Comrade Mpayukaji
Senior Member
- Sep 26, 2007
- 198
- 12
Mkapa hakutukanwa tusi hata moja.Aliambiwa fact kwamba aeleze kifo cha mzee wetu nyerere,aliambiwa aeleze kwa nini ameuza nchi.Unaweza kutoa mfano wa tusi hata moja toka kwa vicent kwenda kwa mkapa?
Hiyo kesi itakuwa kituko tunaanza na Lema, alete ushahidi wake kuthibitisha mahakamani Siyoi ni shoga.
Alama moja wapo ya shoga ni kutoga skio moja kwa Mwanaume najua Lema atapeleka
Hivi kisheria, unaweza kumshtaki LUSINDE kwa matusi aliyomwaga hapa kwenye hii VIDEO? Au kisheria inabaki kuwa ni sehemu ya kampeni? Maana naona kama kwenye kampeni unaweza kupiga hata chini ya Mkanda.
Hivi kuna watu wanaweza kujikusanya na kuchangia kwa mfano gharama kidogo na Tundu Lisu akishirikiana na wanasheria wengine wampandishe huyu jamaa kizimbani?
Hivi kumwaga Matusi mazito mbele ya watoto wadogo kama hao wanaoonekana hapa kwenye Video, katika sheria za Tanzania inaruhusiwa? Kama hapana, kuna uwezekano wa kumshtaki huyu Mgogo wetu?
Naomba Mods muiache hii hapa kwani nimeiweka kitengo cha sheria.
kumshitaki huyo Kilaza ni kuendelea kufuja kodi za wananchi maana huyo akishitakiwa na watu wakasimama kidete anakula miaka...
Haina haja ya kumshitaki ni wa kuachana nae tu maana hapo tayari ushahidi upo wazi, ni sawa na kesi za Wabunge wa CCM na CDM, ni uharibifu wa muda na pesa za walalahoi
hehehehehehe
we kweli henge
hapa hatupo mahakamani mambo ya ushahidi nenda mahakamani ama tafuta crip ya halima mdee usikilize alichokisema juu ya wasila
mimi sina sio CCM wala CDM lakini huwa sipendi sana pale ambapo wanachama wa chama kimoja kujifanya kuwa hawana makosa kulinganisha na chama kingine.
Lusinde anasema
kama ni matusi nae anaweza kwani amechoka kunyamazishwa sasa anajibu mapigo
kwa upande wangu huwezi jibu mapigo kama hakuna aliyekuanza
Kitendo cha Mh Lusinde kuwatukama viongozi na wanachama wa CHADEMA,ajiandae kufikisha kortini kwa kosa la kutukana wana CHADEMA hadharari.Nilipo wasilisha list wa matusi siku ya kwanza,wengi hawakuamini na kuona kama nimetunga thread na kunitukana sana.
Mambo yamedhihirika,Fungua Mh Lusinde Matusi kwenye YouTube
Nawasilisha...
Atashitakiwa na NANI?
Hapana Mkuu, si kutumia hela za Chama au Serikali.
Hapa nataka kujua kama hata Wadau wa haki za binadamu wanaweza kuingilia na kumpandisha kizimbani kwa kumwaga lugha chafu mbele ya watoto wadogo.
Kichama sifahamu kama inaruhusiwa maana kwenye siasa itaanza "uhuru wa kuongea na mambo ya kampeni."
Ndiyo maana nikauliza kwa wataalamu wa Sheria kama hiki kitu kinawezekana ili kumburuza huyu mtu Mahakamani.
Ila ninaamini kuwa kama si leo, basi hata kesho siku itafika mtu atapandishwa kizimbani.
Nadhani Lusinde atakuwa na matatizo ya akili akapimwe. Kwa kitendo alichofanya anatakiwa kushughulikiwa. Kama hizo ndo sera za ccm hatufiki. naona wameamua kuweka hadharani tabia zao sasa
Kiongozi, Sina shaka hata kidogo Lucinde asingekuwa bungeni angekuwa kibaka. Na kuna tofauti kubwa sana kati ya kauli za wana siasa na kauli za vibaka. Kauli alizotoa Arumeru, zinamfunua kabisa ukondoo wake, na kama Mtera waliamini wamemchagua mheshimiwa sasa wakae wakijua wapata kibaka. Hawana mbunge.