GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
- Thread starter
- #21
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rufaa imeishia wapi mwagito? Naona ya ndani mwako yamekushinda sasa umehamia kwa mabingwa...mchecheto huo!Huyu Mhindi sijui kawashika wapi patamu Wana Yanga manake si kwa kumng'ang'ania hivi. Mbona Mzee Akilimali hawamnyenyekei hivi?
Rufaa imeishia wapi mwagito? Naona ya ndani mwako yamekushinda sasa umehamia kwa mabingwa...mchecheto huo!
Mpaka siku ifikie hizi timu za bongo ziwe kampuni ndio tutaona soka lenye malengo. Sasa hivi klabu zinaendeshwa na wafia tumbo. Subiri msimu ujao uone mauzauza Jangwani, maana mwenye kauli katoka.Viongozi wetu wameshatufanya sisi Malofa sasa subiria Kesho tusichukuwe Ubingwa wa ASFC ( FA ) ndipo watatutambua.
Mpaka siku ifikie hizi timu za bongo ziwe kampuni ndio tutaona soka lenye malengo. Sasa hivi klabu zinaendeshwa na wafia tumbo. Subiri msimu ujao uone mauzauza Jangwani, maana mwenye kauli katoka.
Ngozi nyeusi hatuwezi kutawala,aliyeweza ni Kimei tuu wa CRDB.Subiri ataingia mmatumbi mwenzetu utasikia migogoro kila kukichaKila nikisikia Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Mehboob Manji akisema anajiuzuru Yanga huwa nawashangaa mno Wana Yanga wanavyoanza kupepesuka huku wakitaka kumlamba hadi Miguu na kumnyenyekea.
Sidhani kama hasa kwa Wanaume waliokamilika kabisa ( namaanisha rijali ) kila mara kumbembeleza Mwanaume mmoja tu ambaye ni Tajiri ili abakie au awe nao ni jambo jema na kwa sisi Wakazi wa Pwani Kitendo hiki cha Wana Yanga wanachokifanya kwa Manji kinaleta taswira mbaya mno ambayo siyo ya Kiume.
Hapa ndipo ninapoikumbuka Kauli ya Manji ambayo aliitoa katika moja ya Mikutano yake na Yanga pale Police Officers Mess aliposema namnukuu " Jamani wana Yanga wenzangu hebu tujipangeni kwa maslahi mapana ya Yanga kwani leo Mimi Yusuph naweza kuwepo na Kesho nisiwepo hivyo msiishi kwa kumtegemea tu Mtu mmoja bali tujitahidi ili Yanga yetu iweze kuwa na Wadhamini wengi na vyanzo vya kutosha vya mapato " mwisho wa Kumnukuu.
Mtu hawataki nyie mnamng'ang'ania wa nini? Hizi njaa za dhiki zitawapelekeni wapi? Hivi Yanga haiwezi kuendelea bila uwepo wa Manji? Bado nasisitiza kusema kuwa kwa Watu wa Pwani ni jambo baya mno ukiona Wanaume wanaojielewa kabisa huku wakijinadi wao ni Vidume / Rijali wakiwa wanajikomba na kujipendekeza kwa Mwanaume Rijali Mkuu mmoja.
Mmeiabisha mno Klabu ya Yanga!