Kumiliki gari ukiwa Tanzania sio jambo la mchezo... yataka moyo.

Kumiliki gari ukiwa Tanzania sio jambo la mchezo... yataka moyo.

Tanzania kichwa cha mwendawazimu alisema hayati
 
Ukishanunua gari unakutana na maandaki + mashimo barabarani

Ova
 
Mkuu gari used kutoka kwa mbongo si utauziwa skrepa
Unakua na fundi wako unayemuamini anaitazama kwanza, akikwambia iko vizuri chukua, akikwambia mbovu achana nayo, magari siku hizi yako mengi sana mjini huwezi kosa la kukufaa, ni kama nguo za mtumba.
 
Hili suala la kukatwa salio kwa ajiri ya kuangalia salio huwa siliewagi kabisa
Cha ajabu wabongo wapo kimyaaa!!! Kama una visa card kutoka nchi nyingine bank za bongo wanakukata kila unapotoa pesa 15,000 na nchi yako unakatwa ili usikatwe nenda KBC bank ya wakenya..kila kitu bongo kipo kukomoana tu..bora Zanziber Mungu ajaalie wajitenge kuepuka hii dhahama,na sisi Mafia tutajiunga Zanziber kina Mwigulu waingie na passport panda hawa.
 
Ndio mana wabongo gari ya 2007 wanaita New model sababu za miaka ya 2018 kuja juu kodi kichefuchefu
 
Unakua na fundi wako unayemuamini anaitazama kwanza, akikwambia iko vizuri chukua, akikwambia mbovu achana nayo, magari siku hizi yako mengi sana mjini huwezi kosa la kukufaa, ni kama nguo za mtumba.
Bongo nyoso ndugu yangu hata uyo fundi wako anaweza kula njama na anaekuuzia gari inategemea tu na nani atamwekea dau kubwa mezani
 
halafu kuna mpuuzi mmoja jana wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha magari kigamboni akamuomba mama aongeze kodi ya kuagiza gari nje ili watu wanunue ma howo kwenye kiwanda chao
 
Tanzania gari ni anasa, second hand bei iko juu, sasa jimix uchukue zero km ndo utapoteana kabisa hiyo kodi watakayokutajia TRA.
Hii nchi kuna kodi tunachangia zinaishia kwa watu ambao hawajali umuhimu wetu km wananchi wenzao. Wanachojua ni kutafuna cake ya taifa na maandazi yake
 
Ameongea maneno ya msingi wewe unafanya utani,hebu jaribu kufikiri tu kidodo Zambia hawana bandari na ushuru ni mdogo mno kuliko sisi kwanini tz imekaa kukomoana sana? na kufanya maisha yawe magumu kwa watu wake?? Hii leo ukiwa na Account crdb na kwengine kuangalia salio kwenye Internet banking unakatwa na mijitu ipo kimya hii ni nini??
Kwanini kila mara uchungulie salio.
 
Nchi ya hovyo,watu wa hovyo na hatujielewi ww watu watengeze gari kwa bei rahisi ili watu waweze kupata huduma ya usafiri.Unakuja kukutana na kodi kubwa kuliko bei ya gari unajiuliza hupati jibu na wala watu hatujali wala kulalamika
Inchi inaongozwa wa watu wenye roho mbaya, warafi na wasio na huruma kwa wananchi wao… ss wenye bahari/bandari ndo tunakod kubwa kuliko nchi zisinzo na hivyo vitu… acha tuendelee kuendesha ma Carina TI
 
Back
Top Bottom