NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Njia nzuri ya kumlinda mtoto ni kumkomaza ajue kukabiliana na maisha pale atapoanza kujitegemea ama ukitoweka kwa kifo na ulinzi wako kwake ukawa haupo tena.
Sina maana ya kusema mtoto umlee maisha magumu tu, NO! Njia sahihi ni kumlea kivugu vugu, raha azijue na shida nazo ajue namna ya kukabiliana nazo (sio kuzijua tu bila kujua namna ya kuzitatua)
aina hii ya wazazi over protective huwa wana nia ya kuwalinda Watoto wao lakini aina hii ya malezi haiwafai watoto wao katika uhalisia wa dunia hii hasa ukizingatia watoto nao wakiwa wakubwa watajitegemea,
Wazazi wa aina hii mara nyingi humuanda mtoto aje kuwa aina mtu wasiemtaka ama kuja kuwa katika hali wasiyoitaka.
Mzazi hataki mtoto wake apitie shida alizopitia, anaanza kumpa pesa na kila anachohitaji, mtoto hajui hata hio fedha na vitu namna gani vinavyopatikana, yeye anajua kupewa tu, mzazi akitoweka ama mtoto akianza Maisha ya kujitegemea bila back up anaweza kurudi kuishi maisha ya chini maana hajui fedha alizopewa jinsi zinavyotafutwa kwa jasho.
Mzazi hataki mtoto awe mchafu, house girl anamfulia nguo na kumfanyia kila shughuli ya usafi mtoto, matokeo yake mtoto hawezi kujifanyia usafi, akianza maisha ya kujitegemea bila house girl anakuwa mchafu.
Mzazi anamfungia ndani mtoto wake geti kali, yani ile mtoto kuleta rafiki zake wacheze nae kwake hataki, mtoto kwenda kucheza kwa jirani nyumba ya pili ama tatu chini ya uangalizi hataki, mtoto anakosa kujifunza mbinu za kuishi na jamii independently na matokeo yake anaweza kuwa mtu wa kupenda kuishi kivyake akaona ni kawaida, mtoto anaweza kuonewa kirahisi sana akiwa kivyake bila mzazi, n.k.
Bruce Lee aliwahi kusema "usiombee kuja kuishi maisha mepesi, Omba upewe uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha".
Hatujui kesho yetu tunaweza kuanguka na ikawa hatari kwa watoto wetu, Tujaribu angalau kuwalea watoto wetu kulingana na maisha ya kiuhalisia watayokutana nayo pindi tukiwa hatupo ama nao wakianza maisha yao ya kujitegemea.