Mkuu, ajali ya ndege ya Precision Air ambayo ililazimika kutua kwa dharura katika ziwa Victoria, iliambatana na changamoto kubwa ya ukoaji wa abiria waliokuwa ndani yale. Hii inatokana na vifaa duni vilivyokuwepo katika eneo husika.
Hakukuwa na namna zaidi ya wavuvi waliokuwapo kutoa msaada wa uokoaji. Ushujaa wa bwana mdogo Majaliwa ndipo hapo ulipothibitika.
Kile kitemdo cha uthubutu na ushujaa wake wa kupiga mbizi na kwenda kuvunja mlango wa ndege, hali iliyopelekea zaidi ya abiria 20 kuokolewa ni kitu kinachostahili pongezi na kuthaminiwa kitaifa.
Mbona tunaona katika picha uwepo wa askari katika eneo husika, na ambao walishindwa kufanya kitendo kama chake, ama kuthubutu kwenda kuungana naye katika zoezi la uokoaji majini!?
Suala la uwepo wa athari katika jamii kutokana na matendo ya vibaka, majambazi, udangaji, matumizi ya madawa ya kulevya na uhalifu wa aina yoyote ile, si ya dharura. Hilo ni jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama. Ukiyaona yanatamalaki basi tambua vyombo husika haviwajibiki ipasavyo, ama la, navyo ni sehemu ya wanufaika wakuu wa matendo hayo ya kiovu.