Kumtambulisha Nusrat Hanje kama mwakilishi wa BAVICHA huko Nyamagana ni uongo wa wazi na ni kumdanganya Rais Samia

Mpumbavu huridhishwa na upumbavu
 
Kwanini CDM wasiitishe Baraza kuu kusikiliza rufaa zao ili kumaliza hili sakata?ugumu unatoka wapi?pesa au kuna utaratibu mwingine?
 
Yaani mkutano wote wa jana umeonekana ni takataka kabisa. Yaani waandaaji wana mdanganya Rais mchana kweupe kuwa huyu ni mbunge wa Chadema Singida wakati sio mbunge?
Jee kama jambo la wazi vile anadanganywa mangapi ya siri wana mpiga changa la macho?
Kumbe huyu mama mwepesi namna hii? Au wanamdharau kwa vile mwanamke?
Rais mnamgeuza mwenyekiti wa kitchen party? Au kiongozi wa Wamama vikoba group?
 
Mheshimiwa Mbunge kaongea kitu chenye manufaa kwa vijana. Hongera Chadema kwa kuwa na hazina nzuri ya vijana kama huyo.
 
Nadhani kuna kikundi kinamhujumu mama
 
Baraza kuu lipo katikati ya mwaka kma ilivyo miaka yote. Kina Halima walishafutwa uanachama wanacholilia ni baraza kuu kuwarudishia/Yaani kupangua hukumu ya kamati kuu lakini sio eti bado ni wanachama!! Hakuna hicho kitu.

Unadhani bado kuna mtu mjinga kama mawazo tena?

Kafa kwaajili ya chadema familia yake inateseka,huyu kajiongeza
Mawazo hakufa sababu ya CHADEMA aliuawa sababu alitaka kuleta mabadiliko usukumani ambapo miaka 50 ya uhuru bado ni eneo maskini sana. Kama hufahamu alikua CCM na pengine angekuwa waziri leo.... Lakini alipata guilt kuona yye anatoboa hku ndugu zake wanapigika na umaskini.

That's what he died for, and it was worth it. Kuliko angebaki CCM atetee mafisadi
 
Amemchafua Samia wapi?na tangu lini Samia akawa mama yenu chadema?kwahiyo ccm ni baba yenu?
Tatizo Jamii Forum imejaza wajinga katika kipindi cha karibuni. Mijitu mingi, wewe ukiwemo, inajadili ujinga badala ya hoja. Sio wote wanaopita humu wana mahaba ya kipumbavu ya mavyama mnayopoteza muda kuyashabikia. Ungekuwa na akili japo kidogo, ungefahamu kwamba linapokuja suala la urais wa Samia anatazamwa kama kiongozi wa wote, hata wasio na mahaba na vyama. Linapokuja suala la urais Samia sio miliki ya CCM. Ulichoandika hapa ni upumbavu. Turudi kwenye hoja sasa. Kuchafuliwa kwa Samia na Hanje kuko hivi: Maono ya Rais Samia ni kurejesha utengamano katika Taifa hili ambalo miaka mitano iliyopita imeshuhudia mvurugano mkubwa, ikiwemo kuzalishwa chuki za kimakundi ikiwemo kisiasa. Hanje ni miongoni mwa wabunge ambao wamefukuzwa uanachama wa CDM, na ubunge wa akina Hanje ni jambo linalogusa kusiginwa kwa Katiba ya nchi, sasa Hanje anapoibukia kwenye mkutano wa Samia, halafu akatambulishwa na waandaaji wa mkutano kuwa ni mwakilishi wa CDM, akili yako haiona kama jambo hili linachafua azima ya Rais Samia kuleta uponyaji wa mioyo kwa makundi ya kisiasa?
 
Huwezi kudanganywa jambo unalojua ukweli wake.

Lakini sasa kwanini Chadema hawakupeleka wawakilishi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…