Anachoongea kwa maandishi
"Na nikuambie siri ya watu wanaorudi katika maisha yako. Wanao rudi au unaokubali kurudi. Kwanza, lazima ujuwe kwamba katika level ya watu kudharaulika, wewe uko kwenye level ya deki hiyo. Au ile bamba tunayoweka mlangoni kabla hatujaingia ndani tunafuta miguu yetu tu. Yani anyway hiyo ndio level yako. Kama mtu kakuacha mwaka mzima, hizi ni siku 365. Ina maana wewe, hujajia-upgrade tu? Simu yenyewe kila baada ya mwezi inakuambia 'receive update'.
Software zote zinajia-update na zenyewe ni computerized. Kwa mwanadamu unayekula, maziwa na nyama, hujajia-update siku 365? Mpaka unahitaji watu wako waliopita warudi tena kwenye maisha yako? Mtu tushakushakuonyesha namna gani watu wanapewa breakfast ya baridi asubuhi. Unapewa chapati za baridi, na chai ya baridi.
Ushajua kwamba huyu mtu mimi mwisho wa siku atanipa breakfast ya baridi. Na bado unarudi? Yani, unataka ku-achieve nini? Au unatafuta muujiza gani? Kwamba unahisi, mara ya kwanza hukuona vizuri sasa hivi ndio utaona vizuri? Kwa hiyo, lazima yule mtu yani, the moment umekubali kurudi kwenye maisha yake au umemruhusu yeye arudi kwenye maisha yako, anakuwa kashakuchukulia poa.
Huyu mtu nimempitisha safari ya wanaisraeli, ameona mashimo na mabonde, nimempitisha mbinu zote za vita nimezimaliza kwake, sasa hivi ameniruhusu nirudi kwenye maisha yake, huyu mtu hajidhamini."