Kuna vitu maamuzi yake huhitaji Hoja, yaan anasimama MTU makini anaelezea Kwa hoja !.
Sasa kumfukuza MTU namna hii, maana yake ni kuifanya habari iwe kuuuuuubwa , embu fikiria vyombo habari vireport " CCM yamfukuza aliyepinga kuvunjwa Kwa Katiba wakati wa zoezi za kuchagua Mgombea Urais'.
Habari kama hii Inakua Kubwa, inaamsha Hisia hata za waliolala , wanatambua kumbe Kuna uvunjifu wa Katiba uliofanyika?. Nao wao wanataman kujua ,wanafatilia zaidi na zaidi !!.
Maamuzi ya Busara ilikua ni Ama Kumpuuza, yaan Asijibiwe , au kumjibu tu Kwa hoja ili kuendelea kutoa sababu za kuhalalisha uhalali wa maamuzi ya Dodoma.
Sasa njia fupi ,Kwa mawazo mafupi , imekua ni Kusitisha Waandishi wa habari na kumfukuza Kwa kosa la Usaliti.
Khaaa yaan MTU kuhoji, ndio Usaliti?.
Kweli Kenge hasikii mpaka Damu imtoke masikioni.