Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mwananchi akichelewa kufanya malipo au akiharibu kitu hakuna msalia mtume, yaani uwajibikaji ni hapo kwa hapo, sasa kwanini wakitukosesha wao huduma inaishia tu kwenye kumradhi? Uwajibikaji uko wapi?
Kwamba sisi ni waelewa sanaaaaa na hasara na usumbufu wote tunapitia hauna maana yoyote?
"Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza" haitoshi na mnatudhulumu wananchi. Hatupewi huduma hizi kwa hisani, tunazilipia, kwanini hatufidiwi ikiwa wanashindwa kudeliver?
Ukipitia mkataba wa TANESCO Kwa mfano wameweka fidia endapo tu utapata hasara kutokana na hitilafu ya umeme (ambayo na wenyewe kuna urasimu wa kutosha mpaka kuipata, yaani yanawekwa mazingira mtu akate tamaa), lakini je hasara inaishia hapo?
Vipi stock yako ya vyakula wewe mfanyabiashara ambaye ulikuwa unategemea kesho uuze upate lakini umeme unakata stock yote inaharibika? Vipi mfanyabiashara wa askrimu ambaye kesho angeuza akapata elf 20 ya kumsogeza lakini umeme kukatika utamlaza njaa siku hiyo? Vipi huyu kijana aliyekuwa na interview ya mtandaoni mmekata umeme usiku nzima chance yake ya kujikwamua na kujitetea ikapita, mfanya biashara wa vinywaji na barafu unafikiri kumradhi inapunguza vipi machungu yake? Kuna mtu alikuwa anadaiwa ripoti/proposal umeme umekata dili la milioni kadhaa limeyeyuka?
Kwanini tuishie kupewa kumradhi kwa kukoseshwa huduma tunayostahili? Uwajibikaji uko wapi sasa kama mnafanya mnavyojitakia tu, maana mnaweza kuamka na kuamua kufanya lolote, si mnajua mtasema kumradhi na hakuna concequences?
ATCL mnadelay ndege masaa 8 afu hao kumradhi (ashum nimebana pua nikisema hii), imetoka hiyo!
Hapana, hii siyo sawa, tunahitaji utaratibu wa fidia kwa wanachi kwenye huduma zote pale mteja anapokoseshwa huduma anayostahili ili walau afidie hasara na usumbufu aliyoupata.
Mnakata umeme masaa mawili walioathirika wapewe extra units, mwezi mzima maji yanatoka siku mbili, bili ya mwezi ujao walipe half of their bill, umekalisha watu airport masaa nane wapewe discount kwenye next flight, nk, nk, huu ni mfano wa kupunguza machungu kutokana na hasara mnasababisha. Wakuu mtaona kama mambo hayajanyooka!
Ndio maana TANESCO, DAWASA Wizara ya Maji, usafiri wa ndege na treni zinatolewa kimagumashi, kipuuzi na nyingine zinatupa nyongo sababu wanajua HAKUNA KUWAJIBIKA, TUTAOMBA RADHI MAMBO YASONGE!
Nadhani msg itafika sehemu stahiki, KUMRADHI HAITOSHI!