nnunu
JF-Expert Member
- Mar 4, 2011
- 654
- 230
Pole sana Belinda! Kitu pekee tunachowezza kufanya ni kukupa moyo na kukufariji. Umefanya vizuri kulileta swala hili hapa kwani moja katika mbinu za kuponya ni kulizungumza hili na marafiki na jamaa zako. Kwa upande wangu, ninaungana na wale waliosema kwa namna moja au nyengine "Hata jambo baya lina uzuri wake", nikimaanisha kuwa "hukuwa unastahiki kuishi na mtu asiyejali kama huyo". Ni vyema kuwa hili limetokea mapema; Mungu kakuepusha na majanga mengi. Fikiria angekuja kukusaliti baada ya kufunga naye ndoa!, maumivu yake yangekuwa makali zaidi.
Baada ya kuondokewa, utapitia katika hatua hizi nne:
1. Kutoamini na kutokubali kilichotokea lakini ndio ukweli.
2. Kwa kuwa ndio ukweli, hili litakuuma sana,
3. Maumivu yataambatana na huzuni.
4. Mwisho utakubali matokeo na ukweli wa mambo. Ni maji yaliyomwagika.
Kwa ushauri jinsi ya "kukusanya vipande vya moyo uliovunjika", fanya baadhi katika haya:
- Kila unapowaza kuwa "Ninampenda na siwezi kuishi bila yeye", utakuwa unakumbuka mazuri tu uliyoyapata na mliyogawana kabla ya mambo kuharibika. Lakini kama unavyokiri kuwa "mlikuwa na matatizo yenu madogomadogo", ukweli ni kuwa hayakuwa madogo kama ulivyokuwa unafikiria. Yalikuwa makubwa lakini ukavumilia kwa sababu ulikuwa unapenda. Sasa ni wakati wa kuyafikiria haya kwa lengo la kukutoa katika mawazo ya kuwa kulikuwa na mazuri tu. Hii itakusaidia umuone kwa jicho jengine.
- Kimbilio lako la mwanzo iwe paketi za tisues - lia kadiri uwezavyo. Jifungie chumbani kwa muda unaotaka, hata masaa 24 mfululizo, lakini ukitoka hapo, jufute machozi na kumbuka "Maisha yanaendelea". Kama ulivyokwisha shauriwa kabla, kimbilio lako la pili iwe marafiki, wazazi, ndugu au jamaa wa karibu. Hakuna tiba nzuri kama kupata bega la kulilia, hasa likiwa la mama, dada, au rafiki. Pamoja nao au peke yako, tembea/tembeeni sehemu za wazi. Epuka vilabu kwa kipindi hiki.
- Kama una uwezo, tafuta mnyama wa nyumbani, hasa mbwa au paka. Huyu atakupa mapenzi yote bila kukudai saaaana zaidi ya mlo wake na kumjali.
- Jiunge na kozi, masomo au amali ambayo daima ulikuwa unahamu uifanye. Muda wako mwingi utakuwa unashughulika na hili badala ya kukaa kumfikiria au kusubiri miujiza...AMESHAOA,hakufai, hakustahiki.
- Fanya kazi za kujitolea kama vile kuwahudumia wazee, watoto na makundi hitaji.
KANUNI YA DHAHABU: KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUUGUZA, USIMSOGELEE; USIMTAFUTE; USIMRUHUSU KUTAFUTA FARAHA NA WEWE NA KUMWACHA AKUMWAGIE UONGO
Naunga mkono hoja 100%......
muda mrefu sikupata bahati ya kusoma comments zako,
Nahisi majukumu mengine yalikuzidi,
karibu once again....lol