Kumpoteza mtu unayempenda!!

Kumpoteza mtu unayempenda!!

Pole sana Belinda! Kitu pekee tunachowezza kufanya ni kukupa moyo na kukufariji. Umefanya vizuri kulileta swala hili hapa kwani moja katika mbinu za kuponya ni kulizungumza hili na marafiki na jamaa zako. Kwa upande wangu, ninaungana na wale waliosema kwa namna moja au nyengine "Hata jambo baya lina uzuri wake", nikimaanisha kuwa "hukuwa unastahiki kuishi na mtu asiyejali kama huyo". Ni vyema kuwa hili limetokea mapema; Mungu kakuepusha na majanga mengi. Fikiria angekuja kukusaliti baada ya kufunga naye ndoa!, maumivu yake yangekuwa makali zaidi.

Baada ya kuondokewa, utapitia katika hatua hizi nne:
1. Kutoamini na kutokubali kilichotokea lakini ndio ukweli.
2. Kwa kuwa ndio ukweli, hili litakuuma sana,
3. Maumivu yataambatana na huzuni.
4. Mwisho utakubali matokeo na ukweli wa mambo. Ni maji yaliyomwagika.

Kwa ushauri jinsi ya "kukusanya vipande vya moyo uliovunjika", fanya baadhi katika haya:
- Kila unapowaza kuwa "Ninampenda na siwezi kuishi bila yeye", utakuwa unakumbuka mazuri tu uliyoyapata na mliyogawana kabla ya mambo kuharibika. Lakini kama unavyokiri kuwa "mlikuwa na matatizo yenu madogomadogo", ukweli ni kuwa hayakuwa madogo kama ulivyokuwa unafikiria. Yalikuwa makubwa lakini ukavumilia kwa sababu ulikuwa unapenda. Sasa ni wakati wa kuyafikiria haya kwa lengo la kukutoa katika mawazo ya kuwa kulikuwa na mazuri tu. Hii itakusaidia umuone kwa jicho jengine.

- Kimbilio lako la mwanzo iwe paketi za tisues - lia kadiri uwezavyo. Jifungie chumbani kwa muda unaotaka, hata masaa 24 mfululizo, lakini ukitoka hapo, jufute machozi na kumbuka "Maisha yanaendelea". Kama ulivyokwisha shauriwa kabla, kimbilio lako la pili iwe marafiki, wazazi, ndugu au jamaa wa karibu. Hakuna tiba nzuri kama kupata bega la kulilia, hasa likiwa la mama, dada, au rafiki. Pamoja nao au peke yako, tembea/tembeeni sehemu za wazi. Epuka vilabu kwa kipindi hiki.

- Kama una uwezo, tafuta mnyama wa nyumbani, hasa mbwa au paka. Huyu atakupa mapenzi yote bila kukudai saaaana zaidi ya mlo wake na kumjali.

- Jiunge na kozi, masomo au amali ambayo daima ulikuwa unahamu uifanye. Muda wako mwingi utakuwa unashughulika na hili badala ya kukaa kumfikiria au kusubiri miujiza...AMESHAOA,hakufai, hakustahiki.

- Fanya kazi za kujitolea kama vile kuwahudumia wazee, watoto na makundi hitaji.



KANUNI YA DHAHABU: KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUUGUZA, USIMSOGELEE; USIMTAFUTE; USIMRUHUSU KUTAFUTA FARAHA NA WEWE NA KUMWACHA AKUMWAGIE UONGO

Naunga mkono hoja 100%......
muda mrefu sikupata bahati ya kusoma comments zako,
Nahisi majukumu mengine yalikuzidi,
karibu once again....lol
 
Kwanza pole sana kwa yaliyokupata. Haukuwa mtu wa kwanza na hautakuwa wa mwisho kukumbwa na tatizo kama hilo. Hili tatizo huwa linatokea sana. Nimeshalisikia mara nyingi sana. Binafsi nafikiri kuna kitu kilichosababisha jamaa kukuacha na kwenda kumwoa mwingine. Kila kitu kinatokea kwa sababu. Inaonyesha umeumia sana japokuwa kwenye maelezo yako unaonyesha kuwa hukuyasababisha haya. Siwezi kukushauri usilie kwa sababu hiyo ni haki hako. Kulia na ni haki yako na lia kadri uwezavyo.

Lakini at the end of the day, unayo haki ya kupata jibu tena toka kwake kwa nini amekufanyia hivyo ikizingatiwa kuwa mlikuwa tayari mmeshakubaliana kuoana. Unaweza shangaa sababu atakayoitoa. Sidhani kama mlikuwa boyfriend and girlfriend tuu. Inaonyesha kama vile tayari kulikuwa na "promise" ya kuoana na ameivunja na kwenda kuoa mwingine bila hata kukupa sababu za kufanya hivyo. Kwa mantiki hiyo unayo haki ya kujua kwa nini amefanya hivyo.

Kwa vile inaonyesha kama vile kulikuwa na promise ya kuoana na ameivunja bila hata ya kukupa sababu, then inabidi ufikirie kwa mapana zaidi. Kuishia tuu kulia na ku-move on, which of course, you're entitled, pia fikiria kama kuna umuhimu wa ku-take further action. Kutegemeana na muda wa mahusiano yenu na pia mambo ambayo tayari ulikuwa umeshayafanya kwa ajili ku-fulfil hiyo promise, unaweza kuchukua hata hatua za kisheria for a breach of a promise to marriage. It may sound crazy lakini hiyo nayo ni option pia. But at the moment, sidhani kama unatafuta ushauri but support. And this is what matter at the moment. Huu ni muda ambao ndugu na true friends matter. They will help you get around this.

I hope you are a strong woman and that you will get through this. Kama alivyosema mdau mmoja alivyosema hapo lia kadri uwezavyo. Ni haki hako. But baada kulia kumbuka kufuta machozi and move on with your life. Just to warn you though that the fact ni mwanaume aliyekufanyia hayo yote, does not mean that wanaume wote wako hivyo. Pia who know may be in future utajikuta mwenyewe unasema duh! heri haya yalitokea.
 
...- Kila unapowaza kuwa "Ninampenda na siwezi kuishi bila yeye", utakuwa unakumbuka mazuri tu uliyoyapata na mliyogawana kabla ya mambo kuharibika. Lakini kama unavyokiri kuwa "mlikuwa na matatizo yenu madogomadogo", ukweli ni kuwa hayakuwa madogo kama ulivyokuwa unafikiria. Yalikuwa makubwa lakini ukavumilia kwa sababu ulikuwa unapenda. Sasa ni wakati wa kuyafikiria haya kwa lengo la kukutoa katika mawazo ya kuwa kulikuwa na mazuri tu. Hii itakusaidia umuone kwa jicho jengine.
...Binafsi nafikiri kuna kitu kilichosababisha jamaa kukuacha na kwenda kumwoa mwingine. Kila kitu kinatokea kwa sababu. Inaonyesha umeumia sana japokuwa kwenye maelezo yako unaonyesha kuwa hukuyasababisha haya...

...dah,...MAMMAMIA na EMT nimeipenda sana leo michango yenu iliyo makini.
bahati mbaya kama asemavyo mwenyewe BJ, anabakiwa na maswali mengi kichwani ni lipi alilokosea
huenda akishajifunza, hatorudia mbeleleni kwenye maisha na mpenzi mpya.

Kunyimwa nafasi ya kuambiwa ukweli ndiko kunakomtatiza, nami naungana nae mkono katika hili.
Kutendwa na mtu unayempenda na kumuamini, kuna uwezekano mkubwa kumuondoshea mtu uwezo wa kujiamini.
Si ajabu mtu akaanza kujiuliza maswali lukuki kasoro zake bila kupata majibu, hivyo kumuathiri kisaikolojia.

Lakini, wachangiaji wengi nao wamedokeza umuhimu wa kuzidisha imani, na kutambua "...likuepukalo lina heri nawe!"
BJ, tambua mateso na machungu uliyo nayo sasa ni nafuu kuliko ungekuwa ndani ya ndoa halafu huyo mwanaume akakutenda hivyo (kuoa mke mwingine bila wewe kutaarifiwa!) Lipi ni bora kwako?

Binafsi nakushauri umshukuru Mw'Mungu wako kwa kusikia dua zako na akakuepushia yaliyo na shari nawe.
Kuendelea kulia na kuilaani bahati ni kumkufuru Mw'Mungu.
 
Samahani Belinda.. Hivi mchumba anaezungumziwa hapa ni yule aliyekuwa ameuteka moyo wako kwenye ile topic yako ya siku za nyuma au huyu ni mwingine? Ni swali tu...
 
duh!!!!

umenikumbusha yule kaka niliyempa moyo wangu akaugeuza choo cha stand!!

i real feel sorry for u my love!! Ila kumbuka imeandikwa " Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana"

Usirudie tena kosa dia kuwekeza kwenye moyo wa mwanadamu, kwakuwa yy hubadilika wkt wowote! bora uwekeze kwa Mungu kwenye hazina isiyoharibika! Yeye hawezi kukuacha maana amesema nimekupa jaribu lakini nimekupa na mlango wa kutokea pia. Jipe moyo mkuu utashinda vita kwa maana imenenwa, Mungu wetu ni Bwana wa vita na alitaka akufundishe jambo.
 
Pole mwali muombe Mungu akupe nguvu uendelee na maisha.Mambo ya mapenzi yanachanganya sana na hasa pale linapotokea kwako kwa unayempenda na kumthamini, ambaye alikuwa anakwambia anakupenda, ambaye ulidhani atakuwa wa mwisho kukuumiza katika dunia hii. but imetokea mpenzi, MOVE ON
 
Kama umeachwa huku ukiwa huna tatizo na msumbufu kwa mwenzako pole sana. Yanawatokea wengi sana. Mapenzi siku hizi kama yapo ya ukweli ni kwa wachache sana. Unaweza ukawa na mtu ukidhani mnaongea lugha moja katika penzi lenu kumbe mwenzio ana lake. Jipe moyo ni aina nyingine ya mungu kukuambia hujapata ubavu wako, afadhali umeachwa sasa kuliko ungekuwa unarudiwa na mwanamke/mwanaume nyumbani hapo mbeleni kama ungeolewa.
Kwa upande mwingine inawezekana umeachwa kwa kuwa mwenzio ameona una matatizo ya kimsingi ambayo amejaribu kwa kipindi kirefu kukurekebisha lakini ikashindikana, so mwanzoni alikuwa anavumilia lakini siku zote katika mambo haya huwa kunakuwa na 'point of no return', yaani amechoka na anaona hawezi kutake it any more na ndo mana amekuacha. Ila ni wewe hasa unayejua ukweli na mara nyingi kama ukweli ni huu wa 2, watu wengi huwa hawajielezi kiuwazi rather huvutia kamba kwao kwamba wao walikuwa nice.

Ol n Ol pole sana kwa hayo. Shukuru mungu kwa kuwa you are gaining an experience to the real now days world you are about to face in later days of ur life. ndo mapenzi ya vijana wa kileo hayo
 
Mfanye rafiki yako wa kawaida, mpigie simu na mwambie kuwa umemsamehe na anza kuwasiliananaye kama mtu wa kawaida. utapona.
 
....changamoto za hapa na pale.... Huenda kwa mwenzio zilikuwa sio changamoto bali matatizo ndo maana kakutema. Tulia hii Dunia haikosi mwenza itakupatia tu.
 
Mfanye rafiki yako wa kawaida, mpigie simu na mwambie kuwa umemsamehe na anza kuwasiliananaye kama mtu wa kawaida. utapona.

urafiki wa nini? Usijaribu kuwasiliana naye, utamsahau tu.
 
Code:
 Kwa faida ya wengi  walio/wanao/watakao/pitia hali kama hii, tungeomba mtumie lugha ya  kiswahili...tunathamini michango yenu...Tafadhali..mtutafsirie na sisi  wengine,

JF is international.na wale wasiojua kiswahili nao tuwatazame kwa jicho la huruma wasiwe wanatoka kapa.....................na wanaojua kiswahili tuwahamasihe kujifunza lugha zaidi ya moja....................we are in a global village................................
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Code:
Mfanye rafiki yako wa kawaida, mpigie simu na mwambie kuwa umemsamehe na anza kuwasiliananaye kama mtu wa kawaida. utapona.

Hivi unamsamehe kwa kosa lipi.......sioni kama kuna ahadi zilitolewa zikavunjwa.....................................nionacho kulikuwa na matarajio ya mwenzetu ambayo njemba haikuwa na habari nayo au haikuyapa uzito..........kwa sababu zozote zile............................
 
....changamoto za hapa na pale.... Huenda kwa mwenzio zilikuwa sio changamoto bali matatizo ndo maana kakutema. Tulia hii Dunia haikosi mwenza itakupatia tu.
atampata ndio ila sio kama yule
 
Hivi ikitokea umempoteza mtu unayempenda unaikabili vipi hii hali?

Yani hata sijui nisemeje, nimechoka kwa mawazo hadi akili kumfikiria sana huyu mtu.
Roho inaniuma na ninakumbuka sana vitu vingi tulivyofanya tukiwa wote. Nahisi nilimpenda sana na kumpa kipaumbele zaidi kuhakikisha tuna penzi imara na lenye muelekeo japokuwa changamoto za hapa na pale hazikukosekana.

Lakini sijui kwa nini amenifanyia hivi? Na hii ndiyo inayonichanganya zaidi akili kwa sababu sipati jibu..Kifupi, ni kuwa ameoa (naomba nisielezee zaidi).

Ooh!..kweli nahitaji ushauri wenu juu ya kuendelea na maisha yangu bila kumkumbuka huyu mtu..japokuwa ukweli ni kuwa siwezi kumsahau 100%!!

I'm so confused, stressed & deeply hurt!!..

and remember in life there are three things
1. things you can fix
2. things others can fix and
3. things God can fix

and in your case you need God to fix your situation , all the time pray pray pray, according to your faith.

God Bless u
 
and remember in life there are three things
1. things you can fix
2. things others can fix and
3. things God can fix

and in your case you need God to fix your situation , all the time pray pray pray, according to your faith.

God Bless u
Apumzike kwa muda ili apone jeraha la moyo alilopata
 
Ndugu yangu asante kwa maono yako. Naomba nikwambie kitu kuwa mimi ni mtu mzima, ingekuwa tumekwaruzana na kuachana wala nisingejisikia hivi. Mimi siyo malaika ila sioni kitu gani nimechangia cha ajabu mpaka kushtukizwa hili jambo. Pia kumbuka angeniambia mbona ningeumia na kujiandaa kiakili hatimae kukubaliana na hilo suala mana nisingeweza kumzuia hata kama nampendaje.

Nimejaribu kutoa short story mana nimeshindwa kuielezea kiundani zaidi kwa vile imetokea karibuni. Nilivyoiweka hii issue ni kuwa nimeshtushwa na jambo la mwenzangu kuoa wakati tulikuwa serious sisi kuoana mwishoni mwa 2011, sijui imenipata. Sasa kama alikuwa na tatizo najiuliza kwa nini hakunishirikisha? kama vile kuniambia tisingeweza kuwa wote au kampenda mtu mwingine na hivyo mimi na yeye basi. simpo as that!

Kweli tulikuwa serious na sijawahi kupinga jambo lolote kuhusu ndoa alivyogusia na tukakubaliana..unajua nini, natamani mwenyewe nipate jibu la hili swali ila sina kwa sababu ukweli anaujua mwenyewe jamaa. Hata kama angeniumiza kuambiwa ukweli ila ungesaidia sana na ningekabiliana nao na maumivu yake.

Shukrani kwa mtazamo wako..


Shukuru mungu amekuonyesha njia, Sio yeye tu watu wengi ikifikia hapo kwenye mambo ya ndoa maelewano yanakuwa mazuri sana na kila kitu mtakubaliana lakini at the end matokeo yanakuwa kama haya wengi wao hawapo serious au mwingine anajuwa kwamba hapa anajibanza ile yule pale ndio atakuwa mke wangu...So shukuru mungu kakufungulia njia mapema so najuwa kwa sasa hivi inauma sana tena sana ila baada ya mda mfupi utasahau kila kitu kitakuwa sawa tu wala usijali......

Pia vile vile kata mawasiliano achana nae iweje kasha owa ndio anakuja na msamaha unataka kumpa msamaha wa nini sasa??Kwamba muendelee au vipi??Angekuwa anakupenda na kukujali angekubali kuowa mwanamke mwingine??

Nakushauri funga huo ukurasa na fungua ukurasa mwingine na mtu mwenye msimamo na uwakika ila huyo achana nae aendelee na huyo mwanamke wake maana hakutakii mema kabisa.........

Pole sana BJ
 
Back
Top Bottom