WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Kitu kinachoniumiza kichwa hasa kwenye tatizo la umeme ni kujaribu kuelewa ni nani mwenye "suluhisho la kudumu" la kumaliza hili tatizo sugu kwa kila awamu ya urais hasa awamu hizi mbili za mwisho.
Rais wetu keshasema yeye hana uwezo kumwambia Mungu anyeshee mvua mabwawa yajae, umeme uzalishwe.Fair enough na ni kweli.Kwanini tunadhani rais ndio mwenye "ufunguo" wa kufungua mlango/milango ya utatuzi? Je hiyo milango ni ipi, iko wapi?
Nilimsikiliza kwa makini Mh John Mnyika akielezea kwa ufasaha tatizo lilivyo na baadhi ya njia za kulitatua na kwamba inahitajika ushirikiano baina ya wadau wote - serikali, kambi ya upinzani na hata sekta binafsi kukaa pamoja na kuweka vichwa pamoja kupata suluhu. Hapo nilijiuliza, kwanini hili halifanyiki?
Nimekuwa pia nikisikia mara kwa mara serikali ikilaumu upinzani kwa kutokutaka kutambua mazuri yanayofanywa na serikali na badala yake wanapinga tu.Je ushirika huu wenye manufaa kwa watanzania badala ya vyama, ushirika unaohitajika wakati huu kuliko wakati mwingine wowote si ndio ungeonyesha namna gani vyama vya siasa vinavyoweza kuweka tofauti zao kiitikadi na kuweka ajenda ya taifa mbele na maslahi ya wananchi juu ya maslahi binafsi ya wanasiasa?
Hivi ndugu zanguni, hivi vyama vya siasa viko kwa manufaa ya nani? Ikumbukwe kwamba wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa ni wachache sana hawazidi hata nusu ya watanzania wote wanaoathirika na hili tatizo la umeme.Je serikali inawatendea haki gani wale wasio wanachama wa chama chochote wanaolipa kodi zao wakitarajia huduma mbalimbali ikiwemo umeme.
Naombeni mnisaidia kupata majibu ya hayo maswali na labda wanasiasa na viongozi wa serikali wanaopita humu JF nao watusaidie sisi wananchi tuliokaa pembeni tukiangalia hili igizo kuelewa.
Asante kunisoma na pia kutafakari na hata kuchangia.
ANGALIZO: Ukiona mada inakukera basi potezea tu badala ya kuweka hasira na maneno yasiyo ya lazima.