Mayunga234
JF-Expert Member
- Feb 17, 2017
- 1,725
- 1,995
- Thread starter
-
- #61
Kuna watu wanashindwa kukuelewa mkuu, Yaani mtu anayeingiza labda milioni 20 kwa mwezi anampeleka mtoto shule ya million 5 kwa mwaka kwake anaona amempeleka shule ya gharama ndo maana wanaropoka tu, ila wanatakiwa kuelewa mlengwa wa maada ni nani? Kwa ufafanuzi ni yule mzazi ambaye anapambana anateseka yaani anakaa njaa kabisa et anasomesha mtoto private then huyo mtoto akimaliza chuo aje akae nyumbani ateseke, kumbe bora angempeleka shule za kawaida tu akapata elimu aje mtaani kupambana na changamoto za maisha au kama mzazi amejaliwa basi yale mapambano ya kusomesha shule za gharama angepambana kumuandalia mtoto cha kuanzia pindi atakapomaliza elimu yake,
umepanic kama ndugu yako mwendazake, huu ukanda wenu una shida sana.
Wakuu kuna shule moja inaitwa St Joseph ipo maeneo ya Mbezi nasikia na yenyewe inafundisha hatari na ina malezi mazuri kwa wanafunzi, hata mwanafunzi awe mtukutu vipi akienda pale siku akirudi nyumbani unaweza kumkataa kwa kudhani labda umebadilishiwa mtoto. Nani anaifahamu vizuri shule hii wandugu? Nataka nimpeleke dogo akapige interview pale.
fees za january zinaleta stress sana..
Asante kwa kunipa moyo mkuu. Shule ipo Mbezi ipi mkuu? Mbezi Beach au Mbezi ya barabara ya Morogoro?Mpeleke nilishawai kusikia
Una mawazo kama yangu.
Mi sipeleki mtoto shule binafsi.
Nitamkazania hukuhuku shule za serikali atafaulu vizuri tu.
Unampeleka shule ya 5M anafika hadi chuo ushatumia gharama kibao then akimaliza anashinda nyumban
Kwa sasa bora hiyo hela ya ada Uwekeze kwenye vitu vya maendeleo hata akija kumalza ana sehem ya kujishikiza
poverty mentality at its core. akili za watu mafukara.Kumpeleka Mtoto shule yenye Ada kubwa au Shule ya Garama ni kupoteza tu hela, cz mtoto atasoma atafika hadi Chuo then atamaliza Vizuri chuo, baada ya kumaliza chuo anakuwa mzigo wako tena anashinda tu nyumbani hana cha kufanya Ajira hamna unaanza kuangaika upya, Wakati Umetumia gharama nyingi hadi kumfikisha Chuo
çok güzel👍Mtoa mada fungua akili yako mkuu. Mwanao haendi shule kusoma tu. Kuna exposure na watu tofauti na mambo tofauti.
Nilibahatika kusoma shule ya Feza O - level na A- level. Kiukweli nilivyoexperience pale vimenishape na kunisaidia katika mafanikio hadi leo hii.
Tulijengwa kwa spirit ya brotherhood na kusaidiana. Tulipewa fursa nyingi za kuwa bora zaidi mara kwa mara. Shule ilikuwa haiishi competition za mambo ya kompyuta, music, lugha ya kituruki, hesabu na mengine mengi. Na ulikuwa ukichaguliwa mnapewa free trip kwenda nje kwa ajili ya hiyo competition. Hata kama haushindi but kwa kuparticipate tu unakuwa unajijenga katika sekta flani na motivation zipo kila siku. Nakumbuka kuna dogo alikuwa anapiga gitaa flani la kituruki vizuri akawa anapiga safari Uturuki kila mwaka na alikuwa analipwa. By estimation mpaka anamaliza form 6 alikuwa ashalipwa yeye kama yeye zaidi ya 10m bila kuhesabu trip ambazo ni free.
Ukiachana na the fact kuwa tulisoma na watoto wa who is who pale ambapo unajenga fursa ya kuonana na wazee wao na kujenga urafiki wa baadae, bado hata after kugraduate unapata msaada. Ishu za kazi, biashara, na kujuliana hali ni nyingi sana kiasi cha kwamba graduates wa Feza hawahangaiki katika kazi kwa sababu ukiinform alumni na una vyeti vyako unapata connection chap. Can you imagine kuna ofisi ya alumni ambayo ina kila kitu na kama wewe ni alumni wa Feza unaweza kwenda hapo na kuitumia kama workspace yako bila charges zozote kwa muda wowote utakao? Totally free. Scholarship opportunities ndio usiseme.
Pia mahusiano ya uongozi na wanafunzi ni smooth sana. Walimu ni washkaji na ni approachable. Wanakujenga kama sibling ili ufanikiwe mbeleni. Hata baada ya kugraduate mambo ni mazuri sana.
Personal stori moja ni nilishawahi kupewa dili la 16 mil na mwalimu pale shule katika mwaka wangu wa kwanza wa chuo. Imagine 19 years old unaaminiwa na 16 mil. Kibongobongo ni ngumu sana ila mwalimu akanipa pande na hakutaka chochote.
Tafadhali sana kama una uwezo usichezee elimu ya mwanao. Shule si kwa ajili ya madaftari ila kunamshape yeye kama yeye na network yake kwa maisha yake yote.
umepanic kama ndugu yako mwendazake, huu ukanda wenu una shida sana.
Kipaumbele changu ni mwanangu/wanangu waishi maisha bora kuanzia elimu na makazi km hela ninayo nitamsomesha shule ya gharama yoyote na hata akikaa nyumbani nitamuhudumia mpaka atakapo pata maisha yake
Unadomesha mtoto shule ya madarasa ya tozo hakuna ada
Hata uniform mpya unakuwa mgumu kununua halafu unajisifu unasomesha [emoji1787][emoji1787]
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Uwezo unao lakini wa kupeleka IST - mil 74 kwa mwaka? Mi sina uwezo. Ningekuwa nao, ningewapeleka.
Then ndo hawa wanaishia kuwa Mashoga na walevi
Gubu la umasikini litakuua... Umejaa hasira na matajiri kama Magufuli!!