Kumi bora ya waandishi mahiri wa hadithi za Kiswahili

Kumi bora ya waandishi mahiri wa hadithi za Kiswahili

Ni kazi sana kupata kazi zao online, nimejaribu bila mafanikio.

Kuna Mama mmoja mtanzania kitabu chake kimetafsiriwa kwenye lugha kadhaa ikiwemo Kifaransa ila sio rahisi kukipata hicho kitabu online

Vitabu common kabisa kama Mabala the farmer, Hawa the bus driver ni ndoto kuvikuta mtandaoni. Watunzi na publishers wao wajiongeze watumie technology kusambaza kazi zao na kujiongezea kipato.
 
Yulenaliyetunga nyota ya rehema mbona hukumweka

Shigongo hata 100 bora haingiii

Sent using Jamii Forums mobile app
M S Mohamed. Ni mtunzi pia wa 'Kiu'
Alafu huyo mwingine ananakili, kutafsiri na kubadilisha riwaya za waandishi wa Marekani. Moja ya vitabu vyake ni tafsri ya riwaya iitwayo 'The Other Side of Midnight' ya Sidney Sheldon. This guy is a literary hack.
 
Mwandishi wa kitabu cha KIVULI KINAISHI mpe nafas ilo bora
 
...Hivi ile sijui ni riwaya ya VIPEPEO WEUSI nani Alikua mtunzi?, Samahani lakini!

Sorry mkuu nilianza kusoma comment kabla ya kuangalia ID, nilitaka kukubishia ila baada ya kuona ID nimeelewa kwamba una haki ya kuwa name him mtazamo.
 
Imefika wakati Serikali ya Tanzania na wachapaji wa vitabu wawe wanatoa tuzo mbalimbali kwa waandishi wa vitabu vya riwaya, tamthiliya na ushairi.

Ni aibu kuendelea kuchukulia poa vipaji vya waandishi.
 
Ujue mie labda nina mtazamo tofauti
1) Asilimia kubwa ya watu wa mwambao wanajua kiswahili fasaha na hivyo kuwafanya wawe wa kipekee unaposoma kazi zao, tafuta waandishi hata wadogo tu ambao hawajukikani kabisa ila ni watu wa mwambao utabaini wanajua sana na si kwenye Hadithi tu bali hata nyimbo, sikiliza maneno ya taarabu na tunzi zao utabaini kujua kwao kiswahili fasaha kunawabeba sana tofauti na sisi wa maeneo mengine kama ya kwa kina mkuu wetu
2) Kuna vipaji vingi sana mitaani tena hata hawana shule kichwani wala utaalamu wa maneno ila ni wazuri sana wa kutunga Hadithi, kitu pekee ninachokifahamu kwa Shigongo hana kipaji kiiiiile cha kutishia amani ila amekua mjanja kuwatumia vipaji vya chini na kuwaweka katika himaya yake kama alivyo Diamond Platinumz hivyo kufanya watu wamuone mkali, mfano Shaluwa ni mkali tu ila yupo chini yake
3) Namba kumi hapo nipo mimi maana nikiangalia kazi nilizoandika na ambazo watu wamezisoma nimepata feedback nzuri sana kama Zafeera, Kitanzi cha upendo, Paka Mweusi, Mshumaa gizani, Monica, Daraja la Misukule, Binti wa ng'ambo na vinginevyo vingi tu vinanifanya niwe balaa katika utunzi wa Hadithi ila ndio hivyo "tatizo nyota"

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijawahi ona kitabu chako hata kimoja tofautisha utunzi mahiri na kutunga vitabu vya biashara kazi zitaishia kapuni
 
Back
Top Bottom