interview maana unaelekea ku-perform kwenye miili ya watu sasa sio kwenye daftari tena.
 
Mwanzo mgumu ila baadae mtazoea tu kufanya usaili
 
Sasa kam Ajira mpk mitihani , necta, vyuo na college mitihani ilikuwa ya kazi gani , ivi MD akakae afanye mitihan kweli !! Watu wajinga sana hii nchi
 
Kwenye udaktari suala muhimu ni ufaulu tu na leseni, haya mengine ya interview ni njia ya kupunguza watu kwa sababu ya ufinyu wa ajira.
Kwaio daktari inatakiwa awe amefaulu tu ila ata kama ana tabia mbovu fresh au hana customer care, ubinadamu nk. Yeye apewe tu kazi au sio
 
Na akipata ajira huko Tamisemi ndio dharau za madiwani wa darasa la 7 atazijua vizuri
 
Inavyotakiwa interview unapika Soft skills ambazo huwezi kuziona kwenye vyeti na hizo ndio zinamtofautisha mwombaji mmoja wa kazi na mwingine ambao sifa za makaratasi hard skills zinafanana.
Mfano uwezo wa kupokes feedback
Uwezo wa kuwasiliana kwa usahihi
Uwezo wa kufanya kazi na wengine n.k
Hizo sifa huzikuti kwenye vyeti.
 
Kwaio daktari inatakiwa awe amefaulu tu ila ata kama ana tabia mbovu fresh au hana customer care, ubinadamu nk. Yeye apewe tu kazi au sio
Tabia mbovu kama zipi??
Ubinadamu unaupimaje kwenye hizo interview ?
Tanzania bado hatujafikia kiwango cha kuajiri madaktari katika hospitali za umma kwa sababu ya customer care.
 
Wahasibu na wanasheria mnasoma miaka mitatu ndio maana ni muhimu kukaguliwa kaguliwa sana tofauti na madaktari. Madaktari wanapewa leseni ku deal na maisha ya watu, nyie mnapata vyeti kucheza na makaratasi.
Ww andika upuuzi tuu ila usaili lazima ufanye mkuu πŸ˜‚
 
Kwenye udaktari suala muhimu ni ufaulu tu na leseni, haya mengine ya interview ni njia ya kupunguza watu kwa sababu ya ufinyu wa ajira.

Una wazimu wewe ,kwamba undergraduate wa MD anapewa hadhi ya Phd ?
Unaelewa unachoandika wewe ?
Hizi akili za waalimu typical kabisa , kumbe walimu wameshawaambukiza ukilaza ninyi manurse na madaktari
Mpwayungu ,njoo uchukue watu wako huku tafadhali πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Dah ! Aisee
Utumishi shikilieni hapo hapo ,maanina πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† yaani mmeshaanza kunena kwa lugha mapema hivi
Angalia msiokote Makopo sasa
 
Daktari hahitaji usahili, leseni yake ya MCT inatosha.
Wakili muhuri wake anaousotea Law School of Tanzania kwa mbinde naye aajiriwe bila interview kwakuwa ana leseni ya uwakili kutoka kwa Jaji Mkuu?

Mhasibu naye kwakuwa ana leseni kutoka NBAA naye aajiriwe pasipo interview?

Hivi what's so special kwa daktari? Hizo leseni zinazotolewa kwa mchongo ndiyo zimfanye mtu asipitie usaili?

Tena walitakiwa wapigwe oral,written pamoja na practical ili kupata wale competent hasa.
 
Ama kweli kumbe kuna watu ni empty Sana aisee , huko hospitalini na kwenye mashule sijui hizo huduma mtazitoa vipi kama analytical thinking na logic zenu ni poor kama hivi , aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…