Tanzanized S
Member
- May 3, 2024
- 12
- 19
Katika taifa linalojivunia kuwa la kidemokrasia, uhuru wa kujieleza na usawa mbele ya sheria ni nguzo kuu zinazopaswa kulindwa kwa nguvu zote.
Hata hivyo, hali halisi ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeanza kufifisha matumaini ya Watanzania wengi waliotamani kuona enzi mpya ya siasa zenye haki na usawa.
Kitendo cha kumkamata John Heche, mmoja wa viongozi wa CHADEMA, akiwa katika eneo la Kariakoo – eneo hilo hilo ambalo Chama cha Mapinduzi (CCM) limekuwa likifanya mikutano bila bugudha yoyote – ni ushahidi wa wazi wa uonevu na ubaguzi wa kisiasa unaoendelea kufanywa na serikali ya Samia.
Heche hakuvunja sheria yoyote.
Alikuwa akitekeleza haki yake ya msingi ya kukutana na kuzungumza na wananchi – haki inayolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kitendo cha polisi kumkamata bila sababu za msingi, huku wakiyafumbia macho matendo kama hayo hayo yanapofanywa na CCM, ni mfano wa wazi wa matumizi mabaya ya vyombo vya dola kwa faida binafsi za mtawala kisiasa.
Hili si tu tishio kwa upinzani, bali pia kwa mustakabali wa demokrasia ya nchi yetu.
Rais Samia amekuwa akijitambulisha kimataifa kama kiongozi anayefungua ukurasa mpya wa kisiasa Tanzania, lakini kwa matendo yake kauli zote nzuri alizowahi kuzitoa kuhusu mageuzi hazina maana tena.
R nne ni UTAPELI 🚮
Hawezi kujinasua katika lawama hizi, kwani vyombo vya dola viko chini ya mamlaka yake.
Kukamatwa kwa Heche si tukio la bahati mbaya; ni ishara ya uendelezaji wa mfumo wa kiimla unaotumia hofu, vitisho na ukandamizaji wa haki za msingi za kisiasa.
Kwa nini CCM iruhusiwe kufanya mikutano Kariakoo bila pingamizi lolote kutoka kwa polisi, lakini CHADEMA ikikanyaga eneo hilo ni kosa?
Huu ni ubaguzi wa wazi wa kisiasa, na ni doa kwa utawala wowote unaojinadi kuwa wa haki.
Kama Samia hawezi kusimamia usawa na kutenda haki kwa vyama vyote vya siasa, basi ameshindwa wajibu wake mkuu kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa nchi hapaswi hata kuvumilia kuona watu katika taifa analoliongoza kuonewa kisa tu Wana mtazamo tofauti
Sasa huyu mama ameenda mbali zaidi
Si tu kwamba atazama uonevu ukifanyika bila kuchukua hatua zozote, yeye ameamua kushiriki moja kwa moja katika kuwafanyia watu uonevu
Kwa hali hii hafai kabisa kuliongoza taifa hili, atafute kazi nyingine ya kufanya, Uongozi tayari umemshinda!
Tanzania inahitaji kiongozi anayesimamia haki kwa wote, si anayependelea upande mmoja (upande wake) na kuwaonea na kuwadhalilisha wengine.