Kumlipa Clinical Officer laki 6 sio haki hata kidogo

Sina mood

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2018
Posts
248
Reaction score
1,442
Clinical officers wanafanya kazi kubwa sana kunusuru Maisha ya watu, kumlipa laki 6 ambayo ni sawa na Tsh elfu 20 kwa siku tena hapo bado makato sio haki hata kidogo.

Tukianza na sekondari, huyu alilipa ada kubwa tofauti na wanafunzi wengine wanaosoma michepuo ya biashara na sanaa.

Pia asilimia kubwa ya Clinical Officers wa sasa walipita ngazi ya advance na walilipa ada kubwa mno tofauti na michepuo mingine mf PCM, HKL, HGE, ECA nk.

Hata Kwenda field tu analipia wakati fani zingine field hulipii Bali wewe ndiye unalipwa.

Serikali wajitahidi kumuongezea Hela Clinical Officer angalau laki 8 kwa mwezi.
 
Rudi chuo kasome uwe daktari (MD).
 
Unaweza pendekeza CO alipwe pesa ngapi? Pia hatulipwi kutokana na ada tulizolipa chuo ,ndo maana unaweza kuta kijana kasoma account yupo TRA mshahara wake mkubwa kuliko wa CO aliyelipa ada unayoita nyingi .

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Angalau laki 8 maana kazi wanazozifanya ni kubwa mno
 
Hao hao form 4 failures waliopata div.3 na 4 ndio unataka walipwe zaidi?

Si haki kabisa kuwapeleka watu wenye ufaulu mdogo kushughulika na usalama wa Afya zetu.Serikali komesheni huu upuuzi.
 
Umetukosea heshima watu wa PCM takers... Tunaamuru toa mara moja kwenye huo mfano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…