Kumfanyisha Interview Medical Doctor aliyethibitishwa na Baraza la Madaktari (MCT) ni dharau kubwa sana

Kumfanyisha Interview Medical Doctor aliyethibitishwa na Baraza la Madaktari (MCT) ni dharau kubwa sana

====================

UPDATES

Kwa taarifa nilizozipokea ni kwamba vijana wameitwq huko Galanos sekondali wakafanyiwe interview ya makaratasi

Hii nchi inashangaza sana

Mbona hilo lilishafafanuliwa tangu siku nyingi
IMG-20240831-WA0001.jpg
 
Huwa kuna sheria daktari akimaliza chuo anaenda intern (hospitali yeyote ya rufaa ya mkoa au ya taifa) huko atakaa mwaka mzima siku 365 kila siku ataamkia wodini kutibu wagonjwa chini ya usimamizi wa dakyari bingwa

Akimaliza hapo anapimwa kwa pepa na kitabu maalum cha ripoti ya maendeleo yake kwenye kila idara aliyopita kwa vitendo kinakuwepo mfano kitengo cha mifupa marks 80 labour 60 n.k ikitokea kafeli atatakiwa kurudia kwa gharama zake

Akifaulu ndio anakidhi vigezo vya kupiga pepa la leseni akitoboa ndio anapata leseni

Sasa mtu kafanya yote hayo uje umuite shule ya gakanos huko umfanyie interview ya makaratasi ya kazi gani sasa?

Si afadhali hata ingekuwa practical labda umpe mgonjwa amtibu umpime kwa mtindo huo hapo inge make sense mkuu

Tatizo wengi humu hawaelewi mchakato ulivyo pia wana roho ya kwanini wale na sio huyu
Nani kwakwambia huko intern hakuna upendeleo na kupita kwa mchongo?

Hivi wewe unaishi Afrika ama ughaibuni? Kama mwanafunzi anaanza kununua paper tangu sekondari hadi chuo atashindwa kumnunua supervisor wake intern?

Hiyo michezo yote tunaijua mkuu labda kama umechelewa kuja mjini ndiyo utaona unachozungumza kina mashiko.

Wapo washkaji zetu mtaani ni empty kichwani lakini kwakuwa anatokea familia inayojiweza basi kila kitu kwake kinawezekana.

Acha wapitishwe kwenye tanuru la moto ili akaoneshe umahiri wake mbele ya kadamnasi ya watu asiowafahamu.
 
Interview lazima, nyie ndo mnafanya operation mnasahau mkasi kwenye tumbo. Juzi mtu kafariki kwa uzembe wa ma Doctor kufanya upasuji kizembe.
Interview lazima.
 
Sema in our next life, tusi sahau kuomba kuzaliwa kwenye familia zenye surname nzito.
Unamaanisha watoto/Wajukuu zetu? au una maanisha utazaliwa mara ya pili?[emoji23][emoji23][emoji23]

Kama ni watoto/wajukuu basi hilo lipo mikononi mwako, watengenezee jina/njia wasije kupitia magumu kama yalivyo sasa
 
Just imagine kijana kapata division one ya 7 au 10 form four kaenda high school kupiga PCB. Kapambana sana kachakaa kajitesa kajinyima kapata division one form six ya point tatu au tano.

Kaaply Muhimbili University kapitia mchujo katoboa akaanza masomo ya udaktari.

Kasoma miaka mitano bila kudisco tena kwa mateso makubwa bila kula bata mpaka kamaliza chuo.

Kabla hajaingia intern kafanyishwa mtihani wa MEDICAL COUNCIL OF TANGANYIKA katoboa kaanza interniship.

Kapiga intern kwa mwaka mmoja kisha kamaliza kisha kapigishwa pepa lingine la MCT katoboa.

Kasajiliwa na kutambulika kama MEDICAL DOCTOR na MCT.

Kijana huyu wa kitanzania aliyesoma kwa kujinyima na kujitesa tangu kidato cha kwanza leo hii anafanyishwa interview tena written interview sio prectical interview ili iweje?

Huyu kijana akikosa nafasi mnajua stress atakazopata mtaani na jamii inayomzunguka?

Hiyo michujo yote alopitia akipata ajira mnamlipa milioni moja na laki mbili ukitoa makato anabeba laki tisa bado mnampigisha interview ya nini sasa?

Hamuoni kama mnakatisha tamaa vijana waliopo shuleni na vyuoni?

Wadau

====================

UPDATES

Kwa taarifa nilizozipokea ni kwamba vijana wameitwq huko Galanos sekondali wakafanyiwe interview ya makaratasi

Hii nchi inashangaza sana
Interview ni muhimu na zaidi ni kupima uelewa wa jumla mfano nje ya nchi hata mtu akiitaji kusomea fani flani anapiga usaili kwanza . Hivyo tusione ajabu
 
Huko intern ndiyo wataelewa? Yaani mtu ashindwe ku master alichofundishwa miaka 5 aje kufanya hivyo kwenye intern ya mwaka mmoja?

Kusoma kwa kukariri ili tu afaulu mtihani ndiyo mtindo wa wanafunzi wengi wa kibongo badala ya kuelewa. Sasa mtu anayesoma kwa kukariri atakariri vingapi?
Acha ujuaji
 
Umesoma ukafaulu theoretically and practically ukawa awarded then unaogopa interview, how comes???
Labda ulalamikie aina ya maswali ikiwa hayakuwa relevance to your career.
Nawashauri mliyomaliza vyuo hamna ajira tumieni muda mwingi ku practice kwenye kozi zenu ili msisahau mkaogopa usaili.
 
Unamaanisha watoto/Wajukuu zetu? au una maanisha utazaliwa mara ya pili?[emoji23][emoji23][emoji23]

Kama ni watoto/wajukuu basi hilo lipo mikononi mwako, watengenezee jina/njia wasije kupitia magumu kama yalivyo sasa
Namaanisha Nita zaliwa Mara ya 2
 
U
Sasa kama wewe MD uko timamu kichwani na una leseni mara PhD haya inakuaje unaogopa usaili kama wewe sio kilaza umepata cheti kwa kusomea mitihani
Umeongea kwanza kwa kutoelewa yaani umesoma kujibu Ila sio kuelewa,mtu akavuka kote huko unamuita kilaza, mie sio daktari Ila najua mziki wake,elewa kwanza ni tz tu md haheshimiwi huko Kenya anakula 18M tzs monthly,huko Kanada wanakula zaidi ya 50M tzs.
Huwezi linganisha daktari na ujinga mwingine,
 
Eti Kenya analipwa 18TZS? Hahaha...

Kama hujui kitu kaa kimya hutodharauliwa.

Anyways hebu tuwekee evidence inayoonesha MD analipwa amount hii uliyoitaja mkuu tuwatafutie wadogo zetu michongo maana tuna ndugu zetu hapo Kenya.
 
U

Umeongea kwanza kwa kutoelewa yaani umesoma kujibu Ila sio kuelewa,mtu akavuka kote huko unamuita kilaza, mie sio daktari Ila najua mziki wake,elewa kwanza ni tz tu md haheshimiwi huko Kenya anakula 18M tzs monthly,huko Kanada wanakula zaidi ya 50M tzs.
Huwezi linganisha daktari na ujinga mwingine,
Basi kama TZ hawalipwi ivyo huoni kua ni ishara kwamba ni wakawaida tu hao.
 
Basi kama TZ hawalipwi ivyo huoni kua ni ishara kwamba ni wakawaida tu hao.
Africans value more politicians than professional,hivi huna aibu kusema kuwa madaktari ni WA kawaida kweli watu wanaoweza fanya operation mkeo akazaa salama na mtt akawa hai,
Wewe subiria ipo siku utajua value yao na hela zako hizo kiburi kitaisha
 
Back
Top Bottom