Kumpatia Majaliwa ajira Zimamoto, kumpelekeka Bungeni na kumpatia mil 5 sio suluhu ya matatizo ya taifa letu

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Tuna changamoto lukuki kama taifa ambazo zinatakiwa kupatiwa suluhu na serikali kupitia vyombo vya dola na wala sio porojo za kisiasa.

Tuna majambazi, panya road na vibaka. Wanasumbua kwa zaidi ya miaka ishirini. Hapa napo tusaidiwe na akina majaliwa?

Tuna wahamiaji haramu kibao wanaishi na kufanya kazi hapa nchini. Warundi, wakenya, waganda n.k. Mbona hatujapata Majaliwa wa kuwadhibiti?

Kila kukicha pesa za umma zinatafunwa halmashauri kama njugu. Mbona hajapatikana Majaliwa wa kudhibiti?

Kupiga porojo za Majaliwa hadi Bungeni kisa tu taifa letu halina uwezo wa kuokoa raia wake ni upuuzi ambao hautasiaidia taifa leti huko mbele.
 
Mkuu, ajali ya ndege ya Precision Air ambayo ililazimika kutua kwa dharura katika ziwa Victoria, iliambatana na changamoto kubwa ya ukoaji wa abiria waliokuwa ndani yale. Hii inatokana na vifaa duni vilivyokuwepo katika eneo husika.

Hakukuwa na namna zaidi ya wavuvi waliokuwapo kutoa msaada wa uokoaji. Ushujaa wa bwana mdogo Majaliwa ndipo hapo ulipothibitika.

Kile kitemdo cha uthubutu na ushujaa wake wa kupiga mbizi na kwenda kuvunja mlango wa ndege, hali iliyopelekea zaidi ya abiria 20 kuokolewa ni kitu kinachostahili pongezi na kuthaminiwa kitaifa.

Mbona tunaona katika picha uwepo wa askari katika eneo husika, na ambao walishindwa kufanya kitendo kama chake, ama kuthubutu kwenda kuungana naye katika zoezi la uokoaji majini!?

Suala la uwepo wa athari katika jamii kutokana na matendo ya vibaka, majambazi, udangaji, matumizi ya madawa ya kulevya na uhalifu wa aina yoyote ile, si ya dharura. Hilo ni jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama. Ukiyaona yanatamalaki basi tambua vyombo husika haviwajibiki ipasavyo, ama la, navyo ni sehemu ya wanufaika wakuu wa matendo hayo ya kiovu.
 
Nchi haiwezi kumaliza matatizo kwa kutumia sera mbovu za Ujamaa.
 
Bunge limedorora halina mvuto hakuna anayeangalia wala kusikiliza wamemuita dogo ili kulipa Bunge uhai kidogo
 
Nauliza wale wenzie watatu waliozamia nae mbona hawasikiki?

Kwenye Maelezo ya bwana Majaliwa anasema walikua wanne
 
Mkuu, ajali ya ndege ya Precision Air ambayo ililazimika kutua kwa dharura katika ziwa Victoria, iliambatana na changamoto kubwa ya ukoaji wa abiria waliokuwa ndani yale. Hii inatokana na vifaa duni vilivyokuwepo katika eneo husika.

Hakukuwa na namna zaidi ya wavuvi waliokuwapo kutoa msaada wa uokoaji. Ushujaa wa bwana mdogo Majaliwa ndipo hapo ulipo thibitika.

Kile kitemdo cha uthubutu na ushujaa wake wa kupiga mbizi na kwenda kuvunja mlango wa ndege, hali iliyopelekea zaidi ya abiria 20 kuokolewa ni kitu kinachostahili pongezi na kuthaminiwa kitaifa.

Mbona tunaona katika picha uwepo wa askari katika eneo husika, na ambao walishindwa kufanya kitendo kama chake, ama kuthubutu kwenda kuungana naye katika zoezi la uokoaji majini!?

Suala la uwepo wa athari katika jamii kutokana na matendo ya vibaka, majambazi, udangaji, matumizi ya madawa ya kulevya na uhalifu wa aina yoyote ile, si ya dharura. Hilo ni jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama. Ukiyaona yanatamalaki basi tambua vyombo husika haviwajibiki ipasavyo, ama la, navyo ni sehemu ya wanufaika wakuu wa matendo hayo ya kiovu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli kijana anastahili pongezi, pamoja na wengine walioshiriki kuokoa wahanga wa tukio lile.

Hata hivyo, namna ambayo pongezi na maelezo yanayotolewa kuhusu huyu Majaliwa ndiyo yanayofanya watu wenye akili za kawaida wawe na changamoto za fikra.

Kwanza kabisa kwa uzoefu na akili ya kawaida, mlango wa ndege haufunguliwi na mtu akiwa nje na hata kuvunja kwa nje ili ufunguke siyo rahisi (hadithi ya Majaliwa kufungua mlango kwa kasia siyo kweli).

Pili mashujaa waliojitokeza pale kuokoa ni zaidi ya huyo mmoja, kwa nini wakimbizane na huyo tu, au wahusika wote serikalini hawawezi kulitambua hili? Tunatakiwa kufikiria kwa mapana zaidi.

Tatu, ukiwasikiliza abiria waliokuwa ndani ya ndege, maelezo yao (ambayo kwa akili ya kawaida ndiyo sahihi/kweli zaidi), unaweza kushangaa mtiririko wa matukio yote hadi kupelekwa bungeni kwa Majaliwa.

Nne, kumpatia mfunzo na ajira kijana Majaliwa (kama atapenda), ni jambo jema na wale wavuvi wote walioshiriki wangepatiwa mafunzo pia ili wayatumie kwenye shughuli zao za kila siku
 
Kwani kapelekwa bungeni kama suluhu ya maisha ya mtanzania!?

Mimi nadhani majaliwa anastahili anavyofanyiwa na zaidi kwa kile alichofanya. Kijana jasiri, mwenye upendo na hamasa kwa jamii
 
Mkuu, ajali ya ndege ya Precision Air ambayo ililazimika kutua kwa dharura katika ziwa Victoria, iliambatana na changamoto kubwa ya ukoaji wa abiria waliokuwa ndani yale. Hii inatokana na vifaa duni vilivyokuwepo katika eneo husika.

Hakukuwa na namna zaidi ya wavuvi waliokuwapo kutoa msaada wa uokoaji. Ushujaa wa bwana mdogo Majaliwa ndipo hapo ulipo thibitika.

Kile kitemdo cha uthubutu na ushujaa wake wa kupiga mbizi na kwenda kuvunja mlango wa ndege, hali iliyopelekea zaidi ya abiria 20 kuokolewa ni kitu kinachostahili pongezi na kuthaminiwa kitaifa.

Mbona tunaona katika picha uwepo wa askari katika eneo husika, na ambao walishindwa kufanya kitendo kama chake, ama kuthubutu kwenda kuungana naye katika zoezi la uokoaji majini!?

Suala la uwepo wa athari katika jamii kutokana na matendo ya vibaka, majambazi, udangaji, matumizi ya madawa ya kulevya na uhalifu wa aina yoyote ile, si ya dharura. Hilo ni jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama. Ukiyaona yanatamalaki basi tambua vyombo husika haviwajibiki ipasavyo, ama la, navyo ni sehemu ya wanufaika wakuu wa matendo hayo ya kiovu.
Jukumu la kuokoa sio la zima koto? Polisi marine n.k?
 
Kwani kapelekwa bungeni kama suluhu ya maisha ya mtanzania!?

Mimi nadhani majaliwa anastahili anavyofanyiwa na zaidi kwa kile alichofanya. Kijana jasiri, mwenye upendo na hamasa kwa jamii
Kampe papuchi sasa
 
Kampe papuchi sasa

Yaani wewe Kwako pupuchi ndio kila kitu🤔 Ukiachilia mbali hicho kiungo ulishajiuliza uliletwa duniani kuja kufanya nini😆😆😆

Shtuka ndugu, hakuna anayekumbukwaga kwenye historia ya familia, ukoo, taifa wala dunia kwa kuchakata pupuchi😂😂😂
 
Labda haukojoi ukipigwa hukojoi
 
Hii yote ni kuficha aibu na fedheha. Jamii Itasahau, tutaenda ukurasa mwingine.
Mjumbe: what are you saying? Wamekufa Watanzania, that are dead, watu 19. Wewe unataka tumehuru itazia pilot asione gizani? Huna huruma?
 
Kuna mwingine atakuwa anajiandaa kufumania box la kura uchaguzi ujao ili atobolee TAKuKuru
 
Acha wivu, mwenzetu kapata bahati na Neema kwa njia hiyo, sasa ya nini umtolee mfano? Majaliwa amajaliwa itoshe tu kusema bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi
Akili za namna hii ndio utegemee nchi kuendelea.
 
Back
Top Bottom