Mtoa mada fungua akili yako mkuu. Mwanao haendi shule kusoma tu. Kuna exposure na watu tofauti na mambo tofauti.
Nilibahatika kusoma shule ya Feza O - level na A- level. Kiukweli nilivyoexperience pale vimenishape na kunisaidia katika mafanikio hadi leo hii.
Tulijengwa kwa spirit ya brotherhood na kusaidiana. Tulipewa fursa nyingi za kuwa bora zaidi mara kwa mara. Shule ilikuwa haiishi competition za mambo ya kompyuta, music, lugha ya kituruki, hesabu na mengine mengi. Na ulikuwa ukichaguliwa mnapewa free trip kwenda nje kwa ajili ya hiyo competition. Hata kama haushindi but kwa kuparticipate tu unakuwa unajijenga katika sekta flani na motivation zipo kila siku. Nakumbuka kuna dogo alikuwa anapiga gitaa flani la kituruki vizuri akawa anapiga safari Uturuki kila mwaka na alikuwa analipwa. By estimation mpaka anamaliza form 6 alikuwa ashalipwa yeye kama yeye zaidi ya 10m bila kuhesabu trip ambazo ni free.
Ukiachana na the fact kuwa tulisoma na watoto wa who is who pale ambapo unajenga fursa ya kuonana na wazee wao na kujenga urafiki wa baadae, bado hata after kugraduate unapata msaada. Ishu za kazi, biashara, na kujuliana hali ni nyingi sana kiasi cha kwamba graduates wa Feza hawahangaiki katika kazi kwa sababu ukiinform alumni na una vyeti vyako unapata connection chap. Can you imagine kuna ofisi ya alumni ambayo ina kila kitu na kama wewe ni alumni wa Feza unaweza kwenda hapo na kuitumia kama workspace yako bila charges zozote kwa muda wowote utakao? Totally free. Scholarship opportunities ndio usiseme.
Pia mahusiano ya uongozi na wanafunzi ni smooth sana. Walimu ni washkaji na ni approachable. Wanakujenga kama sibling ili ufanikiwe mbeleni. Hata baada ya kugraduate mambo ni mazuri sana.
Personal stori moja ni nilishawahi kupewa dili la 16 mil na mwalimu pale shule katika mwaka wangu wa kwanza wa chuo. Imagine 19 years old unaaminiwa na 16 mil. Kibongobongo ni ngumu sana ila mwalimu akanipa pande na hakutaka chochote.
Tafadhali sana kama una uwezo usichezee elimu ya mwanao. Shule si kwa ajili ya madaftari ila kunamshape yeye kama yeye na network yake kwa maisha yake yote.