Kwani kukinzana mawazo imeshakuwa jinai? Maana miaka michache iliyopita wengi wenu walipigania uhuru wa mawazo. Watu waruhusiwe watoe mawazo yao. Mbona leo mmegeuka? Uhuru wa maoni ni pamoja na kukubali kusikia yale usiyopenda kusikia. Ni pamoja na wale wanaopinga chanjo kukubali kusikia wale wanaoikubali, na wale wanaoikubali kukubali kusikia wale wanaoipinga. Sio Jinai.
By the way wengi mnaopenda chanjo naona mtu akikataa mnasema mbona dawa so and so anatumia? Well ni maamuzi ya mtu. Kuna watu hawatumii dawa fulani na wanazipinga. Lakini zingine wanatumia. Bob Marley alikataa kukatwa mguu ili kuponya kansa. Lakini alikuwa anatumia Mic za wazungu na magitaa yao kuimba na kupiga muziki.
Kila mtu aachwe aseme anachokiamini. Nje ya hapo ni udikteta tu!